Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Ahsante sana
Pole sana Mkuu
Umepambana sana,Mungu ameona mapambano yako ila jua tu Mungu anaweza kufanya mambo yote,na wala makusudi yake hayazuiliki.
We may have our own plan but God has last say.

Apumzike kwa amani Mkeo Mpenzi,
Bwana alitoa na sasa ametwaa,jina la Bwana lihimidiwe.

Pole kwa familia,Mungu aliyemchukua mpendwa wenu ndiye pekee anajua namna nzuri ya kuwapitisha kwenye maumivu.
 
HAIJAWA BAHATI KWANGU, SARATANI IMESHINDA VITA YA KUPIGANIA UHAI NA MKE WANGU
Maumivu unayo.. Tena maumivu hasa..

Pole Sana .. .. kaza moyo usije kuathirika .. mna mtoto anahitaji mapenzi ya baba zaidi kwa sasa maana mama ndio keshatwaliwa!

M/Mungu akufanyie wepesi InshaAllah
 
Yapata miaka miwili imepita tangu mke wangu alipogundulika ana saratani ya matiti, tulianza dozi ya CHEMOTHERAPY pale GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL Ifakara, tulipatiwa jumla ya mizunguko 8 ya CHEMO, hali ilionekana kuwa nzuri ila ndani ya muda mfupi sana uvimbe ulianza tena.

Baada ya kuona uvimbe umeanza upya tulihamia Dodoma BENJAMIN MKAPA napo tulipatiwa chemo 4 kisha ukafanyika upasuaji ili kuondoa titi lililoathirika na saratani, upasuaji amefanya mwezi wa 4 mwaka huu.

Baada ya upasuaji hali ilionekana kama ipo vizuri, ila baada ya miezi ipatayo mi3 mgonjwa ameanza kusumbuliwa tena.

Anasumbuliwa na; MAUMIVU MAKALI SANA MAHALA ALIPOFANYIWA UPASUAJI
KIDONDA KISICHOPONA (kilianza kidogo sana, kama kiji upele, hatimae kikakua. Hakionyeshi dalili ya kupona.

Najua yote ni mipango ya Mungu, ila sina matumaini kama mke wangu anaweza kupona kwa sasa.

KUNA MTU ASHAWAHI KUUGUZA MGONJWA WA SARATANI naomba ushuhuda ambao unaweza nisaidia cha kufanya.

KAMA KUNA DAWA ZA TIBA MBADALA ULITUMIA ZIKASAIDIA, NAOMBA MSAADA PIA.

Kwa sasa mgonjwa yupo tu nyumbani tunasubiri neema ya Mungu

Ushauri wowote pia napokea.
Nimeikuta hii sehemu sijui kama inaweza kusidia
Screenshot_20240205-092945.png
 
HAIJAWA BAHATI KWANGU, SARATANI IMESHINDA VITA YA KUPIGANIA UHAI NA MKE WANGU

Pole sana mkuu[emoji24][emoji22]
Mwenyezi Mungu akawe mfariji kwako na kwa familia katika kipindi hiki kigumu mnachokipitia.

[emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431]
 
Back
Top Bottom