SI KWELI Kanu ni Mnyama anayenukia harufu ya ubwabwa porini/vichakani

SI KWELI Kanu ni Mnyama anayenukia harufu ya ubwabwa porini/vichakani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Huyu ni mnyama mkali sana, mkorofi, na mwenye nguvu katika jamii ya paka.

Akiingia bandani, anondoka na kuku mzima na anaenda kula kichwa mpaka shingoni. Kama ni kifaranga, anakula chote au akikuta mayai ambayo bado kidogo ya yaanguliwe, ndio soshi wake.

Anakaa vichakani au porini, sehemu yenye msitu mkali. Akigundua kwamba yupo kwenye eneo lenye adui kama mbwa, chui, fisi au binadamu, anaachia ushuzi wake ambao unanukia kama wali au ubwabwa, kiasi kwamba utadhani mtu kaficha huo wali vichakani.

Kumekuwa na dhana kwamba ukisikia harufu ya ubwabwa vichakani, ni chatu. Hapana, sio kweli; ni huyu mnyama anayeitwa kanu katika Kiswahili (kwa huku mtaani, sijui upande mwingine).

Naendelea kutega; nikikamata nitawaletea mumjue.

Huyu nimetega baada ya kula kuku wangu sana.

Kanu.jpg
 
Tunachokijua
Kanu ni wanyama wadogo, Wanyama hawa ni warefu na wembamba wenye mkia mrefu, kichwa kidogo na masikio makubwa. Rangi yao ni nyeupe hadi njano na wana madoa meusi na mkia wenye miviringo. Mpaka sasa kuna spishi 17 za kanu zilizoainishwa.

330px-Rusty-spotted_Genet_%28Genetta_maculata%29_%2832484079077%29.jpg
Kumekuwa na hoja inayodai kuwa mnyama Kanu hutoa ushuzi wenye harufu ya wali pale anapohisi adui kama njia ya kujilinda.

Je, ukweli wa hoja hiyo ukoje?
JamiiCheck imepitia makala na tafiti mbalimbali kuhusu maisha ya Kanu ili kupata uhalisia wa madai kuwa Kanu hutoa ushuzi ambao una harufu kama wali na kubaini kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.

Kanu wana tezi zinazozalisha harufu ambazo zipo kati ya mwanzo wa mikia yao na karibu na sehemu ya haja kubwa. Tezi hizo za harufu hutoa majimaji yenye harufu ya mkojo ambayo kanu hutumia kwa mawasiliano, kuashiria maeneo yao, na wakati mwingine kuwatisha wanyama au maadui wanaowawinda.

Kama wanyama wengine wengi, kanu hutegemea kuacha alama za harufu kama njia ya kutoa taarifa kuhusu uwepo wao, hali yao ya uzazi, na mipaka yao kwa wanyama wengine.

Aidha, Harufu inayotolewa na tezi za kanu hainuki kama wali kam inavyodaiwa bali Kanu hutoa harufu ya mkojo kutoka kwenye tezi zao, harufu ambayo mara nyingi huelezwa kuwa kali na isiyopendeza, sawa na harufu ya wanyama wengine walao nyama.

Pia JamiiCheck imemtafuta na kuzungumza na Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja ambaye ameeleza kuwa harufu ya Ubwabwa au wali porini haihusiani na wanyama mbalimbali ambao wamekuwa wakihusishwa nayo, aidha amesema kuwa harufu hiyo hutolewa na aina fulani ya miti.

"Kuhusu harufu ya ubwabwa porini wengi huihusisha na wanyama mbalimbali. Lakini Kiuhalisia kuna aina fulani ya miti Mti kama Potato Bush (kiingereza) na Jina la kisayansi ni PHYLLANTHUS RETICULATUS ambayo hutoa harufu ya aina hiyo na sio Kanu wala Gamba la nyoka maana wengine wanahusisha na nyoka kujivua gamba".:-Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja
Huyu ni mnyama mkali sana, mkorofi, na mwenye nguvu katika jamii ya paka.

Akiingia bandani, anondoka na kuku mzima na anaenda kula kichwa mpaka shingoni. Kama ni kifaranga, anakula chote au akikuta mayai ambayo bado kidogo ya yaanguliwe, ndio soshi wake.

Anakaa vichakani au porini, sehemu yenye msitu mkali. Akigundua kwamba yupo kwenye eneo lenye adui kama mbwa, chui, fisi au binadamu, anaachia ushuzi wake ambao unanukia kama wali au ubwabwa, kiasi kwamba utadhani mtu kaficha huo wali vichakani.

Kumekuwa na dhana kwamba ukisikia harufu ya ubwabwa vichakani, ni chatu. Hapana, sio kweli; ni huyu mnyama anayeitwa kanu katika Kiswahili (kwa huku mtaani, sijui upande mwingine).

Naendelea kutega; nikikamata nitawaletea mumjue.

Huyu nimetega baada ya kula kuku wangu sana.

