Kanuni Mpya Ligi Kuu Timu ikisajili mchezaji wa Kigeni atalipiwa ada ya Milioni Nane TFF

Ubaya Ubwela

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2024
Posts
1,353
Reaction score
3,060
Mchezaji yeyote wa Kigeni anayesajiliwa katika Ligi Kuu atalipiwa ada maalum ya Sh. 8,000,000 (milioni nane) kwa msimu ili usajili wake uweze kuthibitishwa na kuruhusiwa kucheza.

Kwa wacheaji 12 ni Sawa na 96M,

ni pungufu kidogo na pesa anayopata mshindi wa Ligi ya NBC.

CHAMBUA
 
Tamaa za tff wanavuna wasipopanda
 
Ni ujinga ujinga tu.

Ila ndugu muandishi ligi ya NBC bingwa sasa hivi anazidi hiyo 100, nadhani kwa sasani kama milioni 500 hivi.

Kakini bado naunga mkono hiyo bei ni kubwa sana, wangepunguza.
 
Safi sana, sio timu zinasajili wachezaji halafu zinashindwa kuwalipa mishahara.
 
Hiyo TFF ni swala pa muda tu kabla haijajugeuza dini ili ikusanye sadaka
 
Hili suala Lita discourage Sana timu ndogo kuweza kuhimili ushindani wa ligi ya ndani hata Yale mashindano ya kimataifa, unless tuamue kubakia na Simb, Yanga na Azam miaka nenda rudi
Down side but advantages ni kubwa zaidi
 
Yaan Bongo kila kitu ni futuhi, badala ya league kukua inadidimia
Hatareee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…