Kanuni ya usawa si kanuni ya kimaumbile, kanuni hii haiwezi kutumika katika Taasisi yoyote ile

Kanuni ya usawa si kanuni ya kimaumbile, kanuni hii haiwezi kutumika katika Taasisi yoyote ile

Me and me

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2023
Posts
393
Reaction score
730
Salam!

Kila Taasisi Lazima kuwepo na Mgawanyo wa Madaraka na Mgawanyo wa Majukumu ndani ya Taasisi Hiyo.

Yaani Lazima Kuwepo na Bosi Mwenye Mamlaka Ya Juu na Kuwepo na Wafanyakazi Wenye Mamlaka ya chini au ya kati na wenye Mishahara tofauti kabisa.

Hili Jambo ndio linafanya Taasisi zote Ziende vile zinavyoenda.(Kwa Sababu kuna Kuheshimiana)

Kanuni ya Usawa Haiwezekaniki.

Tunapokuja kwenye suala la Ndoa hii Pia ni Taasisi inayohitaji Bosi na Wale wachini yake wenye Kutii mamlaka ya Juu. (Kama Zilivyo Taasisi zengine zote)

Unapotambulisha Usawa wa Kimamlaka na Kimajukumu katika Ndoa(Familia) jee Taasisi hii Itaendelea kubaki 'Stable'??.

Au Ndio Kile tunachokiona Leo Hii Kuhusu Hii Taasisi ya Ndoa. TAASISI INAYOFELI NA INAYOENDA KUFA!!

Wanaotetea Haki sawa ndani ya Taasisi ya Ndoa. Hawaoni Haja ya kuwa na Haki sawa Kwenye Taasisi zengine pia? Kwani huko hakuna Binadamu???

Kanuni ya Kimaumbule na ya Asili ni UADILIFU NA SIO USAWA.

Uadilifu ndio unaohitajika katika jamii na Sio Usawa. Usawa hauwezekaniki Katika maisha ya kila siku...(Usawa utabaki kwenye makaratasi)

Kwaiyo ikiwa Mama atapewa Mamlaka sawa na Baba(tukisema ni Usawa),,

Pia Mama akapewa Majukumu ya Baba(Tukisema ni Haki) Jee Taasisi ya Ndoa itaendelea kuwa Imara??

Karibuni.
 
Back
Top Bottom