Mjukuu wa kigogo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2023
- 445
- 1,094
Binafsi Mimi ni kati ya wadau wa elimu katika Taifa langu la Tanzania.Napenda kutumia wasaa huu kuushauri uongozi wa juu wa kanisa la Anglikana ngazi ya Taifa kuhusu Shule ya wasichana ya Bunda girls ambayo wao ni wamiliki wakuu.
1. Eneo la Taaluma
Katika eneo hili Taaluma ya Shule bado hairidhishi ukilinganisha na hadhi ya shule husika kuwa 'private'.Nitatoa mfano katika shule nyingi za umma maarufu kwa jina la shule za kata ambako wanafunzi takribani 300 hufanya mtihani wa Taifa kidato cha nne ambapo katika hao watahiniwa waliofanya mtihani unaweza chukua matokeo ya kundi la watahiniwa wanaozidi 100 na usipate daraja la nne(division four).Cha kushangaza shule ya Bunda girls watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne huwa ni chini ya 40 lakini bado utapata wanafunzi wenye daraja la nne wengi tu.(Teaching load ndogo bado matokeo mabaya)Hapa kuna shida kubwa sana. Kwa shule yenye status ya kuitwa private hayo siyo matokeo !Hebu jifunzeni kwa shule za Roman Catholic namna wanavyoendesha shule zao.Nendeni kowak girls hapo rorya ambayo ni private kama nyie mlinganishe matokeo!!Eneo hili liangaliwe kwa kina maana mbeleni kuna anguko kubwa la kitaasisi! Sasa hivi hata division one nzuri unazipata kwenye shule za kata ambazo kwa walio wengi huziona kama shule za watoto wasio na chochote kichwani.(Ukitaka kuhakiki hili chukua matokeo ya mitihani wa kidato cha nne miaka mitatu iliyopita au minne na ulinganishe na matokeo ya shule za kata ndani ya halmashauri utaamini)
2. Malezi ya wanafunzi (hususan wagonjwa)
Wazazi wanalipa ada pamoja na pesa ya matibabu lakini Kuna jambo linashangaza.Mara nyingi mtoto akiugua mzazi huitwa kwa kupigiwa simu akamchukue mtoto na mbaya zaidi hili linaendana na kukuta mgonjwa (mwanafunzi)akiwa chini ya uangalizi wa wanafunzi wenzake!!!Lakini pia watoto wenye bima mnawachangisha pesa za matibabu sawa na wasio na bima kwa logic ipi?Awali hili suala halikuwepo ila limekuja kuibuka ghafla majuzi.Hatujui nani yupo nyuma ya hii kadhia!
3. Kuwapa mateso ya kisaikolojia wanafunzi
Kipindi cha mitihani ya Taifa inapoelekea kuanza baadhi ya walimu huanza kutisha watoto ambao hawajakamilisha ada kwa maneno ambayo yanawatoa katika concentration ya mtihani.Hapa mwalimu ongea na mzazi,mwanafunzi usimweleze chochote.Maneno kama 'hamtafanya' mtihani au mkifanya mtihani matokeo yenu hayatatoka ni kuwatengenezea taharuki na kuwaathiri kisaikolojia.Hapo mtoto atafanya mtihani ili mradi tu.Mnakuwa sasa mnaviolate haki za watoto kupata ufaulu mzuri!
Comedy kuhusu mahafali
Ndani ya kipindi cha kama mwezi mmoja na nusu mmehimiza wazazi kuchangia gharama za mahafali.Ili kurahisisha hilo mkaunda na group na mwitikio wa wazazi kuchangia umekuwa mkubwa.Ghafla mmetoa tamko mtoto ambaye hajakamilisha ada hafanyi mahafali hata kama kakamilisha mchango wa mahafali.Hapa pia napata utata na maswali yangu kuhusu hili ni kama ifuatavyo:
i-Ilikuwaje suala la mahafali mkawahusisha mpaka wanafunzi ambao hawakukamilisha ada huku mkijua hawatashiriki na kupokea pesa zao badala ya waliokamilisha tu?Kwa nini msingesema tu kwamba wanaodaiwa hawatashiriki?Leo Kuna watoto washaalika ndugu toka maeneo mbali ya nchi kuja kusherehekea mahafali na washafika, halafu ghafla wanaambiwa hawatashiriki hayo mahafali,je mnakwepaje lawama Kwa usumbufu huu?Tukitumia neno 'utapeli' hapa tutakuwa tumekosea?Haya kweli ni maamuzi ya walimu wengi au mtu mmoja tu bila kushirikisha wenzake?
ii-Haya kuna wanaodaiwa ada na tayari wamelipa pesa ya mahafali na mmetoa tamko hawatashiriki mahafali.Je huo mchango wa mahafali walioutoa utapelekwa kwenye replacement ya ada? Kama jibu ni ndiyo je ni halali kulipia ada kupitia m-pesa,Airtel money,Tigo pesa na Halopesa kwenda kwenye simu ya mwalimu?Na kumbukeni zilitumwa na za kutolea!Staff nzima kabisa mmekosa smart person kuliweka sawa hili suala?
Ushauri sasa Kwa dayosisi;
1. Kanisa lina watu wengi makini,watumieni katika kuisimamia shule imeanza kutoka kwenye njia kuu.
2. Tathmini za matokeo ya mitihani ya kitaifa katika shule ziwe na tija na zisiwe zinafanyika Kwa mazoea.
3. Viongozi wa kanisa zuieni pia majungu.Mwaka juzi shule ilipoteza mwalimu mahiri wa kiswahili(Madam Yunice)Kwa majungu lakini pia mwalimu mmoja wa basic mathematics alinusurika dakika za jioni.Majungu huweza kupoteza walimu mahiri na kuleta wasio na uwezo.
4. Suala la kulipia ada liwekeni vizuri.Mnasema mwanafunzi anaruhusiwa kulipia awamu nne kwa mwaka.Lakini inashangaza baada tu julai kuisha wazazi huambiwa kumaliza michango yote na kisha wanafunzi huanza kufukuzwa.Hii pia inaleta mkanganyiko.Ni Bora mkasema wazi ada italipwa Kwa awamu mbili tu!
5. Utunzaji wa taarifa za kifedha bado haujakaa sawa.
Hili Eneo liboresheni kuondoa utata.Bado kunakuwepo na changamoto.Taarifa unayoitoa Kwa mhasibu kuhusu malipo Kuna nyakati inakuwa tofauti na ofisi kuu! Hapa wekeni utaratibu wa kutunza kielektroniki!
6.Pia mkuu wa shule apewe mamlaka kamiliya kiuongozi anapokuwa anatetea hoja.Sentensi kama "wenye shule ndio wamesema" zinaleta ukakasi sana.Anakuwa kama shadow headmistress!
Pongezi
Ninalipongeza kanisa Kwa mambo mawili kwenye shule
1.Kuondoa ukabila
2.Kuwa na uzio
Asanteni....
NB:Kuna taarifa kesho tarehe 27.11.2024 mtaanza rasmi kufukuza wanafunzi ambao hawajakamilisha ada ili wasoshiriki mahafali,hakikisheni mazingira salama pindi watakapokuwa safarini