SI KWELI Kanu ni Mnyama anayenukia harufu ya ubwabwa porini/vichakani

SI KWELI Kanu ni Mnyama anayenukia harufu ya ubwabwa porini/vichakani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Huyu ni mnyama mkali sana, mkorofi, na mwenye nguvu katika jamii ya paka.

Akiingia bandani, anondoka na kuku mzima na anaenda kula kichwa mpaka shingoni. Kama ni kifaranga, anakula chote au akikuta mayai ambayo bado kidogo ya yaanguliwe, ndio soshi wake.

Anakaa vichakani au porini, sehemu yenye msitu mkali. Akigundua kwamba yupo kwenye eneo lenye adui kama mbwa, chui, fisi au binadamu, anaachia ushuzi wake ambao unanukia kama wali au ubwabwa, kiasi kwamba utadhani mtu kaficha huo wali vichakani.

Kumekuwa na dhana kwamba ukisikia harufu ya ubwabwa vichakani, ni chatu. Hapana, sio kweli; ni huyu mnyama anayeitwa kanu katika Kiswahili (kwa huku mtaani, sijui upande mwingine).

Naendelea kutega; nikikamata nitawaletea mumjue.

Huyu nimetega baada ya kula kuku wangu sana.


Kanu.jpg
 
Tunachokijua
Kanu ni wanyama wadogo, Wanyama hawa ni warefu na wembamba wenye mkia mrefu, kichwa kidogo na masikio makubwa. Rangi yao ni nyeupe hadi njano na wana madoa meusi na mkia wenye miviringo. Mpaka sasa kuna spishi 17 za kanu zilizoainishwa.

330px-Rusty-spotted_Genet_%28Genetta_maculata%29_%2832484079077%29.jpg
Kumekuwa na hoja inayodai kuwa mnyama Kanu hutoa ushuzi wenye harufu ya wali pale anapohisi adui kama njia ya kujilinda.

Je, ukweli wa hoja hiyo ukoje?
JamiiCheck imepitia makala na tafiti mbalimbali kuhusu maisha ya Kanu ili kupata uhalisia wa madai kuwa Kanu hutoa ushuzi ambao una harufu kama wali na kubaini kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.

Kanu wana tezi zinazozalisha harufu ambazo zipo kati ya mwanzo wa mikia yao na karibu na sehemu ya haja kubwa. Tezi hizo za harufu hutoa majimaji yenye harufu ya mkojo ambayo kanu hutumia kwa mawasiliano, kuashiria maeneo yao, na wakati mwingine kuwatisha wanyama au maadui wanaowawinda.

Kama wanyama wengine wengi, kanu hutegemea kuacha alama za harufu kama njia ya kutoa taarifa kuhusu uwepo wao, hali yao ya uzazi, na mipaka yao kwa wanyama wengine.

Aidha, Harufu inayotolewa na tezi za kanu hainuki kama wali kam inavyodaiwa bali Kanu hutoa harufu ya mkojo kutoka kwenye tezi zao, harufu ambayo mara nyingi huelezwa kuwa kali na isiyopendeza, sawa na harufu ya wanyama wengine walao nyama.

Pia JamiiCheck imemtafuta na kuzungumza na Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja ambaye ameeleza kuwa harufu ya Ubwabwa au wali porini haihusiani na wanyama mbalimbali ambao wamekuwa wakihusishwa nayo, aidha amesema kuwa harufu hiyo hutolewa na aina fulani ya miti.

"Kuhusu harufu ya ubwabwa porini wengi huihusisha na wanyama mbalimbali. Lakini Kiuhalisia kuna aina fulani ya miti Mti kama Potato Bush (kiingereza) na Jina la kisayansi ni PHYLLANTHUS RETICULATUS ambayo hutoa harufu ya aina hiyo na sio Kanu wala Gamba la nyoka maana wengine wanahusisha na nyoka kujivua gamba".:-Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja
😃😃😃😃 daaah ukute all my life najidanganyaga nilishawahi kutana na chi face 2 face, yaweze kana alikuwaga huyu mdudu. Maana nakumbuka utotoni nilishawahi zua kiazaa zaa kijiji kizima kilijua kijijini hapo kuna chui, by the way nilikutana na linyau kama hilo nahisi,
Ndio huyu hata kipindi niko jkt tulifanikiwa kumwu asee
 
Jamii check rudini upya mkafanye utafiti wenu:huenda tumetofautiana jina la huyu mnyama ila mnyama anaenukia ubwabwa ni huyu.
 
wa stendi taratibu mzee naona kama umepanic hiv baada ya uzi wako kupata neno "si kweli" punguza mzuka bro
Sawa
Ila ninachoamini ni hiki nilicholeta maana nimekamata mwenyewe harufu ipo na sio mara ya kwanza kunasa.
Labda tuu walichaleta wao ni aina ingine jamii hii hii.maana hata fisi wa mikumi hawafanani na wa serengeti au ni kama unavyoona chiter leopard au tiger.
 
wa stendi unataka kupotosha Umma Mzee.
Hawa jamii heck wamegoovle wakaletewa mnyama tofauti maelezo walopewa wakaleta kama walivyoambiwa.
Yaani ni kama unavyoona beberu kuna wanaonukia na ambao hawanukii ila ukweli ni huyu nimemkamata na anaukia ubwabwa kama hamuamini amini hawa jamii check na google yao.
 
Hawa jamii heck wamegoovle wakaletewa mnyama tofauti maelezo walopewa wakaleta kama walivyoambiwa.
Yaani ni kama unavyoona beberu kuna wanaonukia na ambao hawanukii ila ukweli ni huyu nimemkamata na anaukia ubwabwa kama hamuamini amini hawa jamii check na google yao.
Kubali tu kuwa ulichemka na uombe msamaha kwa kuuongopea umma. Umekazana ubwabwa ubwabwa. Mwanaume kwanza unaaanzaje kung'ang'ania hilo jina. Omba msamaha wananzengo.
 
Fungo ni mwingine ambae ni huyu nae nimenasa jana kwa jina jingine ni karasa
Bro wewe ni noma nahitaji unifundishe au uniuzie huo mtego nami niwanase watesi wangu, huku nilipo kuna yale yenye mikia mirefu mieupe yanatembea usiku tu, na yale mavicheche yanamikia mirefu huwa yanatembea solo mchana ni yana nitesa sana.
 
Wa stendi Unasema mnyama mwingine? Waliomuweka kwenye picha naona anafanana na huyo wako, pia kwenye hizo video hapo ukifungua mnyama ni huyo huyo na maelezo yako kama walivyoweka hapo.

Pia Kuna majibu ya mtaalamu wa wanyama hapo wote wawe wamekosea kasoro wewe?
 
Jamii check rudini upya mkafanye utafiti wenu:huenda tumetofautiana jina la huyu mnyama ila mnyama anaenukia ubwabwa ni huyu.
Sio kweli. Mnyama anayetoa harufu ya chakula Kama Ni kanu anafanya hivyo kwa lengo gani? Yani Kwanini atoe hiyo harufu? Tunajua wanyama au wadudu wanaofanya hivyo Ni kwa lengo la kuwavutia wanyama wanaopenda vyakula ili wawale
 
Yaani nifanye tafti zangu alafu niandike uzi hapa jamvini alafu moderator waje kusema sio kweli ,🙃🙃 hakika nitatafuta nauli nifike mpaka ofisini kwao na nimuhitaji mkuu wao maana ni Kama juhudi zangu ni bure
 
Back
Top Bottom