Kanuni Mpya ya Mpya ya TFF, Shindano la Jamii Ngao ya Jamii Kushirikisha Timu 4

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Kwa mujibu wa Barua iliyotumwa kwa vyombo vya Habari, Kupitia kwa Bodi ya Ligi, Bodi imeboresha kanuni ya Ngao ya Jamii ambapao kwa kwa kanuni mpya kutakuwa na shindano la Ngao ya jamii ambalo litashirikisha timu 3 za juu kwenye ligi, ambapo ikiwa timu ni mshindi wa kombe la FA na ipo kwenye nafasi ya 1-3 kwenye ligi basi atachukuliwa mshindi wa 4.

Aliye elewa Kanuni ya 19:1 Ufafanuzi please naona Mapicha picha tu.

Screenshot_20220815-192525.png
 
Kama hiyo barua ni kweli basi ngao ya jamii sasa itashirikisha timu nne, tatu zilizomaliza nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi, au nne, endapo bingwa wa shirikisho atakuwa miongoni mwa zile timu tatu zilizomaliza nafasi tatu za juu, hapo itachukuliwa timu iliyomaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

TFF wanapanua wigo wa mashindano waingize pesa zaidi.
 
Simple ni kuwa kutakuwa na shindano la ngao ya jamii ambalo litashirikisha jumla ya timu NNE . timu tatu zitatokana na mshindi wa kwanza , pili na watatu kwenye msimamo wa mwisho wa kumalizika ligi. Timu ya NNE ni bingwa wa kombe la FA. Ikitokea bingwa wa kombe la FA akawa miongoni mwa wale watatu . kama ilivyokua kwa yanga mwaka huu 😁😁😁😁 basi yule aliyeshika nafasi ya NNE kwenye msimamo ndiye atashiriki.
 
Naona TFF wamepata sehemu ya kupiga hela kwa kisingizio cha Ngao ya Jamii...

Kama mchezo wa ngao ya jamii ni CSR, (Kurudisha mapato yaliyopatikana katika mchezo huo kwa jamii) je Kwenye mechi ya juzi Yanga na Simba, mapato yalipatikana kiasi gani na kiasi gani kilirudishwa kwa jamii? au kwenye mechi zilizopita huko nyuma... Halafu mbona imekuja ghafla?

Binafsi naona hii kanuni ni ya kimaslahi zaidi
 
na ndio maana wamechukua zile top team,kuongeza hawasa na msisimko

Sasa basi km ni hv basi wakujibu kuhusu pesa za CSR toka mchezo wa juzi wa watani wa jadi zimefanya,then waendelee na hili
 
Wanataka kufanya kama spain ila wao spain inakua hivi

Mshindi wa ligi anacheza na mshindi pili wa fainali kwenye kombe

Mshindi wa pili ligi anacheza na mshindi wa kwanza fainali kwenye kombe

Then ndio kunakuwa na fainali.

Ya kwetu imekua tofauti kidogo. Nafikiri tff wameona timu za top 3 au top zitatoa wachezaji wazuri so mechi zitavuta mashabiki na mapato
 
Kama kigezo ni kuongeza Idadi ya mashindano basi bora wangerudisha kombe la Muungano kama ilivokua miaka ya nyuma.

Ngao ya Jamii ni mchezo wa ufunguzi wa Ligi na kurudisha kwa Jamii mapato yake ... sasa uliona wapi Ngao ya Jamii ikawa ya timu nne?
 
Kama hiyo barua ni kweli basi ngao ya jamii sasa itashirikisha timu nne, tatu zilizomaliza nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi, au nne, endapo bingwa wa shirikisho atakuwa miongoni mwa zile timu tatu zilizomaliza nafasi tatu za juu, hapo itachukuliwa timu iliyomaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

TFF wanapanua wigo wa mashindano waingize pesa zaidi.
Ni ujinga mtupu na kuchosha wachezaji. Hii wameitoa wapi? Ngao ya jamii ibaki mechi moja, haya mambo mengine no ufisadi na ulafi wa na tff
 
TFF chini ya uongozi wa Wallace Karia itaendelea kubakia kuwa taasisi ya kidwanzi mpaka siku huyu kiumbe atakapotoka madarakani!

Binafsi sijaona sababu yoyote ile ya msingi, ya kubadilisha huu utaratibu uliopo sasa.
 
Kwa hiyo bigwa wa fa hata shiriki
Simple ni kuwa kutakuwa na shindano la ngao ya jamii ambalo litashirikisha jumla ya timu NNE . timu tatu zitatokana na mshindi wa kwanza , pili na watatu kwenye msimamo wa mwisho wa kumalizika ligi. Timu ya NNE ni bingwa wa kombe la FA. Ikitokea bingwa wa kombe la FA akawa miongoni mwa wale watatu . kama ilivyokua kwa yanga mwaka huu 😁😁😁😁 basi yule aliyeshika nafasi ya NNE kwenye msimamo ndiye atashiriki.

Kama kigezo ni kuongeza Idadi ya mashindano basi bora wangerudisha kombe la Muungano kama ilivokua miaka ya nyuma.

Ngao ya Jamii ni mchezo wa ufunguzi wa Ligi na kurudisha kwa Jamii mapato yake ... sasa uliona wapi Ngao ya Jamii ikawa ya timu nne?
Wangerudiaha kweli Kombe la Muungano
 
Kwa mujibu wa Barua iliyotumwa kwa vyombo vya Habari, Kupitia kwa Bodi ya Ligi, Bodi imeboresha kanuni ya Ngao ya Jamii ambapao kwa kwa kanuni mpya kutakuwa na shindano la Ngao ya jamii ambalo litashirikisha timu 3 za juu kwenye ligi, ambapo ikiwa timu ni mshindi wa kombe la FA na ipo kwenye nafasi ya 1-3 kwenye ligi basi atachukuliwa mshindi wa 4.

Aliye elewa Kanuni ya 19:1 Ufafanuzi please naona Mapicha picha tu.

View attachment 2324727
Wameona Yanga anaenda kuchukua ngao ya jamii kwa mara ya tatu mfululizo, wameanza ngojera zingine! TFF poleni kwa timu kufungwafungwa na Dar Young African.
 
na ndio maana wamechukua zile top team,kuongeza hawasa na msisimko

Sasa basi km ni hv basi wakujibu kuhusu pesa za CSR toka mchezo wa juzi wa watani wa jadi zimefanya,then waendelee na hili
Kama TFF inaendeshwa kwa misingi ya ukweli na uwazi, yale mapato tuone yameelekea wapi..kusaidia jamii gani au kitu gani kwenye jamii
 
TFF chini ya uongozi wa Wallace Karia itaendelea kubakia kuwa taasisi ya kidwanzi mpaka siku huyu kiumbe atakapotoka madarakani!

Binafsi sijaona sababu yoyote ile ya msingi, ya kubadilisha huu utaratibu uliopo sasa.
ndio kwa mara ya kwanza duniani
 
Back
Top Bottom