Kanuni ya muhimu katika Drafti; "Ukitaka Kula nyingi nawe lazima ukubali kuliwa" ndio inayotumika sasa?

Kanuni ya muhimu katika Drafti; "Ukitaka Kula nyingi nawe lazima ukubali kuliwa" ndio inayotumika sasa?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Niliwahi kumsikia Mzee wetu, Rais Mstaafu Jakaya mrisho Kikwete akisema; ukikata Kula sharti nawe uliwe. Naweza kuwa sijanukuu Kama ilivyo lakini ujumbe ulikuwa na maana Sawa na huo.

Taikon ni moja ya wacheza Drafti mahiri Sana katika mchezo huo. Mabingwa wa Drafti wanajua kanuni hiyo ya kukubali kuliwa ili nawe ule nyingi zaidi. Katika mchezo wa Drafti ukijifanya mbahili Sana WA kuzuia kete zako kuliwa inaweza pelekea ukafungwa bao la mapema.

Hata hivyo Lazima tukubaliane kuwa katika kukubali kuliwa lazima kuwe na mpango mzuri wa Kula nyingi zaidi huko mbeleni. Na sio kuliwa tuu bila malengo.

Nafikiri Mzee kikwete atakuwa mchezaji wa Drafti na ndipo alipoutolea Msemo huu.

Kwa mwenendo wa awamu hii nafikiri kanuni hii inatumika zaidi; Rais ameona kanuni ya kukubali kuliwa ili nasi tule ndio itaisaidia nchi yetu.

Hata hivyo nampa angalizo Mkuu wetu WA nchi aangalie usijeliwa TUTUSA! Tukaishiwa na kete mapema kabla mchezo haujaisha.

Tuliwe Kwa mahesabu makali ili nasi tulambe asali,
Tuliwe Kwa adabu, ili nasi tule kiustaarabu
Tuliwe Kwa Raha isiyotabu, ili nasi tumung'unye kibubu Bubu!
Tuliwe mbili kasoro, tupate tatu kasorobo,
Wapate nusu Kwa nusu, nasi tule Pasi na kisu.

Anyway!
Mchezo wa Drafti huwahusu wajanja, mabingwa hawapigagi kelele, na ukiona bingwa kwenye Drafti anapiga kelele ujue ameshakukamata pabaya.
Ukiona bingwa yupo kimya wakati wewe kibushuti unatamba ujue unatafutiwa Angle nzuri.

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Wewe unaona inawezekana? Acha kuuliza maswali ya kitoto ila kufurahisha ego yako.

Mfano kwani Barrick gold aliyetafiti,kuweka mtaji,teknolojia na mwenye soko anakula sawa na Tzn?

Mimi kazi yangu kuuliza na kuchambua Mkuu!
Usinikasirikie!

Lakini Madini si yakwetu?
Watafiti wao na vifaa vyao lakini madini sio Yao Mkuu
 
Mimi kazi yangu kuuliza na kuchambua Mkuu!
Usinikasirikie!

Lakini Madini si yakwetu?
Watafiti wao na vifaa vyao lakini madini sio Yao Mkuu
Kama ni yako tafiti basi hadi ugundue kwamba kumbe ni madini xy na yana Kazi zt..

Kabla hayajagundulika sio yako.Kwenye geraza la Songwe watu waliweka gereza hata hawajui kuna nini hadi alipokuja kugundua mzungu kwamba kuna niobium .
 
Kwema Wakuu!

Niliwahi kumsikia Mzee wetu, Rais Mstaafu Jakaya mrisho Kikwete akisema; ukikata Kula sharti nawe uliwe. Naweza kuwa sijanukuu Kama ilivyo lakini ujumbe ulikuwa na maana Sawa na huo...
ukiona bingwa kwenye Drafti anapiga kelele ujue ameshakukamata pabaya.

Ukiona bingwa yupo kimya wakati wewe kibushuti unatamba ujue unatafutiwa Angle nzuri.

Hii nmeipenda
 
Back
Top Bottom