Elections 2010 Kanuni za Uchaguzi 2010 na mgogoro wa Sheria ya Gharama

Elections 2010 Kanuni za Uchaguzi 2010 na mgogoro wa Sheria ya Gharama

Status
Not open for further replies.
jambo la msingi ni kusoma na kuyaelewa vyema mawazo ya Dr.
kiukweli tunahitaji kuwa na mawazo na hoja mbadala katika hili
ni rahisi san ku-challenge pasipo evidence, ndio maana Dr katoa quotes kadhaa kwa ajili reference

Na makusudio yake ni kuomba mawazo ya wadau JF. nami kwa kutambua hilo nadhani nianze na mawazo yangu. Sitofautiana sana na wale walioshauri kujaribu njia ya kukimbilia mahakamani kwa sababu najua serikali hii iliyojaa 'Wachibya matwi' (watu walioziba masikio) tunaweza kupiga kelele wasitusikie na uchaguzi huo umefika.

Dr. Slaa anza na hilo inagwa kama aliyeusaini tena kwa mbwembwe aliulilia mapema na ndiye aliyeteua majaji tena wengi katika mahakama zetu, napungukiwa imani iwapo watakuwa tayari kumwangusha aliyewateua wakasimamia HAKI na KATIBA kuzuia uozo huyo.
 
Kama alivyosema Dr. Slaa sheria hii ni njema sana ila mia ni ovu na kila mpenda haki anaihitaji ili tuwe na viongozi wanaopatikana kwa ridhaa ya watu na si fedha lakin kinacho shangaza Bunge kazi yake ni kuridhia matakwa ya kamati ya wabunge wa CCM ndo maana dr. anasema baada ya kukarabatiwa sana ndio imekuja kwa sura hio kama walivyotaka na kanuni zitatungwa kama wanavyotaka kwa maslahi ya chama chao nao kubakia madarakani.Somo la chaguzi za serekali za mitaa linatosha kwa wenye akili pamoja na kelele zote walishinda kwa kishindo asilimia 93 bado wanakubalika na watanzania Kombani aliisaidis CCM hata Marmo ataisaidia CCM ishinde kwa staili ileile.

Dr. kwenda Mahakamani watanzania hawatakuelewa maana sheria imesainiwa hadharani kwa staili ambayo haijapata kutokea tangu tupate uhuru. Kazi kwenu wapenda haki !! MTAWEZA ?
 
Dr. Slaa,

Fanyeni petition Uchaguzi Mkuu uahirishwe hata ikiwezekana ufanyike December au Sheria hii mpya isitumike kabisa mwaka huu, na ianze kupitiwa upya na kufanyiwa kazi.

Je Bunge na Bungeni hamuwezi kupiga kura kusitisha muswaada huu kuwa Sheria?

Nakubaliana na wewe 100%. Sheria hiyo ni mbovu sana haina maslahi kabisa na haindelezi demokrasia bali inadumaza. Sheria ya uchaguzi ndio usiseme technically hakuna sheria ya uchaguzi, katiba nayo bado inadumaza demokrasia na tume ya uchaguzi ina muundo usokubalika.

Kwa maoni yangu, bunge haliwezi kupiga kura kusitisha muswaada kwani na tayari umesainiwa na sasa ni sheria kwa hiyo kinachotakiwa kufanywa ni kwenda mahakamani kupinga hiyo sheria chini ya basic rights and duties enforcement act kuwa sheria hiyo ina vipengeleambavyo vinapingana na haki za msingi zilizopo kwenye katiba.

Swali ni jee nani atafungua kesi hiyo, napendekeza Dr. Slaa awe petitioner katika petition hiyo na kama kuna watu na vyama vingine vinavyoona vitaathirika na sheria hiyo inawezekana wakajoin haitakuwa mbaya hata kidogo.
 
asante Dr. Slaa.. hii sheria ni mkuki tu; imeandikwa kwa kukurupuka bila kuangalia the unintended consequences. Na ukiangalia itaumiza sana demokrasia, uhuru wa vyama kuendesha mambo yao na ninaamini inaingia kwa kiasi kikubwa uhuru wa kujieleza kuliko sheria nyingine nyingi.
MM, kilichopo ni kitu rahisi mno, Watendaji wa serikali kwa maana ya wizara ya katiba na sheria na mawaziri wao woote na cabinet kwa ujumla jumlisha wana CCM wote , mara nyingi hutunga sheria kandamizi ama za hovyo hovyo kwa kufikiri kuwa wao watakaa madarakani milele na milele AMINA.

