Ndekwakwise
Member
- Mar 22, 2010
- 49
- 3
Mhm! Jethro ulikuwa na mapungufu gani tena?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mkuu ikulu yetu na watendaji wake wengi hawako makini na kazi zao zilizowapeleka pale wanachofanya ni hicho tu(kamuhogo)lakini pia hakuna wa kuwasahisha make wengi wao ni haohao
Labda tu tuseme kwamba Rais hakusoma huo mswada; lakini kusema kwamba watu wa ikulu hawana umakini mimi kwa hili siamini. Yawezekana watu wa ikulu haohao wakishirikiana na baadhi ya vigogo ndio waliochomeka hayo mambo mageni. Wachomekaji lazima wawe ni watu wajanja, walijua fika wanachokifanya. Kumbe kuwalaumu watu wa ikulu kwamba hawakuwa makini si sawa vinginevo tuna uhakika hao wana-ikulu si washiriki wa hiyo mbinu chafu, tukimtoa Rais.
BAK,Sio Watendaji tu hata huyo Rais mwenyewe hayuko makini maana inaelekea hakusoma alichokuwa anasaini vinginevyo angeshtuka kabla ya kuweka wino.
Mheshimiwa Dr. Slaa, wewe ni kiongozi, Mbunge wetu, huwezi kututamkia "Watanzania hawaelewi issues"!
Kisiasa inaonyesha hujali hata kutuonyesha unanyenyekea kwa tuliokupa taadhima ya kutuongoza, na ulivyo mwepesi kutumia lugha za kujumuisha watu jumla jumla na kuwashusha. Tafadhali Mheshimiwa.
Baadhi ya Wananchi tunadai kutodharauliwa na Waheshimiwa.
Binti Sayuni, ktk familia yeyote, baba akiwa kalewa wakati wote na mama anapiga ukahaba saa zote unategemea watoto watafanya nini? Ndivyo ilivyo wa wasaidizi wa jumba kuu.Hivi haya mapungufu mbona yanatokea sana katika kipindi hiki cha huyu mkulu?
...acha kutoa excuse ya kijinga na rojo rojo wewe,huwezi kuongoza nchi kwa kubase kwenye ushauri na briefings!! yeye mwenyewe rais lazima ajue mambo yote kama yeye!!! asome miswaada ya sheria kikamilifu na kufuatilia mijadala ya bunge na kile wanachoamua yeye mwenyewe!! ndio maana watz tunarahisisha mambo holela holela tu, URAIS siyo briefings!!!! nchi nyingine kiongozi lazima athibitishe kwa dhati kwamba anafaa kwa kazi hiyo anayotaka!!!mkuu hivi unafikiri rais atapitia kiukamilifu mambo mangapi?? tena ya nchi nzima na mengine ya kimataifa?? usifanye mchezo mkuu!! ndio maana akawekewa wasaidizi ... laiti kama kila kitu angekuwa anafanya yeye basi nadhani angeshakuwa chizi!!
Walijua haya:
1)Kwamba muswada una mushkeli...
2)Rais hayuko makini
Kwa hiyo wakamsainisha mbele ya waandishi asije kukana saini yake baadae...HAIJAWAHI TOKEA katika nchi hii rais kusaini muswada kwa mbwembwe
Labda tu tuseme kwamba Rais hakusoma huo mswada; lakini kusema kwamba watu wa ikulu hawana umakini mimi kwa hili siamini. Yawezekana watu wa ikulu haohao wakishirikiana na baadhi ya vigogo ndio waliochomeka hayo mambo mageni. Wachomekaji lazima wawe ni watu wajanja, walijua fika wanachokifanya. Kumbe kuwalaumu watu wa ikulu kwamba hawakuwa makini si sawa vinginevo tuna uhakika hao wana-ikulu si washiriki wa hiyo mbinu chafu, tukimtoa Rais.
Kumbuka kashfa ya kutoa ambulance hakuna aliyewajibishwa.....huu mwenendo wa kubebana
Mpwa wataka kuniambia Mkulu huwa hapitii hayo makablasha kabla ya kusaini? au ndio kamtindo kake na ndio maana wana mwingiza mkenge? na walisha msoma kwa hilo?
Je sasa nani anatakiwa kuhakiki hayo makablasha kabla ya mkulu kumwaga wino wake?
Enzi za mwalimu JKN ukimleteaa issue tu kuhusu kitu fulani anakuambia nisha ipata 2hours ago unajiuliza vipi huyu mtu sasa mkulu tulie nae ni mpaka ameisha mwaga wino ndio anakuja shtuliwa tena na watu walioko nje ya IKULU hii si aibu kwa kiongozi mkubwa kama yeye na inaashiria si makini katika kuperuuuzii na kudadisi makablasha ya IKULU
Kumbuka kashfa ya kutoa ambulance hakuna aliyewajibishwa.....huu mwenendo wa kubebana
JKN alikuwa na watu ikulu ambao ni chapa kazi na alikuwa na watu wa usalama kila kona ikawa inamsaidia kujua kila kitu kiendeleacho