Nampa pole sana huyu kijana Mongela kwa kufanyiwa huu uhuni na huyu Fisadi. