mimi sijaona kosa la waumini wa gwajima kuadhibiwa kwa sababu gwajima mmoja tu amekemea utekaji na mauaji. kosa la gwajima lipo wapi? basi tuseme amekosea, sasa kosa la waumini wake liko wapi hadi wazuiwe kufanya haki yao ya kikatiba ya kuabudu? muumini aliyepo mwanza, anazuiwa kuabudu ambayo ni haki ya kikatiba, yeye hajahubiri siasa wala chochote, anaadhibiwa kwa kosa lipi sasa? kwanini tunaatack makanisa na sio watu ambao nao lazima wapelekwe kwenye vyombo vya sheria?
1. gwajima kabla ya kuadhibiwa alipewa haki ya kusikilizwa?
2. ufufuo na uzima kabla ya kufutwa usajili walipewa haki ya kusikilizwa?'
3. kukemea utekaji na uuaji ni kosa?
4. Je? Tanzania hakuna watu wanatekwa na kuuawa?
5. Mdude, soka, kibao, na wengine wengi, hawajatekwa na kuuawa wengine?
mwenye jibu aniambie.