Kapt. Mkuchika na Maagizo yake!

Nyani,
Tim Russert alikuwa lawyer. Alianza kazi kama mshauri wa mbunge mmoja Capitol Hill. Tim Russert sijui na Katie kasomea TV journalism. Anyway, acha uvivu na wa-google mwenyewe:-

Siyo kwamba nimekuwa mvivu kutafuta hizo info mwenyewe (ingawa wakati mwingine huwa niko mvivu kusoma na kutafuta habari za mambo au vitu nisivyo na interest navyo). Swali au maswali yangu yalikwa rhetorical tu....

Hivi na wewe umesomea uandishi wa habari?
 
kwi!kwi!kwi!
Umejuaje?
 
Tatizo Bongo tunapenda sana vyeti, lakini hatujajua kuwa vyeti havitusaidi kwani unaweza kuwa na digrii lakini kichwani sifuri. Sasa hao watu wanao-graduate kutoka vyuo vya uandishi wa Bongo ni vichekesh na ndio hao hao tunawaita wababaishaji. Sasa hivi hupati press card bila kuwa na cheti cha uandishi, so it's futile. Kama serikali iko committed to standard in journalism waanze with freedom of information act, alafu tuendelee na mengine....
 

Boooo, Boooo, Boooo, Boooo (inatamkwa Buu kizungu na si kwa matamshi ya kiswahili ambayo huleta maana nyingine)! au kwa kiswahili tutasema ziii, ziii, ziii!
 
Tanzania bado haijaondokana na mfumo wa Chama Kimoja na songombingo za Ki-Lenin, Mao au Stalin!

CCM wanaogopa sana Independent thinkers! Domancy (possibly not even a word but fits to display rotten minds of CCM!) ya CCM inawatoa jasho. Wana Mwenyekiti Kilaza ambaye kakiri kuogelea na mawimbi hayawezi, hivyo kila siku wakisoma chambuzi kuonyesha uozo wao, wanatafuta sheria mbali mbali kudumisha utawala na udhaifu wao.

Ngoja nimalize kusahihisha "Waraka wa Mchungaji" nitauchapa kwenye Magazeti yote ya binafsi waongeze chachu ya kunitafuta kisha nitawatwanga na "Mwanitafuta ni mimi" na kumalizia na Screw Muungwana!
 
Kuna watu wengi tuu wanaoweza kujenga madaraja na kutengeneza transistor bila ya kwenda shule Je nao wawe wahandisi bila ya kusomea na kuwa na cheti cha uhandisi?
Kwa sababu tu marekani muhandishi anaweza kuwa mtu yeyote asiyesomea haimaanishi kwamba ndio sahihi na wala haimanishi kwamba na sisi tufanye hivyo hivyo....
kama nchini mwetu tunaona kwamba ubora wa habari zetu utaboreshwa kwa kuwa na wahandishi waliosomea uandishi basi hatuna budi kufanya hivyo hata kama wengine hawafanyi hivyo... hiyo mifano mnayotoa ni mifano ya marekani kwa sababu hao watu ni maarufu huko haimaanishi kwamba ni wahandishi wazuri..
Uhandishi wa habari ni kazi kama kazi nyingine yeyote na ubora wake unatokana na kuelimishwa ktk hiyo fani (chuoni) na si viniginevyo.... mpaka sasa hivi hatujui njia nyingine yeyote ya kuweza kuthibisha ubora wa mtu ktk fani yake dhidi ya cheti cha uhitimu wa fani hiyo... kama un/mnafahamu njia nyingine tuambieni ambayo ni bora na tuanze kuingalia na tuone kama ni bora kuliko hiyo ya kusomea....
 

Kichuguu,

Kwa nchi iliyoendelea kama Marekani, ambao wenzetu huku degree ya kwanza ni kama form four huko kwetu, bado kuna waandishi maarufu kama kina Peter Jennings na Larry King ambao hawana/ hawakuwa hata na college degree.

