Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Peter Jennings alikuwa nani na alisoma nini? Kama alisoma at all!
Huyu alikwa high school leaver.....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Peter Jennings alikuwa nani na alisoma nini? Kama alisoma at all!
Huyu alikwa high school leaver.....
Nyani,
Tim Russert alikuwa lawyer. Alianza kazi kama mshauri wa mbunge mmoja Capitol Hill. Tim Russert sijui na Katie kasomea TV journalism. Anyway, acha uvivu na wa-google mwenyewe:-
kwi!kwi!kwi!Siyo kwamba nimekuwa mvivu kutafuta hizo info mwenyewe (ingawa wakati mwingine huwa niko mvivu kusoma na kutafuta habari za mambo au vitu nisivyo na interest navyo). Swali au maswali yangu yalikwa rhetorical tu....
Hivi na wewe umesomea uandishi wa habari?
kwi!kwi!kwi!
Umejuaje?
Tido Mhando Na Mpendu Wana Elimu Gani?
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mhe. George Mkuchika amesema kuwa ni lazima kwa waandishi wa habari wa Tanzania kuwa ni wale waliosomea fani hiyo, kwani fani hiyo ni kama fani nyingine muhimu. Amesisitiza kuwa hata sheria mpya ya uhuru wa habari itazingatia jambo hilo. Ameyasema hayo leo katika hotuba yake ya makadirio ya bajeti yake ya mwaka huu. Bunge limepitisha bajeti ya wizara hiyo.
Kuna watu wengi tuu wanaoweza kujenga madaraja na kutengeneza transistor bila ya kwenda shule Je nao wawe wahandisi bila ya kusomea na kuwa na cheti cha uhandisi?1984 inaanza pole pole,
Kwanza watasema wasomee, halafu watasema wawe wanachama wa guild lao, halafu watasema guild lazima lipitishwe na NEC, halafu watasema lazima wawe na kadi za CCM, halafu watasema lazima waonyeshe shahada ya kura na ushahidi kuwa walimpigia kura mgombea wa CCM wa urais na ubunge... there is no stopping this.
Mwandishi wa habari lazima asomee, asomee nini sasa? Uandishi? Ina maana mtu mwenye PhD ya Philosophy hawezi kuwa mwandishi under that system? Kigezo cha kusoma kitakuwa nini?
Uandishi zaidi ya kuwa taaluma, ni kipaji na sanaa.Kuna watu hawajaenda shule lakini wanaandika vizuri kuliko waliosomea and vice versa.Sasa kwa nini kuweka mtego wa panya utakaowapata wanaotakiwa na wasiotakiwa?
.
Nadhani kinachotakiwa hapa ni kwamba wawe na elimu ya kiwango fulani inayowasaidia kuchambua mambo ya kuandika au kutangaza, siyo lazima elimu hiyo iwe ni katika Journalism tu. Sehemu nyingi duniani wanahabari maarufu hawakuosema journalism lakini wana taaluma fulani inayohusiana na aina ya journalism wanaofanya.
Watangazaji maarufu kule CNN hawana digrii za journalism lakini wana digrii zinazoendana na utangazaji wao: Dr. Sanjay Gupta ana M.D. (hivyo hutangaza mambo ya afya na tiba), Wolf Blitzer an M.A. katika international relations (na hupenda kutangaza habari za namna hiyo) , Lou Dobbs an M.A ya Economics (utangazaji wake unaendana na taaluma hiyo), Bill Schneider ana Ph.D ya political Science (hutangaza mambo ya siasa tu), Fareed Zakaria ana Ph.D ya international relations (hufanya inteviews zinazohusu mambo ya kimataifa).
Wote hao uliowataja walikuwa na digrii zinazoendana na utangazaji wao. Tom Brokaw ana digrii ya Political Science (kabla ya kuwa mtangazaji mkuu wa habari alikuwa akishughulika na habari za kisiasa), Tim Russert alikuwa na Juris Doctor (hivyo alikuwa akifanya interviews za kisiasa kwa mtindo wa cross-examination), na Katie Couric ana digrii ya American Studies (naye kabla ya kupanga ngazi alianza kama mtangazi wa mambo ya mitaani huko Miami).
Kuna watu wengi tuu wanaoweza kujenga madaraja na kutengeneza transistor bila ya kwenda shule Je nao wawe wahandisi bila ya kusomea na kuwa na cheti cha uhandisi?
Kwa sababu tu marekani muhandishi anaweza kuwa mtu yeyote asiyesomea haimaanishi kwamba ndio sahihi na wala haimanishi kwamba na sisi tufanye hivyo hivyo....
kama nchini mwetu tunaona kwamba ubora wa habari zetu utaboreshwa kwa kuwa na wahandishi waliosomea uandishi basi hatuna budi kufanya hivyo hata kama wengine hawafanyi hivyo... hiyo mifano mnayotoa ni mifano ya marekani kwa sababu hao watu ni maarufu huko haimaanishi kwamba ni wahandishi wazuri..
Uhandishi wa habari ni kazi kama kazi nyingine yeyote na ubora wake unatokana na kuelimishwa ktk hiyo fani (chuoni) na si viniginevyo.... mpaka sasa hivi hatujui njia nyingine yeyote ya kuweza kuthibisha ubora wa mtu ktk fani yake dhidi ya cheti cha uhitimu wa fani hiyo... kama un/mnafahamu njia nyingine tuambieni ambayo ni bora na tuanze kuingalia na tuone kama ni bora kuliko hiyo ya kusomea....
mkuchika inabidi tuanzishe na vyuo vya uwaziri,ili kila fani iwe na wasomi waliobobea.kwani mawaziri wamekuwa wanasaini mikataba bila utaalamu wa kutosha.
Hivi Mwanakijiji ana Degree ya nini?