Hakuna mtunga sheria ama mleta sheria anaeegemea CCM anayeweza kuleta sheria ya kuweka mfumo wa sawa wa kisiasa........kwao wanalalia kwenye fikra za wao walindwe bila kufikiria maslahi ya taifa kwanza.
 
Kama alivyosema Dr. Slaa sheria hii ni njema sana ila mia ni ovu na kila mpenda haki anaihitaji ili tuwe na viongozi wanaopatikana kwa ridhaa ya watu na si fedha lakin kinacho shangaza Bunge kazi yake ni kuridhia matakwa ya kamati ya wabunge wa CCM ndo maana dr. anasema baada ya kukarabatiwa sana ndio imekuja kwa sura hio kama walivyotaka na kanuni zitatungwa kama wanavyotaka kwa maslahi ya chama chao nao kubakia madarakani.Somo la chaguzi za serekali za mitaa linatosha kwa wenye akili pamoja na kelele zote walishinda kwa kishindo asilimia 93 bado wanakubalika na watanzania Kombani aliisaidis CCM hata Marmo ataisaidia CCM ishinde kwa staili ileile.

Dr. kwenda Mahakamani watanzania hawatakuelewa maana sheria imesainiwa hadharani kwa staili ambayo haijapata kutokea tangu tupate uhuru. Kazi kwenu wapenda haki !! MTAWEZA ?
Kama nimemuelewa Daktari vizuri yeye hapingi sheria kwa sababu rais kesha pitisha muswada na umekuwa sheria., mara baada ya sheria kuna kanuni, na hizi ndo mhe anaona zina shida bado kuna nafasi kwa wanasiasa na wanaharakati kufanya utaratibu wa kuziboresha, CCM lazima wavutie kwao na tungesinzia tu ingekula kwetu.
ni muhimu kwa wanachama wa vyama vya siasa wanaotegemea kuwania nafasi mbalimbali za kuchaguliwa wakazisoma na kuzielewa kwanza sheria yenyewe na hizi kanuni, wasije fanya makosa otherwise CCM itashinda kilaini zaidi.
Asante Daktari!
 
KWanza sheria yenyewe na muda wa watu kujua ni mfupi sana na italeta vurugu kubwa sana kwenye uchaguzi, hivyo hawa jamaa walikuwa wanatungua kulingana na Chama chao kinasema nini, Hii ni mbaya sana katika Taifa lenye kujifanya linaenda kidemokrasia kama Tanzania. Hivyo kuna haja ya kukataa kwenda kwenye uchaguzi mpka vifungu vyote virekebishwe na watu kujulishwa sahihi. contradictions zote na katiba ni jambo baya sana kwenye uhuru wa vyama
 
Sheria ni nzuri kama itatumiwa kwa makusudi yaliyodhaniwa ila kuna baadhi ya vipengele vya kanuni vimewekwa utafikiri ni kanuni za chama kimoja mfano ile Mh Slaa anayosema kufikiri mfumo wa vyeo wa CCM uko sawa kwa vyama vyote (Regional Women Organ) kuna baadhi ya vyama havina viongozi wa ki-mkoa wana viongozi wa ki-kanda na kanda moja inaweza kuunganisha mikoa zaidi ya miwili vilevile kufikiri kila chama kinapata wagombea kwa kura za maoni si sahihi kuna baadhi ya vyama hawatumii mfumo huo wagombea aidha wanateuliwa au kupendekezwa au ku volunteer mwenyewe.
 
Ukijaribu kutazama maudhui ya sheria yenyewe utaamini kuwa wakati wanatengeneza kama vile walikuwa wamejifungua pekee yao chumbani na hakuna mdau yoyote yule alishirikishwa hata kidogo hapa kuna kazi kubwa sana katika kujua na kuona kuwa demokrasia ya kweli itakuwa Tanzania
 
sheria hii ipo kuwabana vyama pinzani na sheria hii kutaka vyama vingine kufuata utaratibu wa CCM ni makosa na huonesha kuwa sheria ilitungwa kukidhi matakwa yao.may democracy prevail na sheria hii kulekebiswa
 
Ningeziona hizo kanuni ndio ningeweza kumuunga mkono Mh. Dr. Slaa, au kutofautiana nae.
 
