Kanitapeli na katuma watu wanivamie. Nimchukulie hatua gani?

Kanitapeli na katuma watu wanivamie. Nimchukulie hatua gani?

mr pipa

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2021
Posts
3,074
Reaction score
6,472
Huyu jamaa yangu kamtuma mtu kunifanyia utapeli nikamstukia baada ya kushindwa hizo mbinu kaandaa watu wavamie nyumban kwangu waniibie na hizo taarifa nazipata kupitia watu wake wa karibu.

Je, nichukue hatua gani kwa mtu kama huyu?
 
Huyu jamaa yangu kamtuma mtu kunifanyia utapeli nikamstukia baada ya kushindwa hizo mbinu kaandaa watu wavamie nyumban kwangu waniibie na hizo taarifa nazipata kupitia watu wake wa karibu je nichukue hatua gani kwa mtu kama huyu ??

Achana naye; ni mwendawazimu tu anayeweza kufanya hayo unayosema, na mwendawazimu hawezi tekeleza anayosema!

Swali:

Huyu ndugu hamna ugomvi naye unaohusu mbususa!?!!!!
 
Huyu jamaa yangu kamtuma mtu kunifanyia utapeli nikamstukia baada ya kushindwa hizo mbinu kaandaa watu wavamie nyumban kwangu waniibie na hizo taarifa nazipata kupitia watu wake wa karibu je nichukue hatua gani kwa mtu kama huyu ??

Ili kutatua tatizo ni vyema kujiuliza haya:
1: Tatizo husika lina madhara kwako?
A: Hapana: achana nalo
B: Ndiyo: tafuta ufumbuzi

2: Je unaweza kupata ufumbuzi wa tatizo husika.
A: Hapana: jifunze jinsi ta kuishi nalo bila kukuletea madhara
B: Ndiyo: anzisha utaratibu wa kutatua tatizo lako usiokuletea madhara

3: Kama ukiamua kutafuta ufumbuzi
Hakikisha unapata taarifa sahihi kulingana na tatizo husika na kufanya maamuzi. Baada ya kukusanya taarifa hizi unaweza kufanya maamzi ya:
A: Kuonana na mhusika wewe binafsi ili muyaongee.
B: Kukutana nae mhusika chini ya watu wenye ushawishi, kuheshimika, wenye busara zao au viongozi ndani ya jamii.
C: Kulingana na uzito unaweza kuhusisha vyombo husika vya serikali.
 
Mfuate umwambie ukweli, na umwambie kabisa kwamba kila mtu anajua kwa missions zake anazotaka kukufanyia. Lolote baya likikupata litakuwa mikononi mwake.

Hapo mbona atakuwa mlinzi wako. 😄 Mtoto mdokozi mpe akutunzie hela.
Cha msingi pata hata kakaratasi kutoka polisi, ili asije kukugeuzia ubao kuwa umeenda kwake kumtishia maisha.
 
Huyu jamaa yangu kamtuma mtu kunifanyia utapeli nikamstukia baada ya kushindwa hizo mbinu kaandaa watu wavamie nyumban kwangu waniibie na hizo taarifa nazipata kupitia watu wake wa karibu je nichukue hatua gani kwa mtu kama huyu ??
Hao Jamaa zake wako tayari kutoa ushahidi pasi na shaka mahakamani? Tuanzie hapo Kwanza
 
Kamfungulie kesi ya Kula njama chini ya kifungu cha 384 sura 16 R.E 2022 ila uwe na ushahidi
 
Huyu jamaa yangu kamtuma mtu kunifanyia utapeli nikamstukia baada ya kushindwa hizo mbinu kaandaa watu wavamie nyumban kwangu waniibie na hizo taarifa nazipata kupitia watu wake wa karibu.

Je, nichukue hatua gani kwa mtu kama huyu?
Mtumie watu na wewe wamvamie.

Dawa ya moto ni moto
 
Back
Top Bottom