Mwandishi gani aliwahi kuhoji wazi wazi mambo ya EPA,Rochimond,BOT na wenzake....kama si zaidi ya Kubenea na mwanahalisi.....Waandishi wa Bongo Makanjanja wasome wapanue mawazo yao mgando......bravo MkuchikaWataka waandishi wasomi wakati hata hao wanaowaita hawajasoma wakiwauliza maswali muhimu wanabaki kurushiana mpira.
Unafikiri sababu kubwa ya magazeti serous hayauzi ni hiyo?.....jiulize kwanini vitabu vya kupanua mawazo haviuziki hapa Bongo kuliko vile vya hadithi za Shigongo? hata magazeti kama raia mwema haliuzi sana kama magazeti pendwa kama kasheshe na wenzake
Vyeti, vyeti, vyeti! Tanzania tunapenda vyeti kama tunavyopenda ulabu na uloda as if it really matters!
Nimelifikiria tamko la Mkuchika kwa upande mwingine si wa kisiasa bali ni wa kielimu.
Nitaanzia hapa ndani uwanja wa fujo. Kila mmoja wetu ana utaalamu wa kuongea, lakini ukiangalia uandishi wa hoja na dataz, unagundua haraka haraka kuwa mtoa hoja, hajafundishika katika suala la uandishi. iwe ni insha au majibu ya kitu, kuna kuchanganya vituo, matumizi mabaya ya herufi kubwa na ndogo, mkazo na maandishi yasiyolingana alimradi mtu kaamua kujiongelea na kutoa maoni.
Sasa kama hapa JF tunatapia hizo hatutumii kanuni tulizofunsishwa tangu shule ya msingi hata kuangalia kuwa maneno tuliyoandika tunayapitia kuyasoma tuyaelewe kwanza sisi wenyewe kabla ya kumpa mtu wa nne ayasome, tunafikiriaje Waandishi wa habari Tanzania watakuwa na tofauti na sisi?
Si sisi wana JF tunaojivuna vifua mbele kuwa tumesoma, tunajua mambo mengi, sasa kama kanuni rahisi za uandishi (writing) zinatushinda, je hao wa Tanzania watakuwaje, wawe wamesoma TSJ Buguruni au UDSM?
Matatizo ya magazeti na Televisheni kuonekana kuwa ni vihiyo si kosa la aliyeajiriwa kama mwandishi, ni makosa ya mwenye mali na mhariri wa idara na mhariri mkuu.
Kama Mkuchika lengo la kutoa kauli yake ni kuhusu uhakiki wa habari kupitia wahariri na wahariri wakuu, ndipo basi kuna haja ya kuwa na waliosomea Taaluma ya Uandishi na wanajua umuhimu wa habari kufanyiwa tahariri na hata wale wanaoajiriwa kama waandishi wa makala, utangazaji au habari kwa ujumla.
Kwa hili la uhakiki na uhariri, nitamuunga mkono Mkuchika, lakini mnalosema wengine hapa kuwa kuandika makala au kutangaza n ilazima uwe na cheti cha TSj, nafikiri huko ni kujidanganya!
Alafu kuna kitu kingine hawa waandika habari wananikera...habari zao hazina uchunguzi na si za kitaalam.....najaribu kuangalia mwandishi gani anaeandika habari za financial sijaona.....huyu kaly Lyimo siku hizi haeleweki....
Huyu Ayubu Lyoba ambae ni mwalimu wa wandishi wa habari nae hana jipya...kipindi chake cha sema usikike hakina la yaani hajakifanya kiwe talk show kama tunazoziona ughaibuni
Hivi jamani kuna tatizo gani waandishi kusomea?kwani uandishi wa habari na utangazaji sio taaluma?hapa sasa wakuu ndio tunapoidhalilisha hii fani ya habari,fani hii inatakiwa ithaminiwe kama zilivyo taaluma nyingine ili hawa jamaa zetu wanaotundikia habari waweze kuwa na maisha bora,waweze kudai maslahi mazuri kwa waajiri wao,na waweze kufanya kazi kwa umakini hasa investigative journalism. Tukiangalia kwa mfano hawa waandishi wa BBC,VOA,CNN nk mbona wamesoma sana and they are proud of their professional hata maisha yao huwezi kulinganisha na mwandishi wa bongo.
Tunachokosea hapa ni kuona kwamba eti tukisema waandishi wasome tuna maana wote wawe na digrii hapana,elimu ipo ya ngazi mbalimbali,kuna certificate,diploma,higher diploma,first degree,second,na doctorates sasa tunahitaji waandishi katika ngazi zote hizo hapo juu,na maslahi yao yatofautiane kulingana na elimu na performance.
Pia kinachohitajika sasa ni kuwa na professional body ya kusimamia taaluma ya habari,ili kuoanisha mitaala na kusimamia ufundishaji wake kwa vyuo vyote vya serikali na binafsi, tofauti ilivyo sasa ambavyo vyuo vinavyotoa taaluma hiyo haviko coordinated wala supervised na specific body.Mwandishi hajui hata namna ya kujitetea akiandika habari ambayo mwingine anadhani ni defamatory.Sasa inabidi waweze kujua mbali ya kuandika vizuri pia wajue media law,law of tort,abc za katiba na uhuru wao,pia mipaka yao ili kesho na keshokutwa waweze kutetea maslahi yao.