Sheria aliyosaini JK kwa mbwembwe yawaliza

na Irene Mark

MAKALI ya Sheria ya Fedha za Uchaguzi ambayo ilitiwa saini na Rais Jakaya Kikwete wiki moja iliyopita inaonekana kuanza kuwakoroga wanasiasa wa kambi ya upinzani walioshiriki kutoa ‘baraka zao’ kwake, wakati ikipitishwa rasmi kwa ajili ya kuanza kutumika.

Miongoni mwa viongozi wa vyama vya upinzani walioanza kukorogwa na sheria hiyo ni wale ambao wao wenyewe au wawakilishi wa vyama vyao walishiriki moja kwa moja katika hafla iliyojaa mbwembwe ambayo Kikwete aliitumia kusaini utekelezwaji wake.

Hali hiyo ya viongozi wa upinzani kukorogwa iliendelea kudhihirika jana wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya kuangalia namna wadau watakavyoitekeleza sheria hiyo kabla ya uchaguzi mkuu.

Baadhi ya viongozi walioonekana kupinga utekelezwaji wa sheria hiyo ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, ambaye katika hafla ya utiaji saini wa sheria hiyo chama chake kiliwakilishwa na Mkurugenzi wa Fedha, Anthony Komu.

Akizungumza katika semina hiyo, Dk. Slaa, ambaye pia ni Mbunge wa Karatu alisema sheria hiyo ilipitishwa kibabe bungeni na asilimia 80 ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika hali inayoweza kuibua maswali kadhaa, Dk. Slaa alisema wakati wa kujadili muswada wa sheria takriban wabunge wote wa kambi ya upinzani waliikataa.

“Kuna kipengele cha 3 (II) kinamtaka mgombea kujaza fomu EE1 itakayoweka wazi mapato yake na (III) kinamtaka mgombea kujaza kiasi cha fedha, vitu anavyoweza kutumia vitakavyothaminiwa kuwa fedha, chanzo cha mapato na kipindi anachotarajia kupata fedha hizo kwa ajili ya kampeni,” alisema Dk. Slaa.

“…Hii ni sheria yenye vipengele vingi vyenye upungufu na ilipitishwa bungeni kwa kura nyingi za wabunge wa CCM… tuliikataa sisi wapinzani lakini tulizidiwa nguvu na asilimia 80 ya wabunge wengi wa CCM,” alisema Dk. Slaa.

Alisema sehemu nyingine iliyolalamikiwa na wadau hao ni mgombea mwenye kura nyingi ndiye atakayesimamishwa na chama chake huku wakieleza kwamba kipengele cha kutangazwa kwa vyanzo vya mapato ya mgombea miezi mitatu kabla ya uchaguzi hakitekelezeki.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa kambi ya upinzani waliompa Kikwete ‘baraka zote’ za kusaini sheria hiyo, alisisitiza kwamba suala litakaloshindwa kutekelezeka kwenye sheria hii ni namna mgombea anavyotakiwa kueleza vyanzo vyake vya mapato kwa ajili ya kampeni.

Alisema, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa utekelezaji wa sheria yenyewe, haijawahi kutoa taarifa ya hali ya vyama vya siasa hivyo haitaweza kukagua fomu za wagombea wa ngazi zote hali inayoweza kusababisha uonevu kwa baadhi ya wagombea na vurugu kati ya msajili na wagombea.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, ambaye kama Lipumba alishiriki katika hafla ya kuipa baraka, alisema kusipofanyika marekebisho kama ilivyopendekezwa na wadau, sheria hiyo inaweza kuwa kitanzi cha wapinzani kutokana na mamlaka makubwa aliyopewa Msajili.

Kuhusu kueleza mapato ya mgombea, Cheyo alisema hilo ni jambo gumu kutokana na ukweli kwamba wagombea wengi hawana uwezo wa kueleza vyanzo vya mapato miezi mitatu kabla hivyo linaweza kusababisha fujo.

