Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani zachangia utulivu na amani duniani

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
VCG111504486925.jpg
Huu ni mwaka wa 70 tangu China kutoa Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani. Miaka 70 iliyopita, aliyekuwa Waziri Mkuu wa China Zhou Enlai alipendekeza kwa mara ya kwanza kanuni tano za “kuheshimiana mamlaka na ukamilifu wa ardhi, kutovamiana, kutoingilia mambo ya ndani, usawa na kunufaishana, na kuishi pamoja kwa amani”. Katika miaka 70 iliyopita, kanuni hizo zimekubaliwa na nchi mbalimbali duniani, na zimekuwa kanuni za kimsingi za kimataifa.

Miaka 70 iliyopita, China ilipendekeza Kununi Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani kutokana na maumivu yake ya kihistoria. Tangu vita vya Afyuni mwaka 1840, China ilianza kupoteza uhuru na usawa, ambapo ilivamiwa na kukandamizwa vibaya na nchi mbalimbali za kibeberu, mpaka Jamhuri ya Watu ya China ilipoanzishwa, na mikataba yote isiyo na usawa kati ya China na nchi za kibeberu kuondolewa.

Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani zinaendana kwa kina na Katiba ya Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa Katiba hiyo, madhumuni na kanuni za Umoja wa Mataifa ni kudumisha amani na usalama wa kimataifa, kuheshimu haki sawa za watu, kuheshimu mamlaka halali za nchi zote, kutatua migogoro ya kimataifa kwa amani na kuendeleza ushirikiano wa kimataifa.

Kinyume cha Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani ni Umwamba. Nchi zinazofanya umwamba hupuuza usawa katika sera zao za kidiplomasia, zinaamini kwamba nchi yenye nguvu inaweza kufanya chochote, na haina haja ya kujali maslahi ya nchi nyingine. Mwanzoni, mara China ilipotoa Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani, zilikaribishwa na kukubaliwa na takriban nchi 30 za Asia na Afrika ambazo zilikuwa zimepata uhuru kutoka kwa nchi za kikoloni, na kuanza kuwa silaha yenye nguvu ya kiitikadi kwa nchi zinazoendelea kushirikiana na kupambana na vitendo vya kimwamba vya nchi za magharibi.

Katika miaka 70 iliyopita, nguvu ya China imekua kwa haraka, na China imebadilika kuwa nchi kubwa zaidi ya kiviwanda kutoka nchi dhaifu ya kilimo. Lakini hali isiyobadilika ni kwamba China siku zote inashikilia Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani katika sera zake za kidiplomasia. Katika mambo ya kijeshi, China inaheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya nchi nyingine, na haijawahi kuvamia nchi yoyote. Katika mambo ya kisiasa, China haijawahi kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kushirikiana vizuri na nchi nyingine kukabiliana na umwamba. Katika mambo ya kiuchumi, China imeshirikiana vizuri na nchi nyingine ili kupata mafanikio ya pamoja.

Nchi za Afrika na China zina maumivu yanayofanana ya kihistoria, na zote zilivamia na kukandamizwa na nchi za kibeberu. Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani zinazotetewa na China zinakubaliwa sana na nchi za Afrika.

Uhusiano kati ya China na nchi za Afrika ulioanzishwa kwa kufuata Kanuni hizo una tofauti ya kimsingi na uhusiano kati ya nchi za kibeberu na Afrika. Katika miaka 70 iliyopita, China siku zote imeendeleza uhusiano na Afrika kwa mujibu wa Kanuni hizo, na kupata mafanikio makubwa.
 
View attachment 3028075Huu ni mwaka wa 70 tangu China kutoa Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani. Miaka 70 iliyopita, aliyekuwa Waziri Mkuu wa China Zhou Enlai alipendekeza kwa mara ya kwanza kanuni tano za “kuheshimiana mamlaka na ukamilifu wa ardhi, kutovamiana, kutoingilia mambo ya ndani, usawa na kunufaishana, na kuishi pamoja kwa amani”. Katika miaka 70 iliyopita, kanuni hizo zimekubaliwa na nchi mbalimbali duniani, na zimekuwa kanuni za kimsingi za kimataifa.

Miaka 70 iliyopita, China ilipendekeza Kununi Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani kutokana na maumivu yake ya kihistoria. Tangu vita vya Afyuni mwaka 1840, China ilianza kupoteza uhuru na usawa, ambapo ilivamiwa na kukandamizwa vibaya na nchi mbalimbali za kibeberu, mpaka Jamhuri ya Watu ya China ilipoanzishwa, na mikataba yote isiyo na usawa kati ya China na nchi za kibeberu kuondolewa.

Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani zinaendana kwa kina na Katiba ya Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa Katiba hiyo, madhumuni na kanuni za Umoja wa Mataifa ni kudumisha amani na usalama wa kimataifa, kuheshimu haki sawa za watu, kuheshimu mamlaka halali za nchi zote, kutatua migogoro ya kimataifa kwa amani na kuendeleza ushirikiano wa kimataifa.

Kinyume cha Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani ni Umwamba. Nchi zinazofanya umwamba hupuuza usawa katika sera zao za kidiplomasia, zinaamini kwamba nchi yenye nguvu inaweza kufanya chochote, na haina haja ya kujali maslahi ya nchi nyingine. Mwanzoni, mara China ilipotoa Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani, zilikaribishwa na kukubaliwa na takriban nchi 30 za Asia na Afrika ambazo zilikuwa zimepata uhuru kutoka kwa nchi za kikoloni, na kuanza kuwa silaha yenye nguvu ya kiitikadi kwa nchi zinazoendelea kushirikiana na kupambana na vitendo vya kimwamba vya nchi za magharibi.

Katika miaka 70 iliyopita, nguvu ya China imekua kwa haraka, na China imebadilika kuwa nchi kubwa zaidi ya kiviwanda kutoka nchi dhaifu ya kilimo. Lakini hali isiyobadilika ni kwamba China siku zote inashikilia Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani katika sera zake za kidiplomasia. Katika mambo ya kijeshi, China inaheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya nchi nyingine, na haijawahi kuvamia nchi yoyote. Katika mambo ya kisiasa, China haijawahi kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kushirikiana vizuri na nchi nyingine kukabiliana na umwamba. Katika mambo ya kiuchumi, China imeshirikiana vizuri na nchi nyingine ili kupata mafanikio ya pamoja.

Nchi za Afrika na China zina maumivu yanayofanana ya kihistoria, na zote zilivamia na kukandamizwa na nchi za kibeberu. Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani zinazotetewa na China zinakubaliwa sana na nchi za Afrika.

Uhusiano kati ya China na nchi za Afrika ulioanzishwa kwa kufuata Kanuni hizo una tofauti ya kimsingi na uhusiano kati ya nchi za kibeberu na Afrika. Katika miaka 70 iliyopita, China siku zote imeendeleza uhusiano na Afrika kwa mujibu wa Kanuni hizo, na kupata mafanikio makubwa.
Kwa sasa hivi China ni adui namba moja wa Afrika. Wizi wa rasilimali, bidhaa duni na hata unyanyasaji wa Waafrika.
 
Adui wa Waafrika ni Mzungu. Siyo mchina. Anayefadhili vikundi vya uasi Congo, Afrika ya kati, Chad, Niger, Mali n.k ni Mzungu. Anayeiba mali za Congo ni Mfaransa, Mmarekani na Mbelgiji n.k
Hayo ni mawazo yako, uliza tu kwa jirani Zambia wakuambie. Unajua hata hapa kujenga reli ya kati walipofika Moro walifanya kitu gani? Chadi, Mali na Niger zinasumbuliwa na makundi ya Kiislam kama yanavyosumbua Nigeria, Msumbiji, Ufilipino etc.
 
Adui wa Waafrika ni Waafrika wenzao wanaokubali kushirikiana na hao wanaolinyonya bara la Afrika.

Mzungu Wala Mchina hawawezi kuiba rasilimali zetu bila kupata msaada ama ushirikiano kutoka kwa Waafrika wenzetu aidha walio madarakani ama wanaowapa Silaha ili kuharibu amani. Hawatushikii mitutu ya Bunduki na kutulazimisha tuwape rasilimali zetu, bali ni upumbafu wetu wenyewe...
 
Hayo ni mawazo yako, uliza tu kwa jirani Zambia wakuambie. Unajua hata hapa kujenga reli ya kati walipofika Moro walifanya kitu gani? Chadi, Mali na Niger zinasumbuliwa na makundi ya Kiislam kama yanavyosumbua Nigeria, Msumbiji, Ufilipino etc.
Hayo makundi ya kiislamu hayajaletwa na China ila matokeo ya itikadi Kali za kiimani.
 
Back
Top Bottom