SI KWELI Kanu ni Mnyama anayenukia harufu ya ubwabwa porini/vichakani

SI KWELI Kanu ni Mnyama anayenukia harufu ya ubwabwa porini/vichakani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Huyu ni mnyama mkali sana, mkorofi, na mwenye nguvu katika jamii ya paka.

Akiingia bandani, anondoka na kuku mzima na anaenda kula kichwa mpaka shingoni. Kama ni kifaranga, anakula chote au akikuta mayai ambayo bado kidogo ya yaanguliwe, ndio soshi wake.

Anakaa vichakani au porini, sehemu yenye msitu mkali. Akigundua kwamba yupo kwenye eneo lenye adui kama mbwa, chui, fisi au binadamu, anaachia ushuzi wake ambao unanukia kama wali au ubwabwa, kiasi kwamba utadhani mtu kaficha huo wali vichakani.

Kumekuwa na dhana kwamba ukisikia harufu ya ubwabwa vichakani, ni chatu. Hapana, sio kweli; ni huyu mnyama anayeitwa kanu katika Kiswahili (kwa huku mtaani, sijui upande mwingine).

Naendelea kutega; nikikamata nitawaletea mumjue.

Huyu nimetega baada ya kula kuku wangu sana.

Kanu.jpg
 
Tunachokijua
Kanu ni wanyama wadogo, Wanyama hawa ni warefu na wembamba wenye mkia mrefu, kichwa kidogo na masikio makubwa. Rangi yao ni nyeupe hadi njano na wana madoa meusi na mkia wenye miviringo. Mpaka sasa kuna spishi 17 za kanu zilizoainishwa.

330px-Rusty-spotted_Genet_%28Genetta_maculata%29_%2832484079077%29.jpg
Kumekuwa na hoja inayodai kuwa mnyama Kanu hutoa ushuzi wenye harufu ya wali pale anapohisi adui kama njia ya kujilinda.

Je, ukweli wa hoja hiyo ukoje?
JamiiCheck imepitia makala na tafiti mbalimbali kuhusu maisha ya Kanu ili kupata uhalisia wa madai kuwa Kanu hutoa ushuzi ambao una harufu kama wali na kubaini kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.

Kanu wana tezi zinazozalisha harufu ambazo zipo kati ya mwanzo wa mikia yao na karibu na sehemu ya haja kubwa. Tezi hizo za harufu hutoa majimaji yenye harufu ya mkojo ambayo kanu hutumia kwa mawasiliano, kuashiria maeneo yao, na wakati mwingine kuwatisha wanyama au maadui wanaowawinda.

Kama wanyama wengine wengi, kanu hutegemea kuacha alama za harufu kama njia ya kutoa taarifa kuhusu uwepo wao, hali yao ya uzazi, na mipaka yao kwa wanyama wengine.

Aidha, Harufu inayotolewa na tezi za kanu hainuki kama wali kam inavyodaiwa bali Kanu hutoa harufu ya mkojo kutoka kwenye tezi zao, harufu ambayo mara nyingi huelezwa kuwa kali na isiyopendeza, sawa na harufu ya wanyama wengine walao nyama.

Pia JamiiCheck imemtafuta na kuzungumza na Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja ambaye ameeleza kuwa harufu ya Ubwabwa au wali porini haihusiani na wanyama mbalimbali ambao wamekuwa wakihusishwa nayo, aidha amesema kuwa harufu hiyo hutolewa na aina fulani ya miti.

"Kuhusu harufu ya ubwabwa porini wengi huihusisha na wanyama mbalimbali. Lakini Kiuhalisia kuna aina fulani ya miti Mti kama Potato Bush (kiingereza) na Jina la kisayansi ni PHYLLANTHUS RETICULATUS ambayo hutoa harufu ya aina hiyo na sio Kanu wala Gamba la nyoka maana wengine wanahusisha na nyoka kujivua gamba".:-Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja
Nashangaa kwanin kuna baadhi ya watu wanamlalamikia bwana wa stendi kuhusu kumkill huyu faken
I think wengi wenu hamjawahi kufuga hasa kwa malengo.
Huu n mwez wa kumi, bado mvua chache tu sikukuu zifike, ukute tayari ushaandaa kuku wako uwauze ujazie ada watoto waende shule alafu huyu ubwabwa awale? Inauma sana.
Mimi kuna mbwa alikua amezoea kula mayai ya kuku wangu, siku moja nkamtaitisha kwenye 18, aisee alipokea kichapo heavy alikua analia zaidi ya ambulance. Sidhan kama atarudia tena.
Eti uite askari wa TANAPA, aje afanye nini?
 