Kwa upande wake Msajili wa Vyama Vya Siasa, John Tendwa, alisema maoni ya wadau hao yatatumika kufanya marekebisho kwenye baadhi ya vipengele kabla ya kuanza kutumika rasmi kwa sheria hiyo huku akieleza kuwa ofisi yake itajitahidi kusimamia haki kwa wagombea wote bila kubagua.

Katika semina hiyo CCM haikutuma mwakilishi licha ya kualikwa kama vyama vingine.

Machi 17 mwaka huu, kwenye viwanja vya Ikulu Dar es Salaam, Rais Kikwete alitia saini sheria hiyo ambapo watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, mabalozi, viongozi wa dini na wanazuoni walihudhuria.

Sherehe hiyo zilihudhuriwa na viongozi wa vyama vya upinzani, na vyama vyao kwenye mabano ni pamoja na John Cheyo (UDP), Ibrahim Lipumba (CUF) Anthony Komu (CHADEMA).

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo vya Ikulu, muda mfupi baada ya sheria hiyo kusainiwa, Cheyo alisema mhanga wa kwanza kuathiriwa na sheria hiyo atakuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho viongozi wake ndio mabingwa wa kutumia fedha nyingi na kutoa rushwa.

“Hili ni suala jema kabisa kufanyika… lakini napenda kuwaambia, nawaonea huruma sana CCM kwa vile wao ndio watakuwa waathirika wa sheria hii… Wamekuwa majimboni kwa muda mrefu wakizunguka kila siku eti wanasema wanaimarisha chama!” alisema Cheyo.

Alisema kutokana na hali hiyo, chama chake hakitakubali tena porojo na kwamba kitakuwa cha kwanza kukataa fomu za wagombea kama Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haitakuwa makini katika utekelezaji wa sheria hiyo.

Kwa upande wake Profesa Lipumba, aliyekuwapo pia katika hafla hiyo, alipinga kitendo cha serikali kuikabidhi majukumu yote Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa madai kuwa haitaweza kutenda haki.

“Kama tulivyosikia Ofisi ya Msajili wa Vyama imepewa majukumu yote, sisi tunaamini haitaweza kutekeleza kwa ufasaha majukumu haya mazito… umefika wakati wa rais anapoandaa mambo haya kushirikisha kambi ya upinzani,” alisema Profesa Lipumba siku hiyo.

Naye Komu wa CHADEMA aliyekuwapo Ikulu siku hiyo, alisema chama chake kilikuwa kimepokea kwa furaha kubwa ujio wa sheria hiyo, kwa vile wao walikuwa wameipigania kwa muda mrefu. “Tumepigania sana sheria hii muda mrefu mno, tunatambua jinsi ilivyokuja na mapungufu… itasaidia baadhi ya mambo katika uchaguzi huu,” alisema Komu.
 
Dkt Slaa tupatie hiyo nakala ili tuchangie, otherwise mjadala huu utauvutia upande wako zaidi kwa sababu wewe uko more informed (una nakala ya Kanuni) kuliko sisi! Bila shaka umenielewa!
 
Kama kuna mtu mwenye kanuni hizo katika soft form naomba aturushie humu mtandaoni. Lakini hoja za Dr. Slaa zina msingi na zinajadilika. Nadhani wawe na forum ya kujadili kanuni hizo kama washika dau wa medani ya siasa nchini! Najua bado waziri mwenye dhamana anaweza kuwa kichwa ngumu lakini anaweza akawa challenged kupitia vyombo vya sheria pamoja na tume ya Uchaguzi na ya vyama vya siasa. Hata mahakamani ikiwezekana kama "omission ni material" sana!
 
Katika uchaguzi ujao, vyama vya upinzani vimsimamishe mgombea mmoja wa urais halafua waweke nguvu nyingi katika kupata wabunge wengi ili wawe na sauti bungeni.

Ni dhahiri kuwa JK atashinda tu uchaguzi ujao hata kama tukijifanya hatuelewi (CCM has locked in voters). Ni muhimu kuwa na wabunge wengi wa upinzani bungeni. Ni muhimu kuhakikisha kuwa katika majimbo ya wapinzan ya sasa, hakuna hata moja litakalokwenda CCM na pia Wapinzani waongeze majimbo mengine. Na hii itawezekana wakianza kufanya mchakato kuwa watamsimamisha nani kama mgombea wa upinzani katika kila jimbo. Ulafi na tamaa ziwekwe kando kabisa.

