Nimetafakari sana kisheria kuhusu kufukuzwa akina Mdee uanachama ninapata shida kidogo. Sina uhakika kama suala hili lilifanyika with due diligence. Hii ni kwa sababu kwa hali ya kawaida walipaswa waandikiwe barua ya mashtaka (kimaandishi)kuhusu makosa/tuhuma zinazowakabili na wapewe muda wa siku 14 kuzijibu na utetezi wao kuupeleka kwa mamlaka yao ya nidhamu ambayo ninaamini ni Kamati Kuu.
Aidha kamati kuu ingechambua utetezi wao kujiridhisha kuhusu tuhuma zao.
Vinginevyo kama kamati isingeridhika na utetezi ingehusisha pia kuunda Tume/kamati ya uchunguzi ili kuwahoji na kupata undani wa tuhuma hizo na kamati hiyo kuwasilisha mapendekezo yake kwa kamati kuu.
Hoja nyingine ya kujiuliza je kulikuwa na uharaka gani kuchukua hatua za kuwafukuza bila kuzingatia misingi ya haki "natural justice principle" kama ilivyo kwenye kanuni za nidhamu ili kukamilisha "administrative fairness procedures" kama kuna Sababu zenye madhara au athari mbaya zingeathiri chama chenu na kulazimisha kuchukua hatua za dharura bila mashtaka ya maandishi zilipaswa kujulikana wazi kwa wajumbe wa kikao hicho na watuhumiwa iwapo kama ndiyo ulikuwa msimamo wa kamati kuu ya CHADEMA.
Shauri hili likienda mahakamani kwa mazingira haya lina utata.
Tujadili kwa weledi