Kanisa la Wasabato Mnapaswa Mkosoe maovu ya serikali zaidi kuliko kukosoa wenzenu wa Roman Catholic

Kanisa la Wasabato Mnapaswa Mkosoe maovu ya serikali zaidi kuliko kukosoa wenzenu wa Roman Catholic

Mungu alishaliona ilo ndomana akaandika haya. Lenyewe linadhan linanguvu na haliitaji kitu.

Ufunuo wa Yohana 3:15-18
[15]Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

[16]Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

[17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

[18]Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
Umeaanza mahubiri 😊
 
Kanisa Katoliki limetajwa wapi hapo?
Unaona sasa.
Yesu walimuuliza mbona huwa unaongea kwa mafumbo na mifano, aliwajibuje?

Luka 8:9-10
[9]Wanafunzi wake wakamwuliza, Maana yake nini mfano huo?

[10]Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe.

Unasubiri alitaje jina katoliki??
Ngoja nikuletee maandiko ya kanisa katoliki
 
Sidhani kama uko sahihi mkuu, SDA siyo chama cha kisiasa, kwanini iingilie mambo ya kisiasa? Pia kwa msabato wa kweli haruhusiwi kujiingiza kwenye siasa!
Kwahiyo msabato kumkosoa mroma ni sahihi maana wote wako kwenye taasisi za kidini.
hawako sahihi pia kuwakosoa roman catholic

Maana imeandikwa 'usihukumu usije ukahukumiwa'
 
Sasa mbona hamjihusishi na siasa kama mwili ma roho vyote ni vya Kristu, na Kristu alijihusisha na siasa?
Yesu alipojaribiwa na shetani aliambiwaje
Shetani alimwambia ukinisujudia malizooote na serikali na falme ntakupa.
Hakuwa anamdanganya,
Serikali na mifumo yote unayoiona the whole world order,ni mpangilio wa ibilisi.
Na ndomana kristo alisema ataileta mji na nchi mpya,haya yote hayana budi kuharibiwa kwakuwa ni mfumo wa ibilisi
 
Unaona sasa.
Yesu walimuuliza mbona huwa unaongea kwa mafumbo na mifano, aliwajibuje?

Luka 8:9-10
[9]Wanafunzi wake wakamwuliza, Maana yake nini mfano huo?

[10]Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe.

Unasubiri alitaje jina katoliki??
Ngoja nikuletee maandiko ya kanisa katoliki
Hapo anawaongelea Wasabato.
 
hawako sahihi pia kuwakosoa roman catholic

Maana imeandikwa 'usihukumu usije ukahukumiwa'
Kukosia sio kuhukumu.

Ufunuo wa Yohana 3:19
[19]Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

Sasa ww unadhani mungu atashuka akuambie kwa upepo wakisulisuli.
Yeye hutumia binadamu kukusahihisha.

Ukiona unanafasi yakusahihishwa na Mungu basi jua ungali anakupenda
Ila ukiona hakuambii kitu basi alishakizira.

Waebrania 12:5-6
[5]tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana,
Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana,
Wala usizimie moyo ukikemewa naye;

[6]Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi,
Naye humpiga kila mwana amkubaliye.

Tatizo mnatetea ukatoliki kuliko biblia mnayodai mnaiamini
 
Yesu alipojaribiwa na shetani aliambiwaje
Shetani alimwambia ukinisujudia malizooote na serikali na falme ntakupa.
Hakuwa anamdanganya,
Serikali na mifumo yote unayoiona the whole world order,ni mpangilio wa ibilisi.
Na ndomana kristo alisema ataileta mji na nchi mpya,haya yote hayana budi kuharibiwa kwakuwa ni mfumo wa ibilisi
Mpaka hapo alishajihusisha na siasa.
 
Mathayo 16:18
Mathayo 16:18
[18]Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

[emoji2][emoji2] Kwaio hapo ndipo mlipodanganywa kuwa ilo kanisa no kanisa katoliki
Soma biblia alafu uone kanisa gani petro alilianzisha.?
Petro alianziwha kanisa la mitume.
Ambalo baadae lilipingwa nakuuawa na roman.
Wakatubi wakaita makanisa majina ya mitume waliowaua ili dunia izani walitubu kweli.
 
Wewe unatafuta like na kusifiwa kupitia mgongo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Hayo malalamiko yako siyo sehemu ya kazi ya Kanisa unasema Yesu alikemea leta mfano wa aya Yesu alikemea hapa tuone wapi alikemea

Yesu alikuja ulimwenguni wakati Taifa lake la Kiyahudi likiwa chini ya ukoloni wa Warumi na walikuwa wakiwatesa hasa lkn kauli yake ilikuwa Ya Mungu mpeni Mungu na Kaisari mpeni kaisari wewe unasema alikemea leta aya yako

Warumi kupitia mtume Paulo anasema mamlaka zote zinatoka kwa Mungu yeye ndiye huziweka na kuziondoa unafikiri Kanisa halijui hili

Waadventista wanapitia changamoto ya kunyimwa haki yao ya kuabudu siku ya jmosi tumeshuhudia mara kadhaa hata utumishi kupanga usaili siku ya jmosi nani umewahi kusikia akiwatetea zaidi ya kufanyiwa kejeli lkn limekuwa likijitahidi kuwasilisha hoja zao bila kelele kama hao wengine

Ukitaka kupata sifa tafuta njia nyingine siyo kulisema hovyo Kanisa la Waadventista wa Sabato
 
Mathayo 16:18
[18]Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

[emoji2][emoji2] Kwaio hapo ndipo mlipodanganywa kuwa ilo kanisa no kanisa katoliki
Soma biblia alafu uone kanisa gani petro alilianzisha.?
Petro alianziwha kanisa la mitume.
Ambalo baadae lilipingwa nakuuawa na roman.
Wakatubi wakaita makanisa majina ya mitume waliowaua ili dunia izani walitubu kweli.
Kwani hiyo Biblia imetokea wapi ? Mbona unajinadi sana bila kujua imetoka wapi ?
 
Kwani hiyo Biblia imetokea wapi ? Mbona unajinadi sana bila kujua imetoka wapi ?
Mmedanganywa biblia imetoka katoliki sio?
Mungu aliiandika biblia kupitia mikono ya watakatifu wake
Petro ,marko daudi, paulo.
Ila mkikaa kanisani mnadangangwa roman ndio walioandoka biblia .
 
Back
Top Bottom