Ninaomba kutofautiana na wewe hapa mkuu, hapa JF tupo wananchi wa namna mbali mbali na kutoka kwenye avenue nyingi na tofauti za maisha, kinachotukutanisha hapa ni uchungu wa taifa letu, na siamini kuwa ili kutoa hoja ikaeleweka ni lazima iwe katika form fulani ya uandishi, au uandishi uliotukuka au ulioenda shule,
Hii comment ninaiona kama ni an insult kwa wale tusioenda shule, au tusioweza kuandika kama unavyotaka wewe kwa maneno yako hapo juu, ninaamini kuwa wananchi wote wanaruhusiwa kuja hapa kutoa maoni yao, bila ya kujali shule zao au uwezo wao kuandika, kwa sababu tukifanya hivyo basi itabidi wengi hapa ambao hatukwenda shule tuondoke,
I mean sina uhakika na the point lakini naona kama you should have been a little bit sensitive na maneno yako hapo juu, sio wananchi wote waliosoma vizuri kama wewe na wengine mnaojua kuandika vizuri, kama ninakuelewa vizuri , waacheni wananchi hapa JF waandike watakavyo na wawezavyo, tukianza hizi hatuwezi kufika mbali maana huu utakuwa ni ubaguzi period, between waliosoma na wanoweza kuandika vizuri na wasioweza, JF tunapswa kuwa bigger than mawazo ya namna hii!
FMES, Agoostoons
Nafikiri hamjanielewa.
Kwa kuangalia mkao wa kisiasa, nimesema tamko la Waziri ni la kikandamizaji. Lakini ukizungumzia kama Taaluma, na hasa Uhariri, ndipo niliposema kuna ulazima wa kuwa na watu wenye fani ya Uandishi ambao kazi yao itakuwa ni kuhakiki kazi.
Nimeongelea tofauti zetu humu ndani (mimi ni kiwa mmoja wapo!) za kuandika bila kuweka vituo, iwe nukta au koma, sentensi kuanza na herufi ndogo au kuchanganya tungo (grammar) iwe kwa kiingereza au kiswahili na nikauliza je hili si somo la awali tunalofundishwa shule ya msingi? Je tuliosoma shule ya msingi mpaka sekondari si kila mwalimu alikuwa akisahihisha kazi zetu kwa kuangalia uzito wa tulichoandika na matumizi mazuri ya lugha sanifu, viuto na hata herufi?
Sasa kama sisi tutasema hakuna ulazima sana kujihakiki katika tunayoandika, iwe hapa JF au kwenye kubeba maboksi, kuna maana gani basi kushupalia kuwa ni lazima waandishi wawe na shahada au kila anayeandika kwenye gazeti awe na shahada ikiwa sisi zile nguzo za msingi wa uandishi (kuandika) hatuzifuatilii?
Suala si kujigamba kuwa fulani ni msomi au najiona msomi. SIna usomi wowote, hivyo kufuata kanuni za uandishi ambazo nakiri bado zanipiga chenga, hakuna maana kuwa najisikia au natukana watu.
Ikiwa tunapuuzia vitu vidogo vidogo kama kanuni za uandishi, kisa ni ghadhabu zetu kukoromea Ufisadi na kutetea maslahi ya Taifa, je tunauhakika tunaweza kufuata na kutii sheria nyingine bila kushurtishwa?
Uandishi wa habari ni fani, kama Uhandisi, Utabibu, Uhasibu, Ualimu, Ubwana Shamba, Mchumi na kazi nyinginezo. Kwa yeyote ambaye anataka kuwa mwandishi wa habari, basi ni lazima awe na uwezo wa kufuata kanuni za uandishi ambazo Augustoon amezitaja.
Tofauti inakuja kwenye kuandika maoni au makala. Haya ni mawazo ya mtu binafsi kutokana na upeo wake, sawa na utenzi wa mashayiri.
Lakini katika gazeti, redio na hata televisheni, ni lazima kuwepo na wataalamu wa fani ya uandishi, ili kuhakiki kazi, kuikosoa na kuiboresha kabla haijalishwa kwa jamii.
Sasa kama tayari tunalalamika udhaifu wa magazeti yetu kutumia lugha za mitaani na hasa Swangish kutoa habari, kosa hili halipaswi kuonyeshwa na kutoa mkazo lazima kuwe na uhakiki wa kuhakikisha kuwa habari au makala inapitiwa kabla ya kuchapwa?
Au kama habari ina mapungufu na walakini, si jukumu la mhariri kuhakiki facts na data kabla hajachapa ili gazeti lidumishe heshima?
Ikiwa kuwa mkweli kujikosoa na kusisitiza haja ya kujisahihisha kati yetu ni kosa la jinai, naombeni wana JF wote radhi.