Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Kaka me naweza kukusaidia kabisa, huwezi amini zipo dawa mkeo anapona kabisa.....kama inawezekana fungua PM yako nakupa no umtafute kuna dada mmoja yeye aliumwa sana mpaka alitaka kukatwa saivi amepona kabisa
Naomba nisaidie tafadhali, japo wangu ameshakatwa.
 
Maji lita 5, na majani ndoo ya kilo 10
Dawa hii nlimponesha shemeji yangu ambaye alilazwa bugando kwa kansa ya tezi dume alipofikia mwisho wakatuambia tumrudishe hom ja asingemaliza 4 weeks, akarudishwa hospitali ya wilaya. Ndo nikawaambia tujaribu hii tiba and baada ya miez 2 tu mzee alikuwa mzima na hospitali wakamdischarge aliishi 2years alikuja kuugua enimonia ikamwondoa na tulimrudisha bugando walishangaa kumwona ana afya nzuri
Ahsante sana, nitafanya hivyo kaka
 
Kwenye shavu tu mkuu,kakidonda kadogo kalianzia mdomoni kwa ndani.

Japo dunia ya leo imeshaharibika, kwanza upewe maua yako kwa kumjali mkeo na kufanya kila unaloliweza kuona anapata faraja ya moyo.
Si rahisi kusema kwamba tunatafuta tiba,maana wanaodai walipona huu ugonjwa sijui sijawasikia.
Bahati mbaya,mbaya sana,unajikuta matumizi ya pesa ni makubwa sana,na mtu badae anaondoka,anaacha simanzi na hali duni kwa familia. Hayayepukiki,hatuna namna.
Binafsi nakuelewa,ndugu yangu mmoja hivi karibuni nae kafiwa na mke,alikuwa Kenya. Kazaa kitoto,hajakinyonyesha,kikaletwa na kuhudumiwa. Kimefikisha miezi 6,mama anaonekana kapata nafuu,huyo,kaondoka.
Nachojaribu kusema hapa nikiangalia jama alivyobaki,asikwambie mtu. Jitahidi kujenga ukaribu na watu,pamoja na maumivu apate watu wa kuwa nae karibu,asijikatie tamaa. Wewe pia hivyo hivyo. Kuumia kwako(ni lazima kama binadamu usieona hatma ya jambo hilo),ila kumbuka unapomuonyesha kuishiwa nguvu,hili linamuathili kisaikolojia,huenda anakuona hutoweza kukabiliana na changamoto za maisha ikitokea akatangulia. Uwepo wa watu,utakusaidia hata wewe kutotokwa na machozi au kuonyesha huzuni.
Binafsi nawazaga,kama jf watu wanaweza kujadiliana mambo ya maana, wanashea upuuzi,kungekua hata na namna watu kama wewe wafikiwe,kwa nyakati tofauti tofauti,hakika mpaka unaandika hapa,mawazo yamezidi. Mpaka unahitaji msaada wa kimawazo kwa watu usiowaona na usiowajua,mi nakuelewa. Watu wangejua wenzao walipo,miongoni mwa watu 100 hata wakikutembelea 5, mnacheka,mnafurahi,unaona haupo mwenyewe,watu wanakufariji,hakiki hili linaweza kusaidia pia.
Ahsante sana kwa ushauri na faraja yako.

Kuna wachache kweli wanapona ama kuwa na afya njema kabisa. Sijui ni jambo la bahati tu au laah
 
