Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Pole, lakini lazima NIKUAMBIE UKWELII.

Hiyo unayoiita TIBA MBADALA ndio TIBA HALISI, Mimea ya asili yenye nguvu ya kukuponya na kuhuisha mwili dhidi ya maradhi ya aina yoyote.

Hayo MAKEMIKALI ndio yalipaswa kuwa TIBA MBADALA. Ukishafeli kutumia MIMEA SAFI (kitu ambacho hakiwezekani) sasa ndio ukajijaze MAKEMIKALI MACHAFU na MIONZI.

Mkiambiwa MNABEZA, ooohh MIMEA NI UCHAWI! Haya sasa!!!!! Umerudi kule kule!!!

Oooohh, wewe hujui sayansi, wewe mchawiii!! Sayansi yenyewe ndio hiyo, umelipa MAMILIONI ukajazwa MIONZI LUKUKI mpaka mwili ukaharibika zaidi na zaidi.

Najua kuna MAKANJANJA watanivamia hapa, lakini sijali. MIMI NAPASUA UKWELI TU, tukana, bwata, lakini HABARI IMEFIKA.
Upo irrational sana!
 
Njoo tupeane moyo.

Nimeanza kumuuguza dada yangu cancer kuanzia mwaka 2019,

Tuliambiwa afanye Chemo baadae afanyiwe upasuaji....

Akaanza mizunguko minne akamaliza, ikaongezwa minne akamaliza. Akarudishwa Muhimbili Kwa ajili ya upasuaji, madaktari wakatuambia arudi ocean road uvimbe haujapungua.

Ikaongezwa mizunguko 8 Tena , akapewa transfer Muhimbili awamu hii mgonjwa akagoma kufanyiwa Op. Akakaa nyumbani mwaka bila matibabu ya hospital.

Ziwa likatoboka likawa linamwaga maji tukarudi hospital,wakasema aanze chemo upya ikaenda mizunguko 6 na mionzi 16. Kamaliza mwez wa 10 mwaka huu Kwa Sasa kapewa mapumziko ya miezi mitatu na dawa anatumia.

Eneo la ziwa limefutika na wekundu kama kamwagiwa maji ya moto.

Cancer ni stage 4.


Ushauri wangu
Kama unaweza mpeleka ocean road mpelekee pale.
Pili kidonda kisafishwe Kila siku na maji ya drip wekeni na fragine ya vidonge mnatwanga mnapakaa eneo la kidonda kabla ya kukifunga

Kidonda usikifunge na khanga Wala kitenge funga na bandage.

Ajitahidi kunywa juisi ya stafeli angalau Kila siku glass Moja.
Majani yake pia chemsha anywee.

Mungu atutie nguvu katika Janga hili [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Daah pole sana, nyie hamkufanya upasuaji?

Vipi hali yake kwa sasa? Chemo na mionzi zimemchosha zaidi au angalau amepata ahueni?

Pole sana ndugu daah
 
Unaonaje ungempa muongozo wa suluhisho badala ya kumbeza? Kumbuka huyu mwenzetu ana wakati mgumu kuliko unavyoweza kufikiria
Yaani mtu mwingine hajui wakati mwingine km huna cha kuandika ni hekima kunyamaza.
Mwenzetu anapitia magumu,ni wakati wa kumpatia msaada pale iwezekanapo,mtu anacheka.
 
Huyo mkeo anapona ndani ya MIEZI MITATU TU.

Ukiachana na wale MAKANJANJA wanaokuuzia MAKEMIKALI na MACHANJO anapona haswa na anakuwa SWALAMA WASWALAMANTA.

Unachotakiwa ni kuwa na AKILI TIMAMU tu, na kujiamini.
Mtoa mada angekutilia maanani akaachana na wategemea miujiza angevuna kitu cha maana sana kwako
 
Kuna mtu mmoja nilikutana nae machakos kenya nikiwa na shida fulani,ni daktari mwenye bustani ya dawa na alinisaidia nikapona kabisa,katika moja ya maongezi yake alizungumzia cancer ila sina hakika na jambo alilonalo mkeo kama liko mahala anapoweza kufanyia kazi,
Nitajitahid nikutafutie mawasiliano yake uone kama kuna analoweza kukushauri ama kukusaidia
Sawa mkuu
 
Pole sana mkuu MWENYEZI MUNGU asaidie, mama yangu alifariki na kansa ya titi mwaka 2013, alikuwa kashafanyiwa operesheni ndo maisha mkuu tutafanyaje!?
Apumzike kwa amani mama. Ina maana baada ya upasuaji aliendelea kuumwa eneo hilo?