Tukipata bunge lenye aslimia hata 40 ya wapinzani nadhani itakuwa rahisi kushinda kwa kushawishi zaidi ya asilimia 10 wana CCM kuwaunga mkono bungeni hasa katika mambo yanayohusu mustakabali mzima wa nchi. Inawezekana kama tukinamini hivyo na kuchukua hatua.
Lazima vyama zifanye kampeni za watu kujiandikisha, bila kujiandikisha hupigi kura na bila kupiga kura wewe si sehemu ya mabadiliko.

Kada ya wafanyakazi huwa wanazembea kujiandikisha kupiga kura na hata kwenda kupiga kura lakini wanabaki wanalaumu wanatozwa kodi kubwa kwenye mishahara.

Hebu fikiria kodi anayolipa Mtanzania anayefanya kazi na kupokea mshahara wa zaidi ya laki tano:

PAYE=30%
NSSF=10% (hii ni kama mzigo kwani hizi hela pamoja na NSSF kuweka haziongezeki na jinsi shilingi inavyoporomoka kutokana na muda (time value of money not considered) inaishia kuwa mfanyakazi anaibiwa.
VAT(kwa kila unachonunua)=18%
Umeme (TANESCO)-REA na EWURA=(3+1)%
Maji (Dawasco)-EWURA=1%
kwa uchache hii ni kama 63%

Na nyingine kama import duty, fuel levy, exercise duty n.k kutokana na matumizi ya mfanyakazi. Zote hizi zinaifanya serikali kuchuwa fadha zote za mfanyakazi!!

Bado unatakiwa ulipie ada ya shule, matibabu, usaidie wazazi na ndugu kijijini, pango la nyumba, chakula cha kila siku, n.k.

Tunahitaji chama kitachotaka kuongoza kitueleze kwamba kitafanya nini kupunguza mzigo kwa wafanyakazi. Wafanyakazi tutumie network yetu kuhakikisha kua budget ya Jun/July ina maslahi yaliyoboreshwa kwa wafanyakazi hasa katika kupunguziwa mzigo wa kodi!!!!! Hii tunaweza na inabidi tuwaunge "TUCTA move" mkono kwa umoja wetu!! Think About It, Think Out of the Box, wafanyakazi wa serikali mnaweza kusema hamko affected kwa sababu serikali inalipa kama wahindi (mshahara mdogo halafu marupurupu mengi yasiyokatwa kodi ili kutolipa kodi) lakini regime will cha nge and you will feel the impact as well!!!!
 
Vema umeona haya DR. ila ilibidi uyatoe mkiwa bungeni. Jiwekeeni utaratibu wa kupitia kwa kina miswada kama group il mzuie na kuwaelimisha wenzenu consequences. Na hakika CCM hawatasikia nikinukuu kauli ya Kingunge kuwa ' mpiganapo mieleka humpi adui yako kisu'. Huo ndio msimamao wa CCM kwenu ninyi wa upinzani!!!
 
Dr Slaa,
Pamoja na mapungufu hayo uliyoyaainisha ambayo naamini utayafikisha kwa msajili (kama kifungu cha 30(2) cha sheria kinavyotaka) ni vema tukaanza mchakato wa kushinikiza mabadiliko katika sheria yenyewe.

Kwa mfano kifungu cha 30 (2) cha sheria kinamtaka msajili wa vyama vya siasa kuvipa daft reulations vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu kwa madhumuni ya kupata maoni kutoka kwa wananchi kabla ya kupeleka kanuni hizo kwa waziri. Hapa kuna shida.

Mimi nilitegemea sheria ingeenda mbele zaidi na kumtaka msajili baada ya kupata maoni chini ya kifungu 30(2), kuyazingatia maoni hayo. Kwa sheria ilivyo sasa msajili anaweza kupata maoni na kuamua kuyatupilia mbali bila ya sababu za msingi.
Wana JF,

Pamoja na kuitoa hapa, nakala pia nilipeleka kwa Msajili na imejadiliwa katika Semina iliyofanyika tarehe 22 March na 23 March. Kwa ujumla naomba niwaarifu kuwa karibu maeneo yote niliyoyataja yamepokelewa. Swala linalobaki ni je zitakubaliwa ziingie katika Kanuni na Waziri husika!

