Kanisa la Wasabato Mnapaswa Mkosoe maovu ya serikali zaidi kuliko kukosoa wenzenu wa Roman Catholic

Kanisa la Wasabato Mnapaswa Mkosoe maovu ya serikali zaidi kuliko kukosoa wenzenu wa Roman Catholic

Mungu hajawahi kubariki siasa
Na wala hatakaa awahi
Siasa ni michezo michafu yote.
Uongo,fitina na uzushi,mauaji na kila baya unalilojua.
Siasa iporadhi ikubali uchafu wajinsia moja na mengineyo .
Mungu kamwee hatakaa ajiingize
Na wala kanisa la kweli la Mungu halitakaa kamwee lijihusishe.
Kwanza kanisa la kweli linachefukwa na siasa

Sasa mbona hata huko makanisani kwenu mnatumia siasa kupata viongozi au wewe siasa unaielewa vipi?yawezekana hata neno siasa hulielewi mana yake.
 
Sasa kazi ya dini ni nini ? Ikiwa viongozi wa serikali wanatenda unyama, wanaiba kura na nyinyi mnaona hilo msiseme eti sio kazi yenu [emoji849]

Mnamsubiri mbowe awasemee
Ndo mana nakuambia kuna mgawanyo wa majukumu, hayo ya wizi wa kura tupaze sauti mimi na wewe,

Viongozi wa dini zote hii nchi sidhani hata kama wanafika 100k, tunabaki na watu 59.9M wa kusemea hayo masuala, kweli sisi tutashindwa kusema hadi tuombe viongozi wa dini waje waseme ?
 
KANISA LA WASABATO MNAPASWA MKOSOE MAOVU YA SERIKALI ZAIDI KULIKO KUKOSOA WENZENU WA ROMAN CATHOLIC.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mimi nimezaliwa kwenye Usabato, nimekua na kulelewa kwenye Usabato. Kimsingi Mimi ni Msabato ingawaje ni Mtibeli kiasili. Yaani tuseme ni Mtibeli aliyezaliwa katika Dhehebu la kisabato. Sasa sisi Watibeli ni Watu wa kusema ukweli hata kama unatugusa wenyewe. Hatunaga ushabiki.

Licha ya Wasabato wengi kubobea katika Mafundisho ya biblia na dini yao lakini wanaupungufu mkubwa wa kuisema Kweli hasa linapokuja suala la siasa, utawala na serikali.

Ni ngumu sana kusikia Kanisa la Sabato likikemea maovu ya Serikali. Kwa upande wangu sijawahi kusikia. Ila wakati huohuo ni rahisi kusikia kanisa la Wasabato wakiipongeza serikali na kuiombea. Hapa ndipo Watibeli tunapoona kuna tatizo fulani la Unafiki.

Wasabato wamefundishwa kutojihusisha na siasa. Kanisa pia moja ya sera zake ni kutojihusisha na siasa.

lakini Wasabato ni mabingwa duniani wa kukosoa dini zingine hasahasa Ukatoliki ambao ndio Mama wa Ukristo. Hata biblia inayotumika ni Wakatoliki walioiratibu na kuipanga. Ukisema bila ukatoliki hakuna biblia utakuwa upo sahihi kwa sababu Biblia ilikusanywa na wakatoliki. Nisitoke nje ya mada, na wala Wakatoliki wasidhani nawatetea hapa.

Hakuna kanisa lolote au dini yoyote itakayokuwa ya haki na sahihi zaidi ya ile inayotetea haki na kuikosoa serikali. Hakuna dini wala dhehebu hilo.

Manabii wote, mitume wote, Makuhani wote, Waamuzi wote walijihusisha na siasa hasa pale mambo yanapoenda Mrama au viongozi wa kisiasa wanapogeuka wadhalimu au kutenda maovu.

Yesu mwenyewe ambaye ndio msingi wa ukristo aliikosoa serikali na vyombo vya Dola.

Sasa iweje Wasabato wanajitoa katika wajibu huo.

Utatakaje Haki bila kujiingiza kwenye siasa ? How?

Yaani uwaambie waumini wako waache dhambi wakati msingi wa dhambi unabebwa na siasa.

Waumini watashikaje amri za Mungu bila kukemea viongozi wao wa kisiasa? how?

Amri kama ya kufanya kazi ambayo ni moja ya amri za Mungu, Muumini anafanya kazi kwenye serikali yenye mazingira ya mengi ya rushwa, wizi, ufisadi, dhulma alafu muda huohuo Kanisa halikemei serikali ikiwa na baadhi ya viongozi madhalimu, hivi kweli inakuja Akilini?

Unasema lengo la kanisa ni uinjilishaji,haya utafanyaje uinjilishaji kwa Watu na jamii inayodhulumiwa?
Badala ya kusaidiana na jamii kukabiliana na baadhi ya viongozi madhalimu ninyi mnawatia moyo wakijinga kuwa ati tumaini lipo wakifika Mbinguni kwani duniani kuna dhiki.

