Kanuni ya kukokotoa utajiri unaotakiwa kuwa nao kulingana na umri wako

Mkuu,
Mbona kama umedandia treni kwa mbele hivi?
Sioni uhusiano wa ulichoandika na nilichoandika.
Sikia mkuu, kama umechelewa, chukua hatua, makasiriko hayatasaidia.
 
Huenda hujakokotoa kwa usahihi.
Unaweza kutushirikisha namba zako hapa tuone? Kwa jumla tu, hatutaki kujua kuhusu wewe. Tupe umri, pato la mwaka na thamani ya utajiri wako kwa kuainisha mali na madeni.
Siwezi kutoa siri za utajiri na kipato changu.

Nina

*chombo cha moto,

*mali zisizohamishika,

*kazi yenye mshahara, na

*biashara.

Vyote hivi ndipo nimepatia jibu kwamba mimi ni moja ya matajiri.
 
Siwezi kutoa siri za utajiri na kipato changu.

Nina

*chombo cha moto,

*mali zisizohamishika,

*kazi yenye mshahara, na

*biashara.

Vyote hivi ndipo nimepatia jibu kwamba mimi ni moja ya matajiri.
Vizuri na hongera sana mkuu.
Endelea kutunza utajiri wako ili uendelee kuwa na manufaa kwa wengine kupitia kutoa fursa mbalimbali kwa wengine.
 
Ukisoma sana unakuwa mjinga yani mtu anakaa chini anachukua karamu na karatasi anaanza andika nadharia zake ambazo ni hewa na wala hazipimiki anasahau utajiri ni bahati wala siyo juhudi na marifa ingekuwa utajiri juhudi na marifa jamii yetu matajiri wangekuwa wengi sana tena sana
 
Nashkuru mungu maana mpaka sasa namiliki chombo cha moto ambae ni birika la kisasa la kuuzia al kasusu na kahawa. Pia namiliki usafiri kwa shughuli zangu phoenix new model bila kusahau ghetto la msonge.
 
Kama umechagua kuwa masikini, hakuna anayeweza kukulazimisha kuwa tajiri.
Na itakuwa vyema kama utakaa mbali na haya mambo ya utajiri, ili uendelee kuteseka vizuri na umasikini wako.
Kila la kheri.
Heheheh....ukichukulia kila kitu serious humu Jf, utabandua kucha nyuma ya keybord....
Nawe kila la kheri.
 
Kusema utajiri ni bahati ndiyo nimeona akili yako imekorogeka.
Ni kweli nilichoshirikisha hapa chaweza kuwa nadharia, ambayo haiwezi kufanya kazi kwa watu wote.
Lakini kwamba utajiri ni bahati, mbona wanaoshinda bahati nasibu au kurithi mali wanapoteza zote?
Kuna zaidi ya bahati mkuu, usikaze shingo, jifunze na uchukue hatua sahihi.
 
Utajiri siyo wa kila mtu kiongozi, ila maisha bora ndio yanawezekana kwa kila mtu endapo atajituma na kuwa na nidhamu ya maisha, naposema maisha naimanisha jinsi tunavyotakiwa tuishi kila siku nikiwa na maana ili tuishi yapaswa tufanye kazi yoyote ile harari yenye kuweza kukupatia kipato cha kukidhi mahitaji yako ya kila siku yani chakula, maradhi, na mavazi, mtu yoyote anayejituma kufanya kazi basi huweza kukizi hayo mahitaji ya msingi, pia aijue jamii yake inaitaji nini hasa upendo na amani kwani ukiwa na upendo na amani utakubalika na jamii yako na pia siraha kubwa ya mafanikio kimaisha ni uaminifu sasa hivi vitu vinawezekana kujifunza na kuvisimamia na kukuwezesha ukaishi kwa furaha kabisa katika jamii yako ila siyo utajiri bro utajiri si wa kila mtu

Utajiri sawa na mafanikio ya kipaji siyo kila mwenye kipaji anafanikiwa wanaofanikiwa ni wale wateule ambao Mungu kamua ikiwa Mungu ajamua pambana uwezavyo utakuwa daraja tu kwa wengine kwaiyo ni vizuri tukajitathimi je wewe wa fungu gani siyo kulishana matango pori kuwa ukifanya hivi utakuwa tajiri wewe acha ndio maana umesema hapo kuwa mbona wanaoshinda bahati nasibu hawawi matajiri yes kwanini wao si wateule wa kuwa matajiri wao ni wateule wa bahati nasibu bro utajiri ni issue nyingine na kuupata ikiwa wewe mteule haitaji nguvu ngoja nikupe mfano wa uteule

Marehemu magufuli kipindi anafundisha shule uko kina marehemu Lowasa kina marehemu Membe walikuwa kwenye system walijua A to Z za jinsi na njia za kuwa Rais nchi hii kina Mzee marechela nk walipambana wawezavyo kuutaka Urais wa inchi japo kujua kila kitu na kuwa na kila kitu ila hawakuwa wateule wa Mungu ila akaja Magufuli from no where kawa Rais, haya mama yetu huyu miaka kumi iliyopita sidhani kama aliwaza kuja kuwa Rais ila kwakua naye ni mteule wa Mungu kawa Rais