Binadamu tuna kaukatili fulani, ilikua kwenye harakati zake za kutafuta riziki ili aweze kuendelea kuishi kwenye ardhi hii ya dunia kama vile tulivyo sisi ama hao kuku, ila ndio hivyo tena kakutana na binadsmuy mwenye ubinasfi .
Mkuu umeongea sahihi kabisa japo wanasema muindaji nae,huwindwa.
 
duuu Mungu Fundi.... harufu ya ushuzi inanukia ubwabwa!!!
Siku zote nilikuwa najua ni chatu... kumbe sio
Wengi tuliaminishwa hivyo tukiwa wadogo. Na tulikuwa tunakula relay ya kutosha tusikiapo hiyo harufu.
 
Kuna watoto wa mama huku wamezoea kukaaa kwa shemej hawajui ata ufugaji ulivo na gharama mkuu tena umemuua kistarabu sana ingetakiwa umcharange mapanga
 
Mkuu hujaelimika, lkn pia wewe sio mstaarabu hata tone na huna akili. Ina maana hujui kwamba unafanya makosa?? Kwanini unamtoa uhai na unapost upuuzi wako. Endapo unasumbuliwa na Mnyama wa aina hiyo ulipaswa kutoa taarifa kwa TAWA mamlaka ya Wanyapori wao wangemwekea mtego na kumpeleka mahala sahihi akahifadhiwe lkn kwa Umbumbu wako umemuua mnyama huyo halafu unaposti ujinga wako. Mpumbavu sana umenikera sana mkuu, ID zetu Zingekuwa zinautambulisho ungefuatwa na mkono wa sheria pimbi wewe.
No thanks kwa video hizi
Aisee....
 
Kuna watoto wa mama huku wamezoea kukaaa kwa shemej hawajui ata ufugaji ulivo na gharama mkuu tena umemuua kistarabu sana ingetakiwa umcharange mapanga
Akitoka akiwa hai kwenye mtego hapo utamkimbia nakuambia
 
Mkuu Kuna yule anaweza enda kwenye shimo akaingia mwili mzima akaacha mkunduh nje, huo mkunduh wake umejaa mavi mavi na mafunza yaliyoozeana... Ndege, kuku au mnyama yoyote akienda kula na kulamba huo mkunduh huyo mwamba atambana kichwa huyu mnyama mpaka afe....
 
Huyu ni mnyama mkali sana, mkorofi, na mwenye nguvu katika jamii ya paka.

Akiingia bandani, anondoka na kuku mzima na anaenda kula kichwa mpaka shingoni. Kama ni kifaranga, anakula chote au akikuta mayai ambayo bado kidogo ya yaanguliwe, ndio soshi wake.

Anakaa vichakani au porini, sehemu yenye msitu mkali. Akigundua kwamba yupo kwenye eneo lenye adui kama mbwa, chui, fisi au binadamu, anaachia ushuzi wake ambao unanukia kama wali au ubwabwa, kiasi kwamba utadhani mtu kaficha huo wali vichakani.

Kumekuwa na dhana kwamba ukisikia harufu ya ubwabwa vichakani, ni chatu. Hapana, sio kweli; ni huyu mnyama anayeitwa kanu katika Kiswahili (kwa huku mtaani, sijui upande mwingine).

Naendelea kutega; nikikamata nitawaletea mumjue.

Huyu nimetega baada ya kula kuku wangu sana.
View attachment 3119620
Kumbe ndo huyu. Siku moja usiku tulivu nimekaa zangu home. Mara nikaona kiumbe kinakwea mti kwa haraka sana. Kilikuwa ni hiki kiumbe kinafuata viota vya ndege, ilikuwa ni maajabu kwangu kwa mara ya kwanza kuona kiumbe hiki nikachukua camera nikipige ajabu ni kuwa hakikuonekana kwenye picha na sijui kilitokomea wapi?
 
Atakua alijificha
 
Back
Top Bottom