Wasabato tumekuwa kama Wamishenari walioungana na makoloni kututawala na kulainisha mioyo yetu kwa aya za kuokoteza.

Tumekuwa Machawa wa Watawala.

Haya mnahubiri neno la kweli, lakini kweli gani yenye mipaka? Kweli inayohusu Watu duni, dhalili, Waumini wasio na Mamlaka ndio kweli?

Kweli inayowaogopa Watawala na serikali? Hiyo ni kweli gani hiyo?

Tumekalia Sabato
Alama ya mnyama!
Sijui Papa!

Kama mnashindwa kuikosoa serikali mnayoiona mtawezana na Mambo ya Mnyama au huyo Papa kweli?

Tuacheni kuwa Machawa wa serikali!

Mbona Wakatoliki na Walutheri mabaraza yao kila mara hutoa matamko ya kukosa serikali pale wanapoona unakosea?

Dini ya kweli ni ile inayopigania Haki. Na huwezi pigania haki bila kuigusa siasa na serikali kwa sababu hao ndio wanahusika na mambo ya kutoa Haki.

Tusiwapotoshe waumini kuwa ati ufalme wa duniani hatuhusiani nao ilhali ibiblia iko wazi kuwa sisi ni Watu wa duniani na asilimia mia moja tunautawala huku duniani. Huko mbinguni sio kwetu na hata biblia yenyewe inakiri hilo. Ndio maana hata tukienda huko kama biblia isemavyo hatutakaa milele isipokuwa miaka elfu tuu.

Acha nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Unakosea sana, kwamba Katoliki ndo walioandika Biblia?? Elimu yako ya dini ni dhaifu. Roma ndo ilificha Biblia katika kipindi chote cha zama za giza, mpaka uprorestanti ulipoingia ndo Biblia ikaachiwa huru kusomwa. Tambua utume wa kanisa mkuu.
 
Ndugu, vijikanisa vidogo vidogo visivyo na mifumo hasa hivi vya kipentekoste ni tatizo, bila kuisifia CCM wanaweza kujikuta wanakosa leseni za biashara zao, nukuu yaliyomkuta Mbarikiwa na kanisa lake kwa kusimamia haki. Kumbuka yaliyomkuta Kakobe baada ya kuihoji CCM, kumbuka yaliyotaka kumkuta mtumishi Mwingira aliposema Lissu hakamatiki ni sauti kutoka mbinguni tuifuate..

Kongole kwa kanisa katoliki kukupita maskofu wenu TEC, nyie ni vinara wa haki - wengine si kwamba hawataki wanataka ila wanaogopa tonge litadondoka.

Wasabato ni taasisi kubwa iliyosambaa ulimwenguni acha kufananisha na hizi local churches
 
Mimi sio msabato, ila sipend hii issue ya wanasiasa kugeuza viongozi wa dini ni wanasiasa,
Itafika kipind cha uchaguzi TEC waseme wao hawaridhishwi na CCM bali wamependa sera za ACT ndio nzuri, kisha wasabato wakasema za CHADEMA ndio nzuri, KKKT wakazipenda za CCM,

Utakuta tunaanza kuchaguana kwa misingi ya dini, hatuna uhaba wa wanasiasa Tz kiasi cha kuanza kulazimisha viongozi wa dini wawe wakosoaji/wasifiaji wa serikali, wabaki kuwa observers wa karibu,

Tukiwaingiza sana kwenye siasa kuna siku tutalia
Ukisikia kujiongeza kwa kijinga ndio huku sasa,

"Yani TEC waseme hawaridhishwi na CCM au sera za ACT"
[emoji16][emoji16][emoji16]

Kama umeelewa kuingilia siasa kwa namna hii basi hujamuelewa Robert.

Yani kama hivi kwenye muswada mpya wa uchaguzi, Raisi ateue tume ateue watendaji, yeye pia ni mgombea alafu uite uchaguzi huo ni wa haki ???

Alafu viongozi wa dini muitwe mtoe maoni alafu useme sisi hatuingilii siasa ???
 
Sio kazi ya kiongozi wa dini kumpangia mwana siasa namna ya kuendesha siasa zake na ndio maana hiyo ikaitwa siasa na nyingine ikaitwa dini kwa maana ni vitu viwili tofauti.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Dini ni siasa ya kale,huoni primitive religions kama uislam wanalazimisha siasa ya kale dini iendelee kutawala katika ulimwengu wa sasa.
 