Nikupe pole sana kwa kuuguliwa na mkeo... ila ningependa tu kuweka kitu kimoja sawa...
Kwanza kabisa kwa wewe kusema "najua yote ni mipango ya Mungu" Kiukweli si kila jambo ni lakusema mipango ya Mungu sidhani kama Mungu anaroho mbaya kiasi hicho cha kumfanya mkeo ateseke na kupitia magumu na uchungu kiasi hicho...
Watu wengi tumezoea kusema mipango ya Mungu na kujikuta kumsingizia Mungu vitu ambavyo hahusiki na kusahau kua shetani yupo pia na yeye mwenyewe ndio mshitaki wetu na asiependa kuona mtu anaongezeka, kufurahi,kufanikiwa n.k
Ningependa kunukuu tu maneno haya kutoka kitabu cha..
Yohana 10
10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
Hivyo kwa kusoma tu hapa nadhani utaona kazi ya adui (Shetani/mwivi) kazi zake hapo na kazi ya Mungu.
Nimeandika tu huenda nikawa nje ya mada ila niseme tu....
Mungu ajawai kushindwa... pale fikra zako zinapoishia na kuona hakuna matumaini tena, ndipo Mungu anapoanzia.
Akili za mwanadamu zina mwisho ila yeye hana mipaka wala ukomo, Mtafute Mungu namaanisha Mungu wa kweli bila kuangalia dini yako wala nini
Mtafute mtumishi wa Mungu Bishop Elibariki sumbe Youtube fatilia mafundisho yake na uchukue hatua ya kufika ibadani, Hakika utamwona Mungu akimfungua mkeo. Akuna lililo gumu kwa Mungu.
Mungu akutie nguvu na ujasiri na roho ya kukata tamaa isipate nafasi, Zidi kumwomba Mungu kutie nguvu wewe pamoja na mkeo mzidi kumwamini yeye na kumtumainia yeye.
Barikiwa Kiongozi.
Ahsante sana, huwa tunasema ni mpangobwa Mungu kwa maana huwa tunamwomba sana atuepushe na haya ila tunaishia kuyapata, ndipo tunasema huenda mwenyezi mungu mwenyewe kapanga iwe hivi.
 
Pole sana mkuu, sipendi kuuongea ukweli huu

Ila ni kwa kuwa umetuomba tutoe ushuhuda

Kiukweli hali aliyofikia si rahisi kupona hapo lazima utampoteza mke wako mpendwa.

Pole sana ndugu.

Tunasali Mungu akupe roho ya uvumilivu, usiache kumfariji mke wako mpendwa na kumwonyesha upendo
Ameen kak. Ahsante pia

Umeshauguza mgonjwa wa namna hii?
 
Hiyo cancer ipo stage gani? It's so sad mtu anapotea na ndugu mnaona huyu anapotea.
Mwanzo wa matibabu hospital ripot ilisema ni stage 2 or 3, kama stage zinapanda sijui kwa sasa ipo stage gani maana yapata miaka miwili sasa imepita
 
Kuna Mtaalam mmoja wa Tiba mbadala (Sio Mganga wa Kienyeji)
Anatoka Songea na ndo office yake ilipo, ila sasa namuona anazunguka Mikoani kutibu watu wenye Matatizo mbalimbali!

Sijawahi kushuhudia mafanikio ya Tiba yake, ila mara nyingi nimekua namskia akisema anazo Dawa za Miti shamba zinatibu na kuponya Cancer aina yoyote, na katika Stage yoyote, ngoja nijaribu kummuulizia namba yake...!

Mambo ya Tiba hasa za Asili ni kujaribu bila kuchoka, hasa kwa tatizo kama la Cancer, na uzuri Wataalam wa Tiba Mbadala hawana gharama kubwa kulinganisha na matibabu ya Hospital.
Sawa mkuu
 
Ndugu yetu pole sana na pia hongera mno kwakupigania afya ya mke wako.
Nimeshuhudia kwa baadhi ya ndugu wakipata shida na hili tatizo na kiukweli hospital hapajawahi kuwaletea ahueni kabisa.
Ngoja tujaribu kuuliza vizur wale waliopata ahueni walipitia njia gani ambazo zilikuwa mitishamba zaid.
 
Naelewa unachopitia mkuu, ila sitaki kueleza mengi upande huu, haraka sana muanzishie, glass moja ya juice ya kitunguu maji na kuichanganya pamoja na vijiko vitatu vya asali, kabla ya kunywa chochote, kila siku asubuhi na jioni kabla hajala kitu kwa siku 21.
 
Back
Top Bottom