mnh!
Kaa ukifahamu kwamba, Katiba ya JMT Ibara ya 78(1) imeeleza wazi kwamba Wabunge Wanawake wa Viti Maalumu wanapendekezwa na chama!!
Hapo kabla, kabla ya akina Halima kuapishwa Katibu Mkuu wa CHADEMA alitamka wazi kwamba yeye hajapeleka majina NEC!! Tamko lake hilo lilitokana na yeye kutuhumiwa kupeleka majina NEC!
Baada ya akina Halima kuapishwa, tuhuma dhidi ya Mnyika zikahamia kwa Mbowe na hasa baada ya Halima kutamka hadharani kwamba wamepata baraka za Mwenyekiti!
Kamati Kuu ikawaita Halima wakajieleze, obviously wakathibitishe madai kwamba walipata baraka za Mwenyekiti!
HAWAKUTOKEA kwenye kikao!!
Ukiangalia huo mtiririko wa matukio unapata picha moja kwamba, the so-called COVID 19 walikusaidia, mosi kuuchafua uongozi wa juu wa chama, na pia kuwagombanisha viongozi hao na wanachama kwa sababu ni kweli, both Mbowe na Mnyika kwa vipindi tofauti waliandamwa sana kuhusika na hujuma hizo!!
Katiba ya CHADEMA inasemaje kuhusu hayo?
Kuhusu Maadili ya Viongozi, Ibara ya 10.1 ( ix) inasema:-
Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi au vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa Chama au wanachama wake.
Kabla ya kugusa vifungu vingine, viongozi waliopo ndani ya COVID-19 wanakuwa wamevunja Maadili ya Uongozi kwa kwa kutaka kuchonganisha au kuzua mgogoro ndani ya uongozi na wanachama wake kama ilivyoonekana dhidi ya Mbowe na Mnyika!!
Hivi kuna serious crime kama hiyo?! Jibu NDIYO kama ilivyolezwa kwenye Ibara ya 3.a (iii) kwamba:-
Usaliti katika Chama litakuwa ndilo kosa kubwa kuliko yote kwa misingi ya kimaadili. Pamoja na mambo mengine, kosa la usaliti litajumuisha matendo kama Kupinga misimamo ya Chama hadharani na nje ya vikao vya Chama.
COVID-19 kwenda kuapishwa bungeni inakuwa ni kupinga msimamo wa chama hadharani na nje ya vikao vya chama, na kwa mujibu wa ibara husika, huo ni USALITI na Usaliti ndio kosa kubwa kuliko yote kwa misingi ya kimaadili!!
Wakati ibara ya mwanzo kabisa, yaani Ibara ya 10.1. (ix) hapo juu ilikuwa inawahusu viongozi peke yao, Ibara hiyo ya 3.a.iii inawahusu viongozi na wasio viongozi! Kwa maana nyingine, kundi ZIMA limetenda USALITI kwa mujibu wa Ibara ya 3... hiyo ni kwa Viongozi na Wanachama!!!
Pamoja na ibara hizo hapo juu, pia Viongozi wamevunja Ibara ya 10.1 (xi)
The question is: Adhabu ya Aina Gani na kwa Namna Gani!!!
Ibara ya 5.4.3 inasema mwanachama atakoma kuwa mwanachama kwa:-
Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa Katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo usioendana na Itikadi, Falsafa, Madhumuni, Kanuni, Maadili na Sera za Chama. Mwanachama atakuwa na haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na adhabu hiyo.
Kwa maana nyingine, wala haina haja ya kuchoshana kuangalia Itikadi, Falsafa and other whatnot zinasema nini kwa sababu hapo juu tumeshaona wamefanya usaliti ambao ndio kosa kubwa kabisa la kimaadili kwa both, Viongozi na Wanachama!!
Kwa maana nyingine, haina haja ya kuchoshana kuangalia ikiwa akina Mdee walipaswa kuvuliwa uongozi kwa sababu so long as walistahili kuvuliwa uanachama kwa usaliti, automatically uongozi wao UNAKUFA kifo cha mende!!
Je, ni kweli kanuni ya Haki ya Kimsingi imevunjwa kama anavyodai mleta mada?! Ibara ya 5.4.4 inasema:-
Bila kuathiri kifungu 5.4.3 cha Katiba, Kamati Kuu inaweza kumwachisha ama kumfukuza mwanachama yeyote kwa utaratibu utakaopangwa na Kanuni za Chama
Nimepita pita huko mitaani na nimesikia COVID-19 wamefukuzwa uanachama na Kamati Kuu! Na hapo juu, inaonesha KK wanayo hayo mamlaka LAKINI, bila kuathiri Ibara ya 5.4.3 ambayo haijataja popote suala la Siku 14 uliloleta mtoa mada!!!
Now,
dndagula umetoa wapi hayo mambo ya Siku 14?! Unaweza kutuwekea vifungu husika?!
NInachojua mimi, ofcourse kwa mujibu wa katiba, hao watu wanapewa siku 30 za kuweza kukata rufaa, na Ibara ya 6.5.5 inatoa room kwa mwanachama aliyewahi kufukuzwa uanachama kuomba kwa maandishi kurejeshwa chamani!!
Mkuu
TUJITEGEMEE,
Nimeona kwenye thread moja uki-argue ikiwa wale uliowaita Mabwenyenye wa CHADEMA wamefuata katiba kufanya maamuzi!!!
Badala ya kuandika tena, jibu ni hilo hapo juu... NDIYOOOOOOOOOO, WAMEFUATA KATIBA, na hivyo kukuonesha what I said earlier is not impartial or even near cuz' y'all guys wanna make people believe CHADEMA violated their own constitution while spraying DDT to COVID-19 Virus!!