Nauliza ili nipate uzoefu wako na mginjwa wa aina hii
 
Daah pole sana, nyie hamkufanya upasuaji?

Vipi hali yake kwa sasa? Chemo na mionzi zimemchosha zaidi au angalau amepata ahueni?

Pole sana ndugu daah
Mgonjwa aligoma kufanya upasuaji. Hali yake sio nzuri sana Wala mbaya sana, Kwa Sasa anasumbuliwa na kifua kubana maana Kuna dalili Kansa inasambaa kwenye mapafu hii kutokana na vipimo vya hospital.
Anapata maumivu ya mifupa na ganzi.

Miozi ilienda kutonesha kidonda kikazidi kuwa kikubwa ila baada ya kumaliza ndio kikaanza kufunga taratibu.
 
Yapata miaka miwili imepita tangu mke wangu alipogundulika ana saratani ya matiti, tulianza dozi ya CHEMOTHERAPY pale GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL Ifakara, tulipatiwa jumla ya mizunguko 8 ya CHEMO, hali ilionekana kuwa nzuri ila ndani ya muda mfupi sana uvimbe ulianza tena.

Baada ya kuona uvimbe umeanza upya tulihamia Dodoma BENJAMIN MKAPA napo tulipatiwa chemo 4 kisha ukafanyika upasuaji ili kuondoa titi lililoathirika na saratani, upasuaji amefanya mwezi wa 4 mwaka huu.

Baada ya upasuaji hali ilionekana kama ipo vizuri, ila baada ya miezi ipatayo mi3 mgonjwa ameanza kusumbuliwa tena.

Anasumbuliwa na; MAUMIVU MAKALI SANA MAHALA ALIPOFANYIWA UPASUAJI
KIDONDA KISICHOPONA (kilianza kidogo sana, kama kiji upele, hatimae kikakua. Hakionyeshi dalili ya kupona.

Najua yote ni mipango ya Mungu, ila sina matumaini kama mke wangu anaweza kupona kwa sasa.

KUNA MTU ASHAWAHI KUUGUZA MGONJWA WA SARATANI naomba ushuhuda ambao unaweza nisaidia cha kufanya.

KAMA KUNA DAWA ZA TIBA MBADALA ULITUMIA ZIKASAIDIA, NAOMBA MSAADA PIA.

Kwa sasa mgonjwa yupo tu nyumbani tunasubiri neema ya Mungu

Ushauri wowote pia napokea.
Pole Sana uchungu unao pata ni mkubwa mno

Ila Acha nikushaur kitu

Mpe furaha mkeo muda wote na mwambie Kila muda kuwa unampenda na umeridhika na Hali yake usimbeze ,usimkaripie wala kumdhihaki kivyovyote vile..

Usiache kumwambia kwamba haya yote ni majaribio ya Mungu na baada ya dhiki faraja

Usionyeshe Una huzuni Sana kwa Hali yake

Vivyo hivyo muombeni Mungu katika Kila Hali

Nimeumia mno pole Sana mkuu

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Kuna tunda linaitwa Stafeli au Brazilian paw paw au soursop
Wengi wanasema inatibu cancer na madonda sugu
Cancer research wameliangalia hili ila kiutaalamu bado ila wanatumia
Screenshot_20231222_185332_Chrome~2.png
 
Mkuu pole kwa Mke wako kuumwa na maradhi ya Sratani ya maziwa aka Breast Cancer nitafute mimi kwa wakati wako ili nipate kumtibia mke wako.Kwani kutumia CHEMOTHERAPY kutammaliza mke wako taratibu atakwenda zake duniani kwani hiyo CHEMOTHERAPY haitibu Maradhi ya Cancer ya aina yoyote ile kwani CHEMOTHERAPY inauwa Cells zilizo hai na cells zilizo kufa kwa hiyo sio rahisi CHEMOTHERAPY kumponyesha mke wako unapoteza pesa zako bure hapo.