Sasa kama wenzetu waliondelea na wenye pool kubwa ya wasomi wanathamini vipaji na kujituma kwa watu, na hawafungii mlango watu wenye vipaji lakini kutokana na makaratee ya life inawezekana hawakwenda shule (wengine wanaanza kuwa ma star wakiwa wadogo sana hata shule inakosa umuhimu, badala yake wao ndio wanakuwa shule!) . Haya hatuyaoni, tunaendekeza elimu ya mikaratasi bila kupima kitu kwa matokeo.

The twisted tool of the totalitarian tyrant tries too tactly to tacitly target timid Tanzanians.
 
mh.Mkuchika yuko sawa, niwakati sasa kila jambo lifanywe kwa utaalamu, tena kiwe cheti cha digrii, wenye MBA au Msc waneweza ruhusiwa kwa makala maalumu tu. Kuna vijana kama Iddi Ligongo waulizeni waliwezaje kusoma hii taaluma ya uandishi wa habari? Kama marekani hawasomi isiwe sababu na wakwetu wasisome!

Labda tuviombe vyuo kama TSJ na SAUT waanzishe evening and weekend programme musome.
 
Hivi Mwanakijiji ana Degree ya nini?
 

Waliotengeneza Ma Pyramid ya Gizah walikuwa na shahada ya wapi? Stonehenge? Zimba-bwe?

All I am saying ni kwamba kazi ipimwe kwa matokeo, sio kwa vyeti.Personally nina value elimu ya apprenticeship -ambayo ndiyo imetumika throughout the ages mpaka the 1600 hapa- kuliko elimu ya darasani.

Njia bora zaidi ya cheti ni track record, mtu anaanza apprenticeship na anapewa majukumu gradually kulingana na performance yake.Chema chajiuza kibaya chajitembeza.Vyeti ni kujitembeza, uwezo wa mtu hujiuza.

All over the "free" world, from India, the UK, to America people did/ are doing away with restrictive guilds, especially when it comes to freedom of speech and human rights. The suggested trend is contrary to that.

Inashangaza kuona mtu anaye value sana usomi wa darasani anakuwa na misgivings kuiga systems za watu ambao wana elimu ya darasani kwa sana.

The concern about freedom of speech and valuing unrestricted innovation is greater than some Vogon bureaucratic excuses to stifle freedom of expression.
 
mkuchika inabidi tuanzishe na vyuo vya uwaziri,ili kila fani iwe na wasomi waliobobea.kwani mawaziri wamekuwa wanasaini mikataba bila utaalamu wa kutosha.
 
mkuchika inabidi tuanzishe na vyuo vya uwaziri,ili kila fani iwe na wasomi waliobobea.kwani mawaziri wamekuwa wanasaini mikataba bila utaalamu wa kutosha.

Na chuo cha urais, tunaweza kunufaika tusitoe tena marais bomu kama hawa wetu, wazo la maana hili.
 
Waziri Mkuchika amesema kuwa, waandishi wa habari wa tz, wanatakiwa wawe wametathimiwa ili tupate waandishi wazuri, tusipate watu wasio na elimu ya uandishi wa habari. hii itapunguza kupata habari manung'ayembe. hili suala limezungumziwa sana na nchi ze jirani, kuwa tz hakuna waandishi wa habari.

Chukua mfano, MTU ANAEITWA JERI MURO wa ITV, yule jamaa hana hata akili ya uandishi wa habari, halafu ni mkorofi kishenzi. kuna siku nilimshuhudia akipigana na mgambo walipotaka kumchukulia kipazasauti na mikamera yao...ni mtu mwenye jazba sana mimi namshauri kama anataka kuendelea na uandishi wa habari, aende shule zaidi(tulisoma nae pale udsm).