Iringa vipo vingi hivi
 
😃😃😃😃 daaah ukute all my life najidanganyaga nilishawahi kutana na chi face 2 face, yaweze kana alikuwaga huyu mdudu. Maana nakumbuka utotoni nilishawahi zua kiazaa zaa kijiji kizima kilijua kijijini hapo kuna chui, by the way nilikutana na linyau kama hilo nahisi,
 
Nashangaa kwanin kuna baadhi ya watu wanamlalamikia bwana wa stendi kuhusu kumkill huyu faken
I think wengi wenu hamjawahi kufuga hasa kwa malengo.
Huu n mwez wa kumi, bado mvua chache tu sikukuu zifike, ukute tayari ushaandaa kuku wako uwauze ujazie ada watoto waende shule alafu huyu ubwabwa awale? Inauma sana.
Mimi kuna mbwa alikua amezoea kula mayai ya kuku wangu, siku moja nkamtaitisha kwenye 18, aisee alipokea kichapo heavy alikua analia zaidi ya ambulance. Sidhan kama atarudia tena.
Eti uite askari wa TANAPA, aje afanye nini?
Ee
 
Hana ni mikwara tuu ukimbananisha anatuna na milio unaweza vunjika kwa mbio.
Ila akikushika mguu au mkono kidole anaondoka nacho.
Hapo kumuu nimepitisha kitanzi ndani ya banda kwanza.
Yaani kwa mfano utege na mtego ule wa kufyatuka anase labda mguu wake,atautafuna huo mguu hadi ukatike aondoke zake bila huomguu
Kumbe ni kinunda na jeuri namna hiyo aisee.
 
Huyu ndiye wa kuitwa fungo ?
Kila sehemu wanajina wanalomwita sijajua kwa upande mwingine ila kwa sehemu niishio wanamwita kanu.
Na nimetega mwenyewe nimmnasa ananukia ubwa bwa mpaka sasa banda la kutegea linanukia
 
Tumekubaliana ni chatu huyo kanu katoka wapi?
Hakuna chatu anatoa harufu msidanganywe mi nakaa sana mapori huku.
Chatu anahema harufu kama mvundo fulani ambayo mnyamaakiisikia anavutiwa nayo mwenyewe anajipeleka hadi mdomoni mwa chatu.
Yaani ni kama unavyoona mamba akiwa nchi kavu anaachama mdomo kutega
 
Huyu ni mnyama mkali sana, mkorofi, na mwenye nguvu katika jamii ya paka.

Akiingia bandani, anondoka na kuku mzima na anaenda kula kichwa mpaka shingoni. Kama ni kifaranga, anakula chote au akikuta mayai ambayo bado kidogo ya yaanguliwe, ndio soshi wake.

Anakaa vichakani au porini, sehemu yenye msitu mkali. Akigundua kwamba yupo kwenye eneo lenye adui kama mbwa, chui, fisi au binadamu, anaachia ushuzi wake ambao unanukia kama wali au ubwabwa, kiasi kwamba utadhani mtu kaficha huo wali vichakani.

Kumekuwa na dhana kwamba ukisikia harufu ya ubwabwa vichakani, ni chatu. Hapana, sio kweli; ni huyu mnyama anayeitwa kanu katika Kiswahili (kwa huku mtaani, sijui upande mwingine).

Naendelea kutega; nikikamata nitawaletea mumjue.

Huyu nimetega baada ya kula kuku wangu sana.

Sasa nimetega nimenasa ananukia huo ubwabwa wao wanadai ni mti.
Niko tayari kujitokeza nimlete akiwakwenye mtego(kama atanasa tena )niwaletee hapo ofisini kwenu mjidhiirishe wenyewe kama mimo ni mwogo au laa.
Labda hapo kinachokinzani ni jin tuu la huyu mnyama ila mnyama nilokamata ni kama huyo huyo sijaona tofauti.labda jina tuu nimekosea sijajua maana nimeandika jina kulingana na wenyeji niishio nao wanavyomwita.
 
Nashangaa kwanin kuna baadhi ya watu wanamlalamikia bwana wa stendi kuhusu kumkill huyu faken
I think wengi wenu hamjawahi kufuga hasa kwa malengo.
Huu n mwez wa kumi, bado mvua chache tu sikukuu zifike, ukute tayari ushaandaa kuku wako uwauze ujazie ada watoto waende shule alafu huyu ubwabwa awale? Inauma sana.
Mimi kuna mbwa alikua amezoea kula mayai ya kuku wangu, siku moja nkamtaitisha kwenye 18, aisee alipokea kichapo heavy alikua analia zaidi ya ambulance. Sidhan kama atarudia tena.
Eti uite askari wa TANAPA, aje afanye nini?
Huyupangaji
 
Attachments

  • 20241012_081202.jpg
    20241012_081202.jpg
    687 KB · Views: 4
  • 20241012_081149.mp4
    5.8 MB
  • 20241012_081350.jpg
    20241012_081350.jpg
    245.7 KB · Views: 3
Mkuu umefanya kosa sana kumuua. Hao viumbe wapo hatarini kutoweka.
Mara ya mwisho kumuona Kanu vichaka makumbuka ilikuwa 1994.

Next time pigia simu Afisa wanyaporiTANAPA watakuja kumkamata sio kuwaua.
Yaani tanapa waje usiku kulinda kuku wangu ili wakamate mnyama ambae hawajui anatokea wapi? Huku ninakoishi ni karibu na msitilu wa makongo juu wanyama ni wengi sana waharibifu kama kenge kicheche na nguchiro ndio balaa nakama
 
Kumbe hilo la harufu ya wali umetupiga jamaa, dah!
Yaani tena mtego unanukia utadhani nimwemwagia huko huo ubwabwa.
Hata ukimgusa mikono inanukia hatani.
Yaani harufu yake ya ubwabwa naona ni mwili wote kama unavyosikia ile ya beberu
 
Mimi ninavojua kuna aina fulani ya majani jamii ya nyasi ya maeneo ya porini hukoooo ndo huwa yanatoa harufu hiyoo
 
Back
Top Bottom