Mheshimiwa Dr. Slaa, wewe ni kiongozi, Mbunge wetu, huwezi kututamkia "Watanzania hawaelewi issues"!
Kisiasa inaonyesha hujali hata kutuonyesha unanyenyekea kwa tuliokupa taadhima ya kutuongoza, na ulivyo mwepesi kutumia lugha za kujumuisha watu jumla jumla na kuwashusha. Tafadhali Mheshimiwa.
Baadhi ya Wananchi tunadai kutodharauliwa na Waheshimiwa.
Kinnega,
Asante sana. Naomba radhi kama umekuwa "offended".
i) Kwanza sikuwa na nia ya ku "Offend yeyote", nimeeleza hali halisi. Ni vema ugonjwa ukijulikana kuliko kuuficha, kwani ukijulikana utapatiwa tiba. Ndiyo maana mara nyingi nimekuwa nikichukua muda mwingi kutoa "awareness" hata kwenye Forum hii ili wote tuwe na level mmoja ya jambo linalojadiliwa. Kuwa na kiwango kimmoja ni jambo muhimu sana, kwani forum hii ni forum pia ya kuelimishana. Hatuwezi kuelimishana iwapo hatutaonyesha kuwa hatufahamu jambo fulani.
2) Watanzania wana mambo mengi sana wanaelewa. Laini nimechagua makusudi neno " issues", na nikatumia "wengi", kubaini kuwa wako wanaoelewa na wako ambao pia hawaelewi. Nimetumia hapa neno hili kwa maana ya kutenganisha "issue" hasa ni nini. Ukisoma kwa makini hata kwenye magazeti, siku ya kwanza nilipoanzisha hoja hii kwenye Semina hakuna gazeti hata mmoja lilielewa, na hata Gazeti la Tanzania Daima, likatoka na kichwa cha habari "Cheyo na Slaa wajikaanga". Kati ya hoja iliyotoka ni kuwa wahusika hao walikuwepo au kuwakilishwa kwenye hafla ya kusaini sheria hiyo. Hata Tofauti kati ya Sheria na Kanuni hakuwa ameipata vizuri. Nadhani tuzungumze "practicalities" na siyo nadharia. Tutawasaidia Watanzania tukiwa wakweli, jasiri tunapoambiwa kuwa jambo hatulielewi ili iwe rahisi kupata elimu inayohitajika, na kadhalika. I normally call a spade a spade, hivyo, nisingeliwez kutafuta neno lingine kwa kuepuka kumwudhi mtu wakati ni dhahiri ninaona kuwa jambo halijaeleweka vizuri.
3) Kwenye jamvi hili hili tumekuwa tukieleza mara kwa mara tatizo la Watanzania ni nini hasa, kwanini watu hawako tayari kubadilika. Tatizo kubwa ni uelewa wa mambo. Nimekuwa vijijini, ukimwuliza mtu kwanini umepokea "kikombe cha Chumvi ( imetokea sana Bussanda, na au kipande cha Sabuni- Biharamulo) jibu ni kuwa ...anayenipa ananipenda. Ukienda mbele zaidi kuwa je thamani yako kwa miaka mitano ni kipande cha sabuni cha shs 200? Ndiyo anaanza kushangaa. Hivyo ndugu yangu tusiogope kusema ukweli ili tuwaokoe watanzania.
4) Issue kubwa ni kwanini "hatutaki kukimbilia mahakamani" na badala yake "iletwe miscellaneous Amendment"? Wengi wametaka nichukue hatua hiyo na wengine hata kuwa tayari wanichangie fedha. Lakini tungelikuwa na level mmoja ya uelewa "tungeliweka pressure au kutafuta avenue ya kuweka Pressure ili swala lirejee haraka Bungeni. This is the Issue. Naomba radhi tena kama umeudhika na kama wako wengine wameudhika kwa kuwa mwazi na direct. Thanks.