Kanuni ya kukokotoa utajiri unaotakiwa kuwa nao kulingana na umri wako

Kanuni ya kukokotoa utajiri unaotakiwa kuwa nao kulingana na umri wako

Ndio maana ukisoma sana unakuwa mjinga uko tranquility kama nyumbani ujakuta mali basi jitoe shiriki sana shughuli za wenzako ila utakapokuwa na jambo lako wenzako waje kwaiyo unajitoa uku u afanya kazi kupata pesa ukodi shamba ukupata pesa unakodi shamba kubwa msimu wa kilimo ukifika unaita wenzako ulioenda wasaidia kulima mashamba yao zamani wanakuja wanakusaidia hapo una imani kuwa msimo wa mavuno navuna mavun9 yakiwa mazuri nanunua shamba langu

Kweli kijana akivuna ananua shamba lake anaweka malengo mwakani nalima nikivuna nikiuza naoa kweli anavuna anaoa anaweka malengo mwakani nalima nikivuna naunua mifugo kweli anaunua mifugo anaweka malengo tena mwakani nikivyna nauza mifugo naongeza shamba na kweli anavuna anafanya hivyo anaweka tena malengo mwakani nikivuna najenga kwakua ana aridhi kubwa kweli anajenga anaweka tena malengo umeona sijui yani mipango tu sasa hawa wenye shule Mungu anajua yeye
Asee kusema ukweli sijakuelewa mkuu
 
Rafiki yangu mpendwa,

Kwenye safari ya kujenga utajiri, watu huwa wanashangaza sana.

Wengi wanapokuwa na miaka 20 na 30 huwa wanaona ni mapema sana kwao kuhangaika na kujenga utajiri. Hivyo wanajiachia na kutumia kipato chao vile wanavyotaka.

Wanapofika miaka 40, wanajiona wameshachelewa kuanza kujenga utajiri, kwa sababu ya kipato wanachokuwa nacho na matumizi makubwa yanayotokana na majukumu wanayokuwa nayo.

Katika pande zote mbili, wanakuwa wamekosea. Kwenye kujenga utajiri huwa hakuna kuwahi wala kutokea. Bali kila wakati kwenye maisha ya mtu ni wakati sahihi kwake kujenga utajiri.

Wengi wamekuwa hawajui hili na hivyo kujikuta wakipoteza muda na kushindwa kujenga utajiri kwenye maisha yao.




Kwa bahati nzuri sana, ipo kanuni ya kukokotoa thamani ya utajiri ambao mtu anapaswa kuwa nao kulingana na umri wake na kipato chake. Kwa kanuni hii hakuna kuwahi wala kuchelewa, bali unapata uhalisia wa maisha yako.

Kanuni hiyo ni kama ifuatavyo; umri wako zidisha kwa pato la mwaka gawanya kwa 10.

Kwa mfano kama una miaka 40 na pato lako la mwaka ni milioni 12, kwa kanuni inakuwa; 40 X 12 / 10 = 48. Hivyo kwa mtu mwenye umri wa miaka 40 na ambaye pato lake la mwaka ni milioni 12, anapaswa kuwa na thamani ya utajiri wa milioni 48.

Baada ya kupata namba hiyo, mchezo haujaisha, bali sasa kuna kuitafsiri namba hiyo kwa kulinganisha na uhalisia wako.

Hatua inayofuata ni wewe kukokotoa thamani halisi ya utajiri wako. Unafanya hivyo kwa kujumlisha thamani ya mali zote unazomiliki na kutoa jumla ya madeni yote unayodaiwa.

Ukishapata thamani ya utajiri wako, unalinganisha na jibu ulilopata kwenye kukokotoa.

Kama thamani halisi ya utajiri wako ni mara mbili au zaidi ya jibu ulilokokotoa, upo kwenye njia ya kujenga utajiri mkubwa kwenye maisha yako. Endelea na hayo unayofanya, kwani utafika pazuri zaidi.

Na kama thamani halisi ya utajiri wako ni chini ya nusu ya jibu ulilokokotoa, upo kwenye njia ya umasikini. Unapaswa kuchukua hatua za haraka sana kutoka kwenye njia hiyo kwani inakupoteza.

Pale unapojikuta upo kwenye njia ya umasikini, hatua ya kwanza kuchukua ni kupunguza sana matumizi yako, kuwa bahili hasa.

Kisha chukua hatua ya kuongeza zaidi kipato chako, kuza kipato chako huku ukidhibiti matumizi yako yasizidi na kumeza kipato hicho.

Kwa kuanzia na hayo, utaweza kutoka kwenye umasikini ulionasa na kujenga utajiri utakaokupa uhuru wa maisha yako.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimefafanua zaidi kuhusu kanuni hii ya kukokotoa utajiri. Karibu ujifunze kwa kina zaidi kutoka kwenye kipindi ili ujue pale ulipo sasa na hatua za kuchukua ili kwenda mbali zaidi.


View: https://www.youtube.com/watch?v=3K1TK0cHewI

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.