''Chemotherapy is an approach that destroy the Cells.
Chemotherapy doesn't distinguish between good cells and bad
cells. It destroys cells. It's an ACID Approach. -Dr.Sebi.
''Chemotherapy ni mbinu inayoharibu Seli.
Chemotherapy haitofautishi kati ya seli nzuri na mbaya
seli. Inaharibu seli zote. Ni Mbinu ya ACID. -Dkt.Sebi.
Endapo hatopona utamlipa fidia ya kumpotezea muda kwenye hayo matibabu yako? Tuacheni masikhara au kuleta biashara kwenye afya za watu, wewe ungekuwa na uwezo huo wa kutibu Cancer wala usingekuwa na muda wa kushinda humu jamvini kuwinda watu wa kuwatibu, watu wangekufuata wenyewe na usingekuwa na muda kabisa maana hata wateja wangekuzidia, pengine hata serikali ingekuwezesha ili uweze kusaidia wengi.


Acheni janjajanja yenu kwenye matatizo ya watu tafadhali.
 
Ñaweza Sema ,ukweli ambao si mzuri kuusikia,
Mtayarishe mkeo kiroho.....wekeza nguvu nyingi kuponya roho yake I mean Muandae,ni ngumu ilà ni muhimu mweke karibu na Mungu kama kuna mila maagano ,dhambidhambi na mambo mengine ya ushirikiana na mambo ya ajabu Acha,
Amrudie Mungu ......aweza ponya roho yake asije akatwseka dunia na motoni.
# ni muhimu kuliko kuwekeza duniani.
Mtafute kiongozi wa kiroho eg tumia redio upendo
  • aungame
  • ajitayarishe KWA wakati wowote
Daah it's not fair

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Apumzike kwa amani mama. Ina maana baada ya upasuaji aliendelea kuumwa eneo hilo?

Nauliza ili nipate uzoefu wako na mginjwa wa aina hii
Alikuwa dar es saalam mkuu alipofanyiwa operesheni alikuwa anachomwa miozi pale muhimbili, mkuu sikuwa karibu nae mi nilikuwa mkoani huku, tulikuwa tunapewa tu taarifa ya hali yake, kuamkia jumapili alifariki akiwa amelala tu kitandani Nyumbani kimya milele, ndo hivyo tu
 
Pole sana ndugu ,pole mno.
Mwenyezi Mungu ampe nguvu ya kuvumilia maumivu, ampe subira na tumaini.
Kuna wakati mwanadamu anafika kikomo kwa namna ya ubinadamu na hapo ndipo Mungu hushika nafasi ,Mungu yupo na yupo kwa wote, wote wenye heri na wenye Shari.
Yupo kwa kila mwenye haja nae, hajifichi wala hayupo mbali sana kwa yoyote aliweka nia ya dhati kumhitaji.

Wakati huu mkiwa mnapitia changamoto hio na maumivu hayo makali na kukata tamaa ndio Mungu hushika nafasi yake.

Ili kukutana na Mungu kwanza kuweni na amani, msilitazame sana hilo tatizo bali muoneni Mungu katika hilo tatizo, mshuhudieni Mungu kwenye hilo tatizo.

Jitahidini sana mfanya ibada na matendo mema na kuwasaidia wengine wenye hali kama ya kwenu, wapeni moyo wenye hali mfano wa ya kwenu, waombeeni wengine walio kama nyie, toeni sadaka za shukurani kwa wenye mahitaji maalumu, tembeleeni wagonjwa, tembeleeni wafungwa tembeleeni wazee na wenye namna yoyote ya udhaifu wanahitaji faraja na tumaini.
Ikiwa mtajaliwa kufanya hivyo itawajieni amani, itawajieni furaha na tumaini, hamtayazama tena tatizo la mke wako kama hapo awali.

Amini kaka nakushuhudia mke wako atapona , kupona kusikotazamiwa wala kudhaniwa .

Binafsi nakuombeeni katika nia zangu hakika nitawaweka nanyi, mwenyezi Mungu yupo na ataonekana kweli katika maisha yenu.
 
Pole sana mkuu. Ni mtihani,kaza moyo.

Uliwahi ulizia kuhusu Butaro Cancer Center of Excellence? Ni kituo cha wamarekani,kipo Rwanda. Nimeonapo watu wengi wa nchi mbali mbali za Africa, sikufatilia kujua ila huenda wakawa na advanced technology kupunguza maumivu. Kupona sizungumzii.

Mgonjwa tuliewahi kuwa nae alitoboka shavu, ila mpaka anakufa, maumivu hayakuwa makali.

Labda ujaribu kufatilia uone kama watakuwa na la ziada
 
Back
Top Bottom