Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,422
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye safari ya kujenga utajiri, watu huwa wanashangaza sana.
Wengi wanapokuwa na miaka 20 na 30 huwa wanaona ni mapema sana kwao kuhangaika na kujenga utajiri. Hivyo wanajiachia na kutumia kipato chao vile wanavyotaka.
Wanapofika miaka 40, wanajiona wameshachelewa kuanza kujenga utajiri, kwa sababu ya kipato wanachokuwa nacho na matumizi makubwa yanayotokana na majukumu wanayokuwa nayo.
Katika pande zote mbili, wanakuwa wamekosea. Kwenye kujenga utajiri huwa hakuna kuwahi wala kutokea. Bali kila wakati kwenye maisha ya mtu ni wakati sahihi kwake kujenga utajiri.
Wengi wamekuwa hawajui hili na hivyo kujikuta wakipoteza muda na kushindwa kujenga utajiri kwenye maisha yao.

Kwa bahati nzuri sana, ipo kanuni ya kukokotoa thamani ya utajiri ambao mtu anapaswa kuwa nao kulingana na umri wake na kipato chake. Kwa kanuni hii hakuna kuwahi wala kuchelewa, bali unapata uhalisia wa maisha yako.
Kanuni hiyo ni kama ifuatavyo; umri wako zidisha kwa pato la mwaka gawanya kwa 10.
Kwa mfano kama una miaka 40 na pato lako la mwaka ni milioni 12, kwa kanuni inakuwa; 40 X 12 / 10 = 48. Hivyo kwa mtu mwenye umri wa miaka 40 na ambaye pato lake la mwaka ni milioni 12, anapaswa kuwa na thamani ya utajiri wa milioni 48.
Baada ya kupata namba hiyo, mchezo haujaisha, bali sasa kuna kuitafsiri namba hiyo kwa kulinganisha na uhalisia wako.
Hatua inayofuata ni wewe kukokotoa thamani halisi ya utajiri wako. Unafanya hivyo kwa kujumlisha thamani ya mali zote unazomiliki na kutoa jumla ya madeni yote unayodaiwa.
Ukishapata thamani ya utajiri wako, unalinganisha na jibu ulilopata kwenye kukokotoa.
Kama thamani halisi ya utajiri wako ni mara mbili au zaidi ya jibu ulilokokotoa, upo kwenye njia ya kujenga utajiri mkubwa kwenye maisha yako. Endelea na hayo unayofanya, kwani utafika pazuri zaidi.
Na kama thamani halisi ya utajiri wako ni chini ya nusu ya jibu ulilokokotoa, upo kwenye njia ya umasikini. Unapaswa kuchukua hatua za haraka sana kutoka kwenye njia hiyo kwani inakupoteza.
Pale unapojikuta upo kwenye njia ya umasikini, hatua ya kwanza kuchukua ni kupunguza sana matumizi yako, kuwa bahili hasa.
Kisha chukua hatua ya kuongeza zaidi kipato chako, kuza kipato chako huku ukidhibiti matumizi yako yasizidi na kumeza kipato hicho.
Kwa kuanzia na hayo, utaweza kutoka kwenye umasikini ulionasa na kujenga utajiri utakaokupa uhuru wa maisha yako.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimefafanua zaidi kuhusu kanuni hii ya kukokotoa utajiri. Karibu ujifunze kwa kina zaidi kutoka kwenye kipindi ili ujue pale ulipo sasa na hatua za kuchukua ili kwenda mbali zaidi.
View: https://www.youtube.com/watch?v=3K1TK0cHewI
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
www.amkamtanzania.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.