ukikumbuka siku ile gorofa lilipodondoka kule mnazimmoja, utaona namna alivyokuwa anahoji yule injinia, huwezi amini kama ni mwandishi aliyeenda shule, becuase he does not ask maswali yenye point, anauliza vile yeye anavyofikiri ndivyo bila hata kutafuta uhakika wake. Tatizo,yeye kama mfano wa waandishi wengine, anahoji kwa kuhukumu kila mtu anaemkuta kwenye eneo bila kujua kama ni mhusika au la, matokeo yake anamwaibisha mtu asiyehusika. ndo maana utaona waliokamatwa na polisi ni wengine, yule ambaye JERI MURO alimtuhumu kama ni mzemba hakuhusika. mwisho, yule jamaa alipata jazba halafu akashindwa kumjibu vizuri, ....

Nilimsikia Jeri muro kwa masikio yangu akitamka maneno haya" Aloo, wewe usinijibu hivi, wananchi watakuua sasahivi ukifanya mchezo", kutokana na hilo, yaani kauli ya kichochezi kama hiyo, wananchi waliokuwa wamemzunguka pale, walianza kutaka kumvamia yule jamaa hadi polisi walipomchukua na kumweka kwenye gari yao kama vila wanamwokoa. lakini sio kwamba aliwekwa mle kwasababu alikuwa na kosa.
 
Nilisikia yote hayo kwa masikio yangu, na Jeri muro wa ITV namfahamu kwa njia ya tv tu. ila, huwa namshangaa hata mimi kusema ukweli, kwasababu anapohoji huwa anakuwa ni mtu wa jazba kama mtu wa mtaani/uswahilini vile. anajaji kabla ya kusikiliza maelezo. yaani, tz hatuna waandishi wazuri. tujifunze toka kwa wenzetu, kama mtu anatangaza mambo ya uchumi, inabidi awe mwandishi aliyesoma journalism halafu akasoma na degree ya uchumi, so it to every sector of journalism. sio kumchukua mtu aliyesoma kachuo fulani hivi pale buguruni au ilala. ndo maana watu wanawafanya kuwa matageti hivyohivyo.

Jeri alitoa kauli ya kichochezi siku ile. yeye alipofika pale kwenye jengo, tayari alikuwa ameweka kwenye mawazo yake kuwa mainjinia wa pale wote wabaya na wanatakiwa kufungwa bila kujua nani wenye makosa. ndo maana yule injinia alipofika kuhojiwa, jeri alikuwa anauliza maswali ya kumweka kifungoni na kama vile anamwamrisha, yaani kama vile yeye jeri na digrii yake moja, kama vile anamwamrisha vile, kumbe yule bosi. na kumwamrisha kwenyewe, alikuwa anamfokea na kuonyesha kuwa yule jamaa ni mzembe.

sijui kama hiyo ndo taaluma ya uandishi wa habari. kama humu ndani kuna waandishi wa habari wanaweza kulieleza hili. pia alitoa kauli ya kichochezi kusema kuwa jamaa atapigwa na wananch, apigwe kwasababu gani? je, hivi unafikiri kama ningekuwa mimi, umeniaibisha kwenye media kama vile halafu sina kosa, nitakuachaa? sikuachi, lazima nikutafute unaishi wapi nikufanyie. Mimi ni mwanasheria by profession, najua tu sheria zinazowahusu majonolisti, ila mengine siyajui. kama tunataka uandishi wa habari hapa tiz uungwe mkono na kila mtu, waandishi wa habari wanatakiwa wasiwe biased wanapofanya kazi zao.

you should not be biased whe you are asking questions, kwa njia hiyo, twaweza kupata ukweli halisi. being a mwandishi, sio mfalme, mtafungwa wengi sana kama hamtakuwa makini, na kama mtatoa habari msizokuwa na uhakika, mtayafilisi makampuni yenu, hamuoni SUMAYE ameshakula mill.100 kwa defamation yenu...hahaha, sisi wanasheria tunachekelea tu, tunataka watuletee watu ili tuwawakilishe tule hela za uwakilishi, hatuna shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…