Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Pole sana,sasa huyo anahitaji dawa za kupoza tu maumivu na kuishi kwa uponyaji wa roho zaidi.Hapo curative stage imeshapita. Na hapo yupo kwenye palliative stage. Anahitaji huduma za kumtia moyo kiroho na kupunguza maumivu mpaka Mungu atakapomchukua.
 
Huwezi kupona kwa KUBUGIA BUGIA TU madawa au TIBA, lazima akili yako isafishwe kwanza.

Kuna mtu yeye anaamini akimeza MADONGE YENYE KEMIKALI anapona, unaona huyu ni CHIZI. Anahitaji msaada wa kiakili kwanza.

Mwingine anaamini kwamba MIMEA ni UCHAWI, huyu ni mpuuzi na goigoi tu wa kawaida, unamchangamsha kwa NAKOZI mbili tatu anazinduka kisha UNAMPA TIBA.
Mkuu kama unaifahamu hiyo tiba ya mmea ebu msaidie kwanza , hii elimu tutaleteana baadaye akishapona, okoa jahazi mkuu
 
Pole sana mkuu
Chukua huu ishauri utanishukuru
Chukua majana ya stafeli changanya na maji masafi lita5 na majani yajae ndoo ndogo ya lita 10. Maji yachemshe hadi yawe ya moto then chukua hayo maji nusu lita saga na majani yamejaa chupa ya blender hadi majani na maji yaishe. Yaache yapoe mdogo mdogo masaa 12. Xhuja them mgonjwa yawe ndo maji yake ya kunywa. Unaweza kuongeza limao kuweka ladha na kamwe usiongeze kitu kingine ila kama ladha itakushinda basi ongeza tunda lenyewe ondoa tu mbegu blend ba maganda yake
Tumia hadi utakapopata nafuu
AHAKIKISHE ANAPATA HILO TUNDA KILA SIKU ASUBUHI NA JIONI HATA KWA KUNUNUA KWA MUDA USIOPUNGUA MIEZI MI3.

YAANI STAFELI IWE KIFUNGUA NA KIFUNGA KINYWA CHAKE PIA.

Hakuna hasara ataipata wala madhara kwa sababu hilo ni tunda pia.
 
Yapata miaka miwili imepita tangu mke wangu alipogundulika ana saratani ya matiti, tulianza dozi ya CHEMOTHERAPY pale GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL Ifakara, tulipatiwa jumla ya mizunguko 8 ya CHEMO, hali ilionekana kuwa nzuri ila ndani ya muda mfupi sana uvimbe ulianza tena.

Baada ya kuona uvimbe umeanza upya tulihamia Dodoma BENJAMIN MKAPA napo tulipatiwa chemo 4 kisha ukafanyika upasuaji ili kuondoa titi lililoathirika na saratani, upasuaji amefanya mwezi wa 4 mwaka huu.

Baada ya upasuaji hali ilionekana kama ipo vizuri, ila baada ya miezi ipatayo mi3 mgonjwa ameanza kusumbuliwa tena.

Anasumbuliwa na; MAUMIVU MAKALI SANA MAHALA ALIPOFANYIWA UPASUAJI
KIDONDA KISICHOPONA (kilianza kidogo sana, kama kiji upele, hatimae kikakua. Hakionyeshi dalili ya kupona.

Najua yote ni mipango ya Mungu, ila sina matumaini kama mke wangu anaweza kupona kwa sasa.

KUNA MTU ASHAWAHI KUUGUZA MGONJWA WA SARATANI naomba ushuhuda ambao unaweza nisaidia cha kufanya.

KAMA KUNA DAWA ZA TIBA MBADALA ULITUMIA ZIKASAIDIA, NAOMBA MSAADA PIA.

Kwa sasa mgonjwa yupo tu nyumbani tunasubiri neema ya Mungu

Ushauri wowote pia napokea.

1. Mkuu hilo gonjwa kwao Ocean road nikadhani ..

2. Huko Ifakara na BM yaweza kuwa muda mwingi mmepoteza bila tija ya kutosha.

3. Jipeni moyo, kama uwezekano wa kufika ocean road upo, pamoja na tatizo kubwa la hospitali zetu la urasimu na usumbufu usio na sababu kwa wagonjwa; pangeni kufika huko.

4. Mungu mkubwa msikate tamaa; kubaki nyumbani au kukimbilia kwa mitishamba hakutawasaidia.
 
Pole sana mkuu..mama yangu mdogo pia alikatwa titi lakini baada ya miezi kadhaa maumivu yamerudi ukweli ni kwamba tunachelewa ssana kuijua kansa so inakuwa imeshaenea..anatumia dawa za kienyeji kwa sasa maumivu yamepungua mpaka anaenda clinic wanamshangaa pole sana ninaweza kukulink nitafute DM nikulink nae labda inaweza kusaidia pole mungu akufanyie wepesi
 
AHAKIKISHE ANAPATA HILO TUNDA KILA SIKU ASUBUHI NA JIONI HATA KWA KUNUNUA KWA MUDA USIOPUNGUA MIEZI MI3.

YAANI STAFELI IWE KIFUNGUA NA KIFUNGA KINYWA CHAKE PIA.

Hakuna hasara ataipata wala madhara kwa sababu hilo ni tunda pia.
Ahsante sana
 
Endapo hatopona utamlipa fidia ya kumpotezea muda kwenye hayo matibabu yako? Tuacheni masikhara au kuleta biashara kwenye afya za watu, wewe ungekuwa na uwezo huo wa kutibu Cancer wala usingekuwa na muda wa kushinda humu jamvini kuwinda watu wa kuwatibu, watu wangekufuata wenyewe na usingekuwa na muda kabisa maana hata wateja wangekuzidia, pengine hata serikali ingekuwezesha ili uweze kusaidia wengi.


Acheni janjajanja yenu kwenye matatizo ya watu tafadhali.
🙏🏿🙏🏿
 
Urea from a mammal haijawahi kuwa toxic kama ammonia!!

Hizo medicine from hospital are More toxic than own urea plus water!!
Mkuu unamshaurije anywe kitu ambacho mwili wenyewe umekitoa kama uchafu(taka mwili) ?

Mwili anasema hautaki mkojo then wewe unamshauri anywe mkojo wake uingie mwilini wakati huo mwili mwenyewe anautoa mkojo huo kama uchafu ? Sio sawa mkuu.

Alafu jiulize tu kama mkojo ni dawa endapo utaunywa basi ni kwa nini mkojo huo usingefanya kazi kabla haujatoka mwilini kwa njia ya mkojo ?

mkojo sio dawa kwa mwili bali ni taka mwili,ingelikuwa mkojo ni dawa si ungetiba wakati bado upo mwilini.
 
Back
Top Bottom