Sasa utajiri nao upo hivyo ila mafanikio ya maisha hayapo hivyo mafanikio yenyewe ndio yanaitaji ujitume siyo utajiri bro, nakupa mfano mwingine kuna watu leo hii wapo machimboni wanatafuta madini wawe matajiri na leo hii pale hospital amana kuna mama anajifungua mtoto baada ya miaka 20 uyu mtoto aliyezaliwa leo ataenda machimboni atamkuta yule mchimbaji ambaye yupo mgodini zaidi ya miaka 20 anachimba ila ana mafanikio tu hana utajiri ila uyu dogo anakaa mwaka mmoja tu shimo linaitika anakuwa tajiri kwanini ni mteule wa Mungu kuwa aje kuwa tajiri
 
Nadhani amekuelewa
 
Huu sasa ndiyo utajiri ninaouzungumzia mimi, siyo wa kuwa kwenye orodha au kuwashinda wengine.
Utajiri ninaofundisha mimi na ambao nataka kila mtu aupate maana yake ni hii; KUWEZA KUISHI MAISHA YAKO KWA NAMNA UNAVYOTAKA WEWE BILA YA KULAZIMIKA KUFANYA AMBACHO HUTAKI KUFANYA.
Ni hivyo tu, mengine ni mbwembwe.
Kwa hiyo narudia kusema Utajiri siyo tu unawezekana kwa kila mtu, bali ni haki ya kila mtu.
Tukirudi kwenye kanuni niliyoshirikisha, ili uweze kuishi maisha yako kwa uhuru bila kulazimika kufanya kitu usichopenda, unapaswa kuwa na uwekezaji ambao unaweza kukuingizia kipato cha kutosha kuendesha maisha yako hata kama hufanyi kazi moja kwa moja.
Hivyo basi, kwa kipato chako na umri wako, unapaswa kuwa unafanya uwekezaji ambao thamani yake inaendana kwa kanuni hiyo.
 
Bongo ishu ni channel sio umri😂, ukiwa kwenye line sahihi hauhitaji hata formula yeyote. Hata ukiwa 65 miaka 5 tu inatosha kusomba lumbesa za dollar.
Kwanza kwanini amegawanya kwa kumi ??kumi inawakilisha nini???atupe validation ya hiyo formulae

Motivesheno spika miyayusho sana.
 
Asante kwa mrejesho mkuu.
10 ni factor tu kwenye formula.
Formula hii sijaitunga mwenyewe, bali imetoka kwenye kitabu cha THE MILLIONAIRE NEXT DOOR, kilichoandikwa na Thomas J. Stanley na William D. Danko.
Karibu.

Sasa kwanini hauweki hizo acknowledgment kwenye Uzi?

Pia ni USD, GBP au TZS?
Na hiyo 12 unayozidisha na umri wako ni kitu Gani, kwamba makadirio ya kipato Cha 1M Kwa mwezi?
 
Huenda hujakokotoa kwa usahihi.
Unaweza kutushirikisha namba zako hapa tuone? Kwa jumla tu, hatutaki kujua kuhusu wewe. Tupe umri, pato la mwaka na thamani ya utajiri wako kwa kuainisha mali na madeni.

Kwanini wewe usiweke hapo kama mfano wa utajiri wako?

Pia hii inaongelea utajiri wa upande mmoja, kipato.

Kuna mambo mengine kama afya, utulivu wa akili, mahusiano n.k yanathamani kubwa pia.
 
Asante kwa mrejesho mkuu.
10 ni factor tu kwenye formula.
Formula hii sijaitunga mwenyewe, bali imetoka kwenye kitabu cha THE MILLIONAIRE NEXT DOOR, kilichoandikwa na Thomas J. Stanley na William D. Danko.
Karibu.
Mwandishi wa kitabu Thomas J. Stanley yeye aliwaza vipi kutumia 10 na si 15, 20, 30, n.k.
Je, hiyo formula ni universal?

"Maisha hayana formula". "Utajili ni kitu uncertain"
 
Kwanza kwanini amegawanya kwa kumi ??kumi inawakilisha nini???atupe validation ya hiyo formulae

Motivesheno spika miyayusho sana.
Ndio maana ukisoma sana unakuwa mjinga uko tranquility kama nyumbani ujakuta mali basi jitoe shiriki sana shughuli za wenzako ila utakapokuwa na jambo lako wenzako waje kwaiyo unajitoa uku u afanya kazi kupata pesa ukodi shamba ukupata pesa unakodi shamba kubwa msimu wa kilimo ukifika unaita wenzako ulioenda wasaidia kulima mashamba yao zamani wanakuja wanakusaidia hapo una imani kuwa msimo wa mavuno navuna mavun9 yakiwa mazuri nanunua shamba langu

Kweli kijana akivuna ananua shamba lake anaweka malengo mwakani nalima nikivuna nikiuza naoa kweli anavuna anaoa anaweka malengo mwakani nalima nikivuna naunua mifugo kweli anaunua mifugo anaweka malengo tena mwakani nikivyna nauza mifugo naongeza shamba na kweli anavuna anafanya hivyo anaweka tena malengo mwakani nikivuna najenga kwakua ana aridhi kubwa kweli anajenga anaweka tena malengo umeona sijui yani mipango tu sasa hawa wenye shule Mungu anajua yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…