Ni kwa kufanya hivi pamoja na mambo mengine taaluma hii itakua sana,wote hapa wanahusika wahariri na waandishi junior.
Mimi nasema wasome na kusoma sio lazima wawe na vyeti vya taaluma yao......kuna waandishi wengi tu maarufu hawajasomea taaluma ya habari lakini wanafanya kazi zao mpaka unapenda.....unaweza kuwa na taaluma ya biashara ukabobea kwenye habari za biashara....Hivi jamani kuna tatizo gani waandishi kusomea?kwani uandishi wa habari na utangazaji sio taaluma?hapa sasa wakuu ndio tunapoidhalilisha hii fani ya habari,fani hii inatakiwa ithaminiwe kama zilivyo taaluma nyingine ili hawa jamaa zetu wanaotundikia habari waweze kuwa na maisha bora,waweze kudai maslahi mazuri kwa waajiri wao,na waweze kufanya kazi kwa umakini hasa investigative journalism. Tukiangalia kwa mfano hawa waandishi wa BBC,VOA,CNN nk mbona wamesoma sana and they are proud of their professional hata maisha yao huwezi kulinganisha na mwandishi wa bongo.
Mimi naamini habari ni zaidi ya taaluma, it is the fourth estate.
Kwa hiyo, kwa kufuatisha uhuru wa vyombo vya habari na demokrasia, kila mtu awe na uwezo wa kuandika na kujieleza.
Juzi nilikuwa nasoma "The Economist" online edition, katika wachangiaji kuna bwana mmoja mwalimu wa art alikuwa analalamika kwamba zile article za uchumi ni nzuri sana lakini zinaandikwa kwa lugha iliyo technical sana na zinakuwa inaccessible.Labda haya ndiyo matokeo ya usomi mwingi, ndiyo sababu magazeti serious hayauzi sana.Labda tunahitaji waandishi wetu wawe respresentative ya population yetu, labda inabidi tuache kuwa condescend watu wasio na degree na stashahada kwani mfumo wetu wenyewe wa elimu ni sandakarawe amina, mwenye kupata apate, mwenye kukosa akose, kipapatikio cha kuku, kuna watu hawajafika chuo kikuu si kwa sababu hawana uwezo wa kishule au hawajafaulu, ila kwa sababu nafasi hamna.
Unaona hapo? Naelewa kuhusu standards na kwa kiasi fulani ninaweza kukubali hili when it comes kujenga madaraja, lakini kuhusu fourth estate this becomes a little bit too much.
It just sounds too much like Mkuchika using some clever guise to stifle freedom of the press.
Augustoons,
Kwa hiyo wanaosoma sheria Marekani, amabao inawabidi wasome bachelor somo lingine halafu degree ya sheria ni ya pili, hawawezi ku practise sheria bongo?
A bit off the track but of substantial interest to me nevertheless.
Mimi naamini katika freedom of expression, hata mjinga naye ana uhuru wa kujieleza ili mradi havunji sheria.Akivunja sheria mpelekeni kortini.Wajinga wa Tanzania wakiamua kuwa na gazeti lao na waandishi wao, wakawaacha wasomi na gazeti lenu, tatizo liko wapi?
Au wanaogopa hawa wajinga si wajinga hivyo?
Ninaomba kutofautiana na wewe hapa mkuu, hapa JF tupo wananchi wa namna mbali mbali na kutoka kwenye avenue nyingi na tofauti za maisha, kinachotukutanisha hapa ni uchungu wa taifa letu, na siamini kuwa ili kutoa hoja ikaeleweka ni lazima iwe katika form fulani ya uandishi, au uandishi uliotukuka au ulioenda shule,
Hii comment ninaiona kama ni an insult kwa wale tusioenda shule, au tusioweza kuandika kama unavyotaka wewe kwa maneno yako hapo juu, ninaamini kuwa wananchi wote wanaruhusiwa kuja hapa kutoa maoni yao, bila ya kujali shule zao au uwezo wao kuandika, kwa sababu tukifanya hivyo basi itabidi wengi hapa ambao hatukwenda shule tuondoke,
I mean sina uhakika na the point lakini naona kama you should have been a little bit sensitive na maneno yako hapo juu, sio wananchi wote waliosoma vizuri kama wewe na wengine mnaojua kuandika vizuri, kama ninakuelewa vizuri , waacheni wananchi hapa JF waandike watakavyo na wawezavyo, tukianza hizi hatuwezi kufika mbali maana huu utakuwa ni ubaguzi period, between waliosoma na wanoweza kuandika vizuri na wasioweza, JF tunapswa kuwa bigger than mawazo ya namna hii!
Rev. Umesomea uandishi lakini?
Watakuja mpaka humu na kusema ili kuandika JF inabidi uwe na degree ya Journalism, this is an online forum after all.
Kuhani,
Uandishi na utangazaji ni kipawa. Jennings nasikia alikuwa high school graduate. And he was one of the best.