Huyu jamaa yangu kamtuma mtu kunifanyia utapeli nikamstukia baada ya kushindwa hizo mbinu kaandaa watu wavamie nyumban kwangu waniibie na hizo taarifa nazipata kupitia watu wake wa karibu je nichukue hatua gani kwa mtu kama huyu ??
Ili kutatua tatizo ni vyema kujiuliza haya:
1: Tatizo husika lina madhara kwako?
A: Hapana: achana nalo
B: Ndiyo: tafuta ufumbuzi
2: Je unaweza kupata ufumbuzi wa tatizo husika.
A: Hapana: jifunze jinsi ta kuishi nalo bila kukuletea madhara
B: Ndiyo: anzisha utaratibu wa kutatua tatizo lako usiokuletea madhara
3: Kama ukiamua kutafuta ufumbuzi
Hakikisha unapata taarifa sahihi kulingana na tatizo husika na kufanya maamuzi. Baada ya kukusanya taarifa hizi unaweza kufanya maamzi ya:
A: Kuonana na mhusika wewe binafsi ili muyaongee.
B: Kukutana nae mhusika chini ya watu wenye ushawishi, kuheshimika, wenye busara zao au viongozi ndani ya jamii.
C: Kulingana na uzito unaweza kuhusisha vyombo husika vya serikali.