Ndo mana nakuambia kuna mgawanyo wa majukumu, hayo ya wizi wa kura tupaze sauti mimi na wewe,

Viongozi wa dini zote hii nchi sidhani hata kama wanafika 100k, tunabaki na watu 59.9M wa kusemea hayo masuala, kweli sisi tutashindwa kusema hadi tuombe viongozi wa dini waje waseme ?
Bado siasa huwezi ikwepa, kwenye familia kuna siasa, hata huko kanisani kuna siasa viongozi mnawapataje kama sio kwa kura ?? Hiyo sio siasa
 
Tangu nazaliwa wasabato wanahubiri ishu ileile Mara mnaabudu sanamu Mara Freemason Mara duh! Sijui Ellen G mweupe aliwafundisha hivyo????

Yaaani,hadi unajiuliza huo upendo wanaofundisha makanisani mwao unamaana gani kama wao kutwa wanatangaza chuki dhidi ya rc,huwa na wambia mpinga kristo namba moja ni dini isiyomkiri kristo kama mwana wa Mungu.
 
Wasabato waamini dhehebu lao ni la kweli.na kwenye kweli kuna Haki.
Swali linakuja, kwa nini hawakemei uovu ambao unafanywa na serikali?
Huo ndio msingi wa swali.

Ukasema kunachangamoto ya kusali jumamosi, sawà!
Sasa tuambie utapataje haki ya kusali jumamosi na utaomba haki hiyo kwa namna ipi ikiwa unaamini utawala wa dunia ni washetani? Kwamba unamuona Shetani haki ya kumuabudu Mungu wako?

[emoji28][emoji28] akikujibu nitag
 
Unakosea sana, kwamba Katoliki ndo walioandika Biblia?? Elimu yako ya dini ni dhaifu. Roma ndo ilificha Biblia katika kipindi chote cha zama za giza, mpaka uprorestanti ulipoingia ndo Biblia ikaachiwa huru kusomwa. Tambua utume wa kanisa mkuu.
Shughuli ya kuiunganisha Biblia na kuanza kuitafsiri ilifanyika chini ya Roma ata ukiwampagani Ili lipo wazi kabisa kulitambua maana ni Roma ndiyo ilikuwa na nguvu chini ya wafalme la Akina Costatine/Costatino waliousamba ukristo

Na kanisa la kwanza kujitenga kutoka Roma lilikuwa Lutheran na waliichukua Biblia iliyokwisha andaliwa na wazee waroma Bali Waruthel kunavitabu walivitoa Waruthel wenyewe wanalijua hilo
 
Bado siasa huwezi ikwepa, kwenye familia kuna siasa, hata huko kanisani kuna siasa viongozi mnawapataje kama sio kwa kura ?? Hiyo sio siasa
Hapa tunaongelea siasa za CCM na CHADEMA na ACT, sio hizo za nyumbani sijui uchaguzi wa KKKT,

Viongozi wa dini wabaki kurekebisha watu waishi kadri apendavyo Mungu ila sio kuingilia siasa za nchi, mwanzoni tutaona raha, ila m nakuambia itafika stage watakuwa na nguvu sana halafu wataanza kuipora madaraka serikali hususani dini zenye wafuasi wengi,

Itakuwa ukienda kinyume na RC au Waisalam bas hutoboi kwenye siasa, itakuwa full kuwalamba nyao watu wa dini,

Sasa hapo ndio itakuwa mwisho wa demokrasia
 
Shughuli ya kuiunganisha Biblia na kuanza kuitafsiri ilifanyika chini ya Roma ata ukiwampagani Ili lipo wazi kabisa kulitambua maana ni Roma ndiyo ilikuwa na nguvu chini ya wafalme la Akina Costatine/Costatino waliousamba ukristo

Na kanisa la kwanza kujitenga kutoka Roma lilikuwa Lutheran na waliichukua Biblia iliyokwisha andaliwa na wazee waroma Bali Waruthel kunavitabu walivitoa Waruthel wenyewe wanalijua hilo

Katoliki ilianza kugawanyika kati ya kanisa la magharibi(Roman Catholic) na la mashariki(Othrodox) huyo mlutheri alijitoa katika kanisa la mashariki RC.
 
Unakosea sana, kwamba Katoliki ndo walioandika Biblia?? Elimu yako ya dini ni dhaifu. Roma ndo ilificha Biblia katika kipindi chote cha zama za giza, mpaka uprorestanti ulipoingia ndo Biblia ikaachiwa huru kusomwa. Tambua utume wa kanisa mkuu.

Utakuwa umenielewa vibaya.

Waandishi wa vitabu vya biblia majina yao yapo karibu kwa kila kitabu.
Japo sio vitabu vyote.
Lakini walioviunganisha ni wakatoliki na kuvipa jina moja Biblia(yaani mkusanyiko wa vitabu) na vipo vitabu vingine vingi havikuunganishwa na hao wakatoliki.

Biblia unayoiona imewekwa kwa utashi wa Wakatoliki kuanzia kitabu cha mwanzo mpaka ufunuo na vipo vitabu vingine ambavyo havijawekwa.
 
Back
Top Bottom