Kamshauri Lucas mashambwa
 
Kwanza kwanini amegawanya kwa kumi ??kumi inawakilisha nini???atupe validation ya hiyo formulae

Motivesheno spika miyayusho sana.
Mungu akusamehe kwa kua hujui ulisemalo,wala unaloandika naona kabisa umekurupuka mkuu,,unapitwa na mengi kwa hii dunia ya mubimu kwa huo ushabiki ambao wewe ndo hujui upo wapi.
 
Kwanini wewe usiweke hapo kama mfano wa utajiri wako?

Pia hii inaongelea utajiri wa upande mmoja, kipato.

Kuna mambo mengine kama afya, utulivu wa akili, mahusiano n.k yanathamani kubwa pia.
Utajiri ni pesa mkuu,
Hayo mengine ni punyeto ya akili (mental masturbation), utajisikia vizuri ukiwa na mahusiano mazuri, lakini huwezi kwenda kununua nayo kitu dukani.
Hivyo basi, PATA PESA.
 
Huyu hata somo la hesabu alikula mshale ila leo amgenduq kanuni ya kujua utajiri mama.e
Mkuu, tuishie kubishana kwenye haya mambo ambayo mtu unaweza kuchagua upande unaptaka mwenyewe.
Lakini tukija kwenye masomo ya darasani, utajiabisha sana mkuu.
Nina ufaulu mkubwa sana wa masomo yote ambayo nimewahi kufanya tangu shule ya msingi mpaka chuo kikuu.
Hivyo njoo na hoja za saizi yako, hizo nyingine zitakutoa pumu bure.
Karibu.
 
Mwandishi wa kitabu Thomas J. Stanley yeye aliwaza vipi kutumia 10 na si 15, 20, 30, n.k.
Je, hiyo formula ni universal?

"Maisha hayana formula". "Utajili ni kitu uncertain"
Mkuu, kwa nini mwaka una miezi 12 na mwezi siku 30?
Maana unakomaa na kitu ambacho ni constant badala ya kuangalia picha kubwa.

BTW; "Maisha YANA formula". "Utajili ni kitu CHA UHAKIKA kabisa ukifuata kanuni sahihi."
 
Utajiri ni pesa mkuu,
Hayo mengine ni punyeto ya akili (mental masturbation), utajisikia vizuri ukiwa na mahusiano mazuri, lakini huwezi kwenda kununua nayo kitu dukani.
Hivyo basi, PATA PESA.

Unaelewa nilichokiandika? Hapo ungesema unalenga utajiri wa pesa. Napo Kuna watu wansupata Kwa kuiba, kudhulumu, kutapeli, kufanya kazi halali n.k

Upande wangu Bora niwe na pesa kiasi lakini nna mahusiano mazuri na watu.

Niambie hiyo kanuni ya utajiri wa pesa unayoihubiri isiyozingatia mambo mengine.
 
Mkuu, kwa nini mwaka una miezi 12 na mwezi siku 30?
Maana unakomaa na kitu ambacho ni constant badala ya kuangalia picha kubwa.

BTW; "Maisha YANA formula". "Utajili ni kitu CHA UHAKIKA kabisa ukifuata kanuni sahihi."
We hueleweki
 
Unaelewa nilichokiandika? Hapo ungesema unalenga utajiri wa pesa. Napo Kuna watu wansupata Kwa kuiba, kudhulumu, kutapeli, kufanya kazi halali n.k

Upande wangu Bora niwe na pesa kiasi lakini nna mahusiano mazuri na watu.

Niambie hiyo kanuni ya utajiri wa pesa unayoihubiri isiyozingatia mambo mengine.
Utajiri ni pesa mkuu,
Kwa sababu hizo ndizo tunazotumia kupata mengine kwenye maisha.
Maana hata mahusiano, yanakuwa magumu sana pale kunapokuwa na umasikini uliopindukia.
Na hilo unalosema bora uwe na pesa kiasi, NDIYO UTAJIRI WENYEWE.
Kila la kheri.
 
Utajiri ni pesa mkuu,
Kwa sababu hizo ndizo tunazotumia kupata mengine kwenye maisha.
Maana hata mahusiano, yanakuwa magumu sana pale kunapokuwa na umasikini uliopindukia.
Na hilo unalosema bora uwe na pesa kiasi, NDIYO UTAJIRI WENYEWE.
Kila la kheri.

Nani kakwambia utajiri ni pesa? Sema unaongelea utajiri wa pesa. Utajiri ni kuwa na wingi wa vitu.

Ndio maana mtu akiwa na mifugo mingi utaambiwa huyo ni Tajiri.

Kutafuta pesa ni majumuisho wa mambo mengi sana. Hiyo kanuni umeiweka hapo ni ya kupima matokeo ya migangaiko ya kuitafuta pesa.

Ukiwa na tabia za kitajiri (utajiri wa pesa) na kuelewa kanuni zake, hauhitaji hii formula umeiweka hapa.
 
Back
Top Bottom