Pole sana .
Alikua na kansa ya eneo gani mpaka anatoboka shavu?
Kwenye shavu tu mkuu,kakidonda kadogo kalianzia mdomoni kwa ndani.
Japo dunia ya leo imeshaharibika, kwanza upewe maua yako kwa kumjali mkeo na kufanya kila unaloliweza kuona anapata faraja ya moyo.
Si rahisi kusema kwamba tunatafuta tiba,maana wanaodai walipona huu ugonjwa sijui sijawasikia.
Bahati mbaya,mbaya sana,unajikuta matumizi ya pesa ni makubwa sana,na mtu badae anaondoka,anaacha simanzi na hali duni kwa familia. Hayayepukiki,hatuna namna.
Binafsi nakuelewa,ndugu yangu mmoja hivi karibuni nae kafiwa na mke,alikuwa Kenya. Kazaa kitoto,hajakinyonyesha,kikaletwa na kuhudumiwa. Kimefikisha miezi 6,mama anaonekana kapata nafuu,huyo,kaondoka.
Nachojaribu kusema hapa nikiangalia jama alivyobaki,asikwambie mtu. Jitahidi kujenga ukaribu na watu,pamoja na maumivu apate watu wa kuwa nae karibu,asijikatie tamaa. Wewe pia hivyo hivyo. Kuumia kwako(ni lazima kama binadamu usieona hatma ya jambo hilo),ila kumbuka unapomuonyesha kuishiwa nguvu,hili linamuathili kisaikolojia,huenda anakuona hutoweza kukabiliana na changamoto za maisha ikitokea akatangulia. Uwepo wa watu,utakusaidia hata wewe kutotokwa na machozi au kuonyesha huzuni.
Binafsi nawazaga,kama jf watu wanaweza kujadiliana mambo ya maana, wanashea upuuzi,kungekua hata na namna watu kama wewe wafikiwe,kwa nyakati tofauti tofauti,hakika mpaka unaandika hapa,mawazo yamezidi. Mpaka unahitaji msaada wa kimawazo kwa watu usiowaona na usiowajua,mi nakuelewa. Watu wangejua wenzao walipo,miongoni mwa watu 100 hata wakikutembelea 5, mnacheka,mnafurahi,unaona haupo mwenyewe,watu wanakufariji,hakiki hili linaweza kusaidia pia.