Kanuni za Ushikaji

Kanuni za Ushikaji

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
Zifuatazo ni Kanuni kadhaa ushikaji/Uwana, ambazo wanaume huwa nazo na kuzifuata bila kufundishwa...
  1. Usitembee(mahusiano) na ex wa jamaa yako.
  2. Mshkaji akimuona manzi na akampenda na kukwambia, basi huyo manzi kashakuwa shemeji.
  3. Msaidie mshkaji kumpata huyo manzi, mpambe huyo mshkaji.
  4. Mkienda Kula bata, mgawane gharama.
  5. Usimtongoze wala kutembea na dada wa mshkaji, tena kaa mbali na ndugu wa kike wa mwana/ mshkaji.
  6. Usiruhusu mwana ajipige tattoo ya manzi/ demu.
  7. Kama mmekunywa, usije ruhusu mwana afanye kitu cha kijinga/kujidhalilisha
  8. Ukigundua shem anachepuka, mjulishe mwana...maamuzi juu yake.
  9. Kama shem akipiga na akauliza mwana yuko wapi, wewe sema mpo wote.
  10. Shem akiuliza kama mwana anachepuka, mtetee mwana kwa kila namna
  11. Mwana akiwa kwenye ugomvi, basi huo ni ugomvi wako pia.....
Ongezea na zako....
 
Zifuatazo ni Kanuni kadhaa ushikaji/Uwana,ambazo wanaume huwa nazo na kuzifuata bila kufundishwa...
  1. Usitembee(mahusiano) na ex wa jamaa yako.
  2. Mshkaji akimuona manzi na akampenda na kukwambia, basi huyo manzi kashakuwa shemeji.
  3. Msaidie mshkaji kumpata huyo manzi, mpambe huyo mshkaji.
  4. Mkienda Kula bata,mgawane gharama.
  5. Usimtongoze wala kutembea na dada wa mshkaji....tena kaa mbali na ndugu wa kike wa mwana/mshkaji.
  6. Usiruhusu mwana ajipige tattoo ya manzi/demu.
  7. Kama mmekunywa, usije ruhusu mwana afanye kitu cha kijinga/kujidhalilisha
  8. Ukigundua shem anachepuka, mjulishe mwana...maamuzi juu yake.
  9. Kama shem akipiga na akauliza mwana yuko wapi, wewe sema mpo wote.
  10. Shem akiuliza kama mwana anachepuka, mtetee mwana kwa kila namna
  11. Mwana akiwa kwenye ugomvi, basi huo ni ugomvi wako pia.....
Ongezea na zako....
If yo die, i die too.
 
Mwana akiwa kwenye ugomvi, basi huo ni ugomvi wako pia.....
Hii inaitwa 'royal to the gang' means ukimuua huyu maana yake umetuua Sisi wana wapo tayari kufa pamoja no matter what Ila kuna Wana ma-snitch hua wanaiua hii kanuni HAWAPO tayari kukupigania Ila wapo tayari uwapiganie na SIO kujipigania wenyewe, nawapenda wanangu wote wanaotembea nami bega kwa bega au waweza sema Sako-2-Bako on all ups and downs TAG zinasomana especially to my dopplegangers , double walkers & double goers wherever you're
 
Hiyo namba kumi na moja,mwaka fulani tulienda kikazi Mkoa X nyanda za juu kusini tulikuwa Mimi na mshkaji wangu wa ofisini,tukafikia lodge moja kama kawaida yetu. Baadae ya wiki mbili tukawa wennyeji pale lodge jamaa akajiopolea manzi fulani mtaa wa pili kutoka pale akawa anajipigia,kumbe siku za mwanzo kabisa jamaa alipita na cashier wa pub mule lodge.

Baadae jamaa ndio kupata huyo demu wa nje ambae alikuwa kisu kweli,sasa yule cashier akaanzisha bifu la chini chini na jamaa yangu,siku moja jumamosi tukaamka mapema tukaanza kupiga gambe pale Pub muda ya saa9 nikamwambia jamaa Mimi nachomoka hapa naenda club fulani kupata mdudu na kuendeleza gambe,jamaa kwa kuwa alikuwa na demu wake na washawaka akasema anaenda kumpuzika then ataamka aendelee nikasema pia. Nikachomoka zangu,mida ya saa4 usiku nikarudi ile kufika mlango mkubwa wa lodge naona watu wanakimbiana kutoka ndani,nikszama nikakuta jamaa anapambana na masela fulani pamoja na security guard wa ile lodge.

Wala sikuuliza shida nini,moja kwa moja nikadaka kiti cha mbao piga sana wale wajinga nikamchomoa jamaa,baada ya hapo tukaanza kuwatembezea kichapo cha mbwa mwizi,gonga sana pamoja na yule cashier,wakakimbia nje mule ndani lodge yote tukabaki wawili tuu. Wakatufungia geti kwa nje tukawasikia wanaita polisi jamaa akaniambia mwana twende fasta vyumbani tukakusanye vitu vyetu ndani ya dakika kumi tuwe tushasepa hapa,kama Polisi tutaenda wenyewe kesho. Kweli ndani ya dakika saba kusanya kila kitu tukaruka ukuta kwa nyuma hao tukaenda mbali kidogo kwenye lodge nyingine,hapa tulikubaliana kila mtu kwa kipindi Hili akae lodge yake ila za karibu kwa usalama wetu ili likitikea lakutokea tusife kama nyumbu.

