Labani og
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 19,637
- 29,473
Mlinzi wa Timu ya Taifa Stars, Dickson Job amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo kati ya Tanzania dhidi ya wenyeji Uganda The Cranes uliopigwa katika dimba la Suez Canal, Ismailia Misri.
Stars iliibuka na ushindi wa 1-0 huku Simon Msuva alifunga bao pekee akiunganisha krosi iliyomiminwa nyota wa mchezo Job kutoka upande wa kulia wa uwanja mnamo dakika ya 68 ya mchezo.
Kwa ushindi huo Stars imekwea mpaka nafasi ya pili ikiwa na alama 4 baada ya mechi tatu nyuma ya kinara Algeria mwenye alama 9 baada ya mechi tatu.
Niger inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama mbili huku majirani Uganda wakiburuza mkia alama 1 baada ya mechi tatu.
Fact kuhusu huyu mwamba
-Licha ya kuchezeshwa nje ya position yake lakn bdo kaonesha kiwango kizur ndan ya mchezo bgap sanaaaa
-Huyu dick Kwa alivyokuwa anajua kupiga pasi hata akicheza Tisa kumi uhakika anajua dogo huyu mpira