Pamoja na yote haya nimegundua jambo mmoja kubwa na baya. Kifungu cha 7 sha Sheria yenyewe iliyojadiliwa Bungeni, iliongezewa kifungu kidogo cha 2 yaani 7(2). Na ndiyo iliyopitishwa Bungeni. Mswada uliowasilishwa kwa Mhe. Rais, na kusainiwa na Rais, unasehemu ya 7(3) ambayo haikujadiliwa kabisa Bungeni. Nimeipitia Hansard, nimepitia Schedule of Ammendment, nimepitia na Majadiliano ndani ya Bunge katika Kumbukumbu Rasmi ya Bunge yaani Hansard, iliyoandaliwa tarehe 16/2/2010...

Inaelekea, katika hatua fulani, kati ya Draft hiyo na siku ya kuiwasilisha kwa Mhe. Rais, kuna mtu katumbukiza kifungu kipya cha 7(3); Kifungu hiki kinazungumzia Campaign Team. Kinasema kuwa Approving authority wa Campaign Team atakuwa Registrar of Political Parties kwa Presidential Candidate, na District Administrative Secretary (DAS) kwa Mgombea Ubunge, na Ward Executive Officer kwa Mgombea udiwani. Approving Authority ya Kampen Team haiwezi kuwa nje ya Chama husika, na hasa kuiweka mikononi mwa watu ambao ni watumishi wa Serikali ambao wengi wao kwa sasa wanafanya kazi ya Chama Tawala.

Kesho nitachukua hatua kuwasiliana rasmi na Ofisi ya Spika kujua hasa ni nani aliingiza kifungu hiki ambacho hakikujadiliwa na kuridhiwa na Bunge. Jambo hili ni baya, lakini pia linaweza kuwa Forgery ambayo ni kosa la Jinai. Nitawajulisha rasmi kesho.

Thanks for all your contributions. Mengine nitayajibu kwa wakati mmoja mmoja pale panapohitaji elimu maalum.
 
Wana JF,
Pamoja na kutitoa hapa, nakala pia nilipeleka kwa Msajili na imejadiliwa katika Semina iliyofanyika tarehe 22 March na 23 March. Kwa ujumla naomba niwaarifu kuwa karibu maeneo yote niliyoyataja yamepokelewa. Swala linalobaki ni je zitakubaliwa ziingie katika Kanuni na Waziri husika!

ndiyo maana mojawapo ya mapingamizi yangu ya sheria yenyewe ni hii nguvu tuliyompa mtu mmoja kuamua nini kinafanyika kwani mapendekezo mliyoyatoa hayamfungi Waziri kuyafuata na haitamzuia kuyabadiilsha with a stroke of a pen huko mbeleni. Waziri ana nguvu kubwa sana wakati na yeye mwenyewe ana maslahi ya chama chake.

Kwanini Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa au Tume ya Uchaguzi isipewe jukumu hilo na baadaye kuachiwa mwanasiasa, sielewi.

Pamoja na yote haya nimegundua jambo mmoja kubwa na baya. Kifungu cha 7 sha Sheria yenyewe iliyojadiliwa Bungeni, iliongezewa kifungu kidogo cha 2 yaani 7(2). Na ndiyo iliyopitishwa Bungeni. Mswada uliowasilishwa kwa Mhe. Rais, na kusainiwa na Rais, unasehemu ya 7(3) ambayo haikujadiliwa kabisa Bungeni. Nimeipitia Hansard, nimepitia Schedule of Ammendment, nimepitia na Majadiliano ndani ya Bunge katika Kumbukumbu Rasmi ya Bunge yaani Hansard, iliyoandaliwa tarehe 16/2/2010...

Inaelekea, katika hatua fulani, kati ya Draft hiyo na siku ya kuiwasilisha kwa Mhe. Rais, kuna mtu katumbukiza kifungu kipya cha 7(3); Kifungu hiki kinazungumzia Campaign Team. Kinasema kuwa Approving authority wa Campaign Team atakuwa Registrar of Political Parties kwa Presidential Candidate, na District Administrative Secretary (DAS) kwa Mgombea Ubunge, na Ward Executive Officer kwa Mgombea udiwani. Approving Authority ya Kampen Team haiwezi kuwa nje ya Chama husika, na hasa kuiweka mikononi mwa watu ambao ni watumishi wa Serikali ambao wengi wao kwa sasa wanafanya kazi ya Chama Tawala.
Na mimi nimeona mambo hayo vile vile na hata baadhi ya mambo ambayo nadhani yalikuwa sehemu ya mjadala sina uhakika yameandikwa kama yalivyokusudia kumaanisha.

Kesho nitachukua hatua kuwasiliana rasmi na Ofisi ya Spika kujua hasa ni nani aliingiza kifungu hiki ambacho hakikujadiliwa na kuridhiwa na Bunge. Jambo hili ni baya, lakini pia linaweza kuwa Forgery ambayo ni kosa la Jinai. Nitawajulisha rasmi kesho.
Je kuna uwezekano wa kufungua kesi ya Kikatiba kuzuia hiyo sheria kuanza kazi au kujaribu kuleta mapendekezo ya mabadiilko yake kwenye kikao chenu kinachokuja?
 
Vema umeona haya DR. ila ilibidi uyatoe mkiwa bungeni. Jiwekeeni utaratibu wa kupitia kwa kina miswada kama group il mzuie na kuwaelimisha wenzenu consequences. Na hakika CCM hawatasikia nikinukuu kauli ya Kingunge kuwa ' mpiganapo mieleka humpi adui yako kisu'. Huo ndio msimamao wa CCM kwenu ninyi wa upinzani!!!
Msavila,
Ni kweli tunahitaji sana kuelimishana jinsi Bunge linavyofanya kazi. Kanuni hazijadiliwi Bungeni. Zinatungwa na Waziri. Na kwa kawaida hatuna hata nafasi ya kuziona mpaka zinapoanza kutumika. Katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi, tulipigania hadi tukafanikiwa kuweka kifungu kinachosema kuwa Kanuni zitatungwa na Waziri kwa kushirikiana na Wadau.

Hivyo, Taratibu za Bunge ndizo zinazotoa utaratibu, huwezi kufanya tu kama unavyopendekeza kama haiko ndani ya Sheria au Kanuni za Bunge.
 
Je kuna uwezekano wa kufungua kesi ya Kikatiba kuzuia hiyo sheria kuanza kazi au kujaribu kuleta mapendekezo ya mabadiilko yake kwenye kikao chenu kinachokuja?

Mimi naamini inawezekana lakini kwa namna mahakama zetu zinavyofanya kazi, inaweza kuwa vigumu sana kufanya maamuzi magumu kama hayo ('kumwaibisha' Rais!).
 
ndiyo maana mojawapo ya mapingamizi yangu ya sheria yenyewe ni hii nguvu tuliyompa mtu mmoja kuamua nini kinafanyika kwani mapendekezo mliyoyatoa hayamfungi Waziri kuyafuata na haitamzuia kuyabadiilsha with a stroke of a pen huko mbeleni. Waziri ana nguvu kubwa sana wakati na yeye mwenyewe ana maslahi ya chama chake.

Kwanini Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa au Tume ya Uchaguzi isipewe jukumu hilo na baadaye kuachiwa mwanasiasa, sielewi.

Na mimi nimeona mambo hayo vile vile na hata baadhi ya mambo ambayo nadhani yalikuwa sehemu ya mjadala sina uhakika yameandikwa kama yalivyokusudia kumaanisha.

Je kuna uwezekano wa kufungua kesi ya Kikatiba kuzuia hiyo sheria kuanza kazi au kujaribu kuleta mapendekezo ya mabadiilko yake kwenye kikao chenu kinachokuja?
MMJ,
Njia pekee ya kutibu (redress hiyo situation) ni kwa Serikali kuleta Bunge la April Miscelaneous Amendment. Muda bado unatosha kufanya hivyo kama nia ipo. Hatua ya pili ni hatua ya kinidhamu baada ya kuchunguza nani alichomeka kipengele ambacho hakikujadiliwa na kuidhinishwa na Bunge, Hilo ni swala la kisheria na kinidhamu. Tutajua nini hasa kimetokea baada ya uchunguzi kamili kushirikisha Ofisi ya Bunge. Lakini ni hatari sana kumsainisha Mhe. Rais jambo ambalo halikupitishwa na Bunge.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom