Karakana ya Luban yathibitisha ushirikiano mzuri kati ya China na Afrika katika mafunzo ya ufundi stadi

Karakana ya Luban yathibitisha ushirikiano mzuri kati ya China na Afrika katika mafunzo ya ufundi stadi

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
VCG111397210809.jpg
Mkutano wa mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika hivi karibuni mjini Beijing, China. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na majukwaa ya ushirikiano ikiwemo FOCAC, China na Afrika zimehimiza ushirikiano wao katika sekta mbalimbali kwa njia ya kiuvumbuzi, mfano ukiwa ni karakana ya Luban, ambayo imekuwa alama ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika mafunzo ya ufundi stadi.

Karakana ya Luban iliyoko mjini Addis Ababa, Ethiopia, ina eneo la mita 830 za mraba, ikiwa ni pamoja na eneo la kufundishia aina tofauti za vyombo vya habari, eneo la kufanya mafunzo na semina, eneo la usimamizi wa kiviwanda, eneo la roboti za viwandani, eneo la mitambo ya umeme, ofisi na maghala, ambapo vifaa vyake ni vya kiwango cha juu zaidi nchini Ethiopita na hata duniani. Hadi sasa karakana hiyo imefanikiwa kutoa duru tano za mafunzo, na kuwafundisha karibu vijana 200 kutoka nchi za Afrika Mashariki zikiwemo Ethiopia, Kenya, na Tanzania.

Wallellgn Yonas Akele ni mwalimu wa Karakana hiyo, na anasema mafunzo wanayotoa katika karakana hiyo yanasaidia sana, na wanafunzi wanaweza kupata maendeleo makubwa, na baadaye kupata kazi nzuri kwa urahisi katika kampuni za kisayansi.

Karakana ya Ruban ya Ethiopia imechaguliwa na Umoja wa Afrika kama kituo cha mafunzo ya ufundi stadi barani Afrika, na inatoa huduma za mafunzo kwa ajili ya Mradi wa Benki ya Dunia katika eneo la Afrika Mashariki.

Karakana ya Luban ni sehemu ya ushirikiano kati ya China na Afrika wa kujenga uwezo katika Hatua Nane zilizopendekezwa na China kwenye Mkutano wa mwaka 2018 wa FOCAC, ambapo lengo lake ni kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wa Afrika. Tangu kuzinduliwa kwa karakana ya kwanza ya Luban nchini Djibouti mwezi Machi mwaka 2019, China imejenga karakana 17 za Luban katika nchi 11 barani Afrika, zikiwemo Kenya, Afrika Kusini, Mali, Nigeria, Misri, Uganda, Côte d'Ivoire, Madagascar na Ethiopia. Karakana hizo zinazingatia sekta zinazohitajika zaidi na nchi za Afrika zikiwemo reli, mashine, umeme, viwanda, magari, habari, madini, biashara ya mtandaoni, na akili ya bandia, na hadi sasa imewafundisha vijana zaidi ya 10,000 barani humo.

Karakana za Luban zinapongezwa na kukaribishwa sana na jamii ya Afrika, wakiwemo maafisa wa serikali, wasomi, vyombo vya habari na watu wa kawaida. Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Uganda, Elioda Tumwesigye anaamini kuwa, Karakana ya Luban itahimiza mchakato wa maendeleo ya mafunzo ya ufundi stadi, na maendeleo ya sekta za viwanda nchini Uganda. Kwa vijana waliopata mafunzo ambayo hawawezi kupata sehemu nyingine kutoka kwa Karakana ya Luban, wanashukuru kwa dhati Karakana hiyo. Owen Alikula, aliyesomea teknolojia ya habari katika Chuo Kikuu cha Machakos nchini Kenya anasema, karakana ya Luban ni darasa bora zaidi la mafunzo ya ufundi stadi, na kuwataka wanafunzi wenzake wajiandikishe na kupata mafunzo kwenye Karakana hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi vimeanza tena kupaka matope na kusema, China ina hila ya kisiri kwa kuanzisha Karakana ya Luban barani Afrika. Lakini bila shaka watakata tamaa kwa maana, China siku zote inazichukulia nchi za Afrika kama ndugu, na inatetea kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja na Afrika. Kwa kupitia Karakana ya Luban, China inalenga kusaidia Afrika kuendeleza mafunzo ya ufundi stadi, ili kupata maendeleo endelevu.
 
Back
Top Bottom