Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Mbona naskia ukiwahi Early stages unapona?
Ni sahihi na ushahidi bint wa marehemu dada yangu aligundulika na Kansa ya kizazi wakati yupo Standard 7 akatibiwa pale Muhimbili na kupona kabisa na mpaka leo yupo na mzima wa afya isipokua huwa kila baada ya muda anaenda kufanyiwa uchunguzi kuona kama kuna viashiria vya kurudi.
 
Mtoto mdogo kansa ya kizazi🥹
 
Mtoto mdogo kansa ya kizazi🥹
Sisi wenyewe tulishangaa sana lakini alianzia temeke tukapewa rufaa Muhimbili huko wakathibitisha na kwasababu na mama yake alikufa na huo ugonjwa tukakubali..Japo mzee hakukubali haraka vilifanyika vipimo zaidi ikathibitishwa akaanza matibabu kwa miaka 2 aliteseka sana na yale matibabu kuna muda hatukuamini kua yule ni ndugu yetu tena mtoto mdogo anapitia mateso yale...nilipokua naenda wodi zao huko ndo nikakutana na watoto wadogo kuliko yeye wana hayo matatizo ya kansa wengine tumbo,wengine sijui damu nk.

Ukiwa mzima mshukuru sana Mungu kwa neema
 
Nidanganye ili iweje?

Kansa ukiwahi unapona kabisa tafuteni taarifa muache ubishi
Nafikiri hujaelewa nilichoquote na lengo la niliyemwuote.

Hilo swali uliloniuliza ndilo nililomuuliza.
 
Daah, sadly ni kwamba tumefunga ndoa mwaka 2020 mwezi wa 9, mwaka 2021 akaanza kuumwa mpaka muda huu.
Kama una Imani ya Muumba huna Cha kusikitika, Bali kuzidi Imani na Subira kwani wanadamu sisi si lolote si chochote, hatuamini Muumba wetu tukiwa salama likitupata khofu inatujaa, tulia wewe na mke wako abuduni, rejeeni kwake kwani hakuna limpatalo mtu ila limepangwa limpate, Amini mponyaji ni Allah, hizo dawa ni sababu tu laiti kama dawa zinaponya basi watu wasingekufa, tumia dawa na muombe Allah akuponye kupitia dawa ambayo ndiyo sababu ya kupona iwe za kisasa au za lishe za asili. Ikiwa utaweka akili Yako sana kwenye Dunia hiyo itakuumiza kwani sote mpaka tunaokupa faraja sote tutakufa na hakuna Kati yetu anayeweza kuchagua njia ya kifo chake kwani tayar kimeshapangwa, Bali kwa Dua za kumuomba Allah asitupe mitihani mizito na magonjwa mazito, kwani yeye ndiye mpangaji wa kila kitu, Allah akubariki na amponye mgonjwa wako.
 
Tuwekee wazi hayo mauchafu na machanjo Ili tuyaepuke
 
Mkuu narudia tena me nimeuguza mgonjwa wa cancer sijui mgonjwa wako iko stagee gani kama imeshasambaa sikushauri labda km umeiwahi na muda unavyozidi huna option nyengine utaambiwa ana muda flani wakuishi japo mungu ndo anajua mwisho wake lini ! Ingekuwa mimi hii option wallah ningeruka nayo nenda hili group la wagonjwa wa cancer liko fb omba ushauri wa protocol gani utumie kwa mgonjwa wako kisha anza mara kufanyia kazi
 

Attachments

  • Screenshot_20250210_031729_Opera Mini.jpg
    71 KB · Views: 4
Mkewe ametangulia mbele za haki asee.
 
Mungu amlaze pahala pema inshallah, pole sana mkuu.
 
Ahsante sana ndugu, japo nilimpoteza yapata mwaka sasa
 
Hakika

Imepita mwaka mmoja sasa tangu mke wangu arudi kwa mola
 
Nyonya chuchu
 
Kuna Dada mmoja yupo Morogoro alikuwa na changamoto kama ya mke wako pls mpigie Nina Iman atakupa ABC yey anasema amepona kabisa nambar yake ni 0768883459
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…