Baadae namuuliza jamaa shida nini,akasema kuwa yule cashier alimpanga ex wa yule demu wa nje aje amfanyie fujo jamaa kama fumanizi hivi,ndio timbwili likaanza na jamaa yangu sio mnyonge mikono anaiweza.

Baadae yule demu akatuambia Polisi wala hawakuja,asubuhi akatuambia kuwa tuu alikuja Mkuu wa ile kampuni ya ulinzi pamoja na mmiliki wa lodge akachukua maelezo pale na yule demu akaongea yote ilivyokuwa,cashier akawa kikaangoni kutoka kwa Bosi wake, Bosi wake akapiga simu na kutuomba msamaha na kuomba turudi pale eti amepata hasara sisi kuondoka pale maana tulikuwa tukae miezi mitatu pale na tulikuwa tunamuungisha sana vinywaji tukagoma kurudi,cashier akapigwa chini. Baadae katika harakati za clubs tukakutana na yule ex wa demu tukiwa na yule demu,tukamfuata tukamwambia leo tunakuua, baadae atukumuona tena mule ndani,kesho yake nakutana nae sehemu anaomba msamaha oh yule cashier ndio alimpanga na kumpa bia na hela akitegemea eti sisi wageni eti tutasanda.
 
12.Wahskaji hawatumii kijiko kimoja(ku share) wakati wa kula...
13.Mshkaji Akija na manzi ndani,wote muondoke makazini hatakama ikiwa usiku.
14.Washkaji hawatekenyani
15.Mwana akitemwa, usimuache anywe peke yake.
16.Mwana ali ukwaju wa Bakhresa
17.Mwana wa mwana naye mwana kwako.
18.Mwana hajichagulii jina la utani, asubirie abatizwe...
 
Hiyo namba kumi na moja,mwaka fulani tulienda kikazi Mkoa X nyanda za juu kusini tulikuwa Mimi na mshkaji wangu wa ofisini,tukafikia lodge moja kama kawaida yetu. Baadae ya wiki mbili tukawa wennyeji pale lodge jamaa akajiopolea manzi fulani mtaa wa pili kutoka pale akawa anajipigia,kumbe siku za mwanzo kabisa jamaa alipita na cashier wa pub mule lodge.

Baadae jamaa ndio kupata huyo demu wa nje ambae alikuwa kisu kweli,sasa yule cashier akaanzisha bifu la chini chini na jamaa yangu,siku moja jumamosi tukaamka mapema tukaanza kupiga gambe pale Pub muda ya saa9 nikamwambia jamaa Mimi nachomoka hapa naenda club fulani kupata mdudu na kuendeleza gambe,jamaa kwa kuwa alikuwa na demu wake na washawaka akasema anaenda kumpuzika then ataamka aendelee nikasema pia. Nikachomoka zangu,mida ya saa4 usiku nikarudi ile kufika mlango mkubwa wa lodge naona watu wanakimbiana kutoka ndani,nikszama nikakuta jamaa anapambana na masela fulani pamoja na security guard wa ile lodge.

Wala sikuuliza shida nini,moja kwa moja nikadaka kiti cha mbao piga sana wale wajinga nikamchomoa jamaa,baada ya hapo tukaanza kuwatembezea kichapo cha mbwa mwizi,gonga sana pamoja na yule cashier,wakakimbia nje mule ndani lodge yote tukabaki wawili tuu. Wakatufungia geti kwa nje tukawasikia wanaita polisi jamaa akaniambia mwana twende fasta vyumbani tukakusanye vitu vyetu ndani ya dakika kumi tuwe tushasepa hapa,kama Polisi tutaenda wenyewe kesho. Kweli ndani ya dakika saba kusanya kila kitu tukaruka ukuta kwa nyuma hao tukaenda mbali kidogo kwenye lodge nyingine,hapa tulikubaliana kila mtu kwa kipindi Hili akae lodge yake ila za karibu kwa usalama wetu ili likitikea lakutokea tusife kama nyumbu.

Baadae namuuliza jamaa shida nini,akasema kuwa yule cashier alimpanga ex wa yule demu wa nje aje amfanyie fujo jamaa kama fumanizi hivi,ndio timbwili likaanza na jamaa yangu sio mnyonge mikono anaiweza.

Baadae yule demu akatuambia Polisi wala hawakuja,asubuhi akatuambia kuwa tuu alikuja Mkuu wa ile kampuni ya ulinzi pamoja na mmiliki wa lodge akachukua maelezo pale na yule demu akaongea yote ilivyokuwa,cashier akawa kikaangoni kutoka kwa Bosi wake, Bosi wake akapiga simu na kutuomba msamaha na kuomba turudi pale eti amepata hasara sisi kuondoka pale maana tulikuwa tukae miezi mitatu pale na tulikuwa tunamuungisha sana vinywaji tukagoma kurudi,cashier akapigwa chini. Baadae katika harakati za clubs tukakutana na yule ex wa demu tukiwa na yule demu,tukamfuata tukamwambia leo tunakuua, baadae atukumuona tena mule ndani,kesho yake nakutana nae sehemu anaomba msamaha oh yule cashier ndio alimpanga na kumpa bia na hela akitegemea eti sisi wageni eti tutasanda.
Huo ndiyo wana
 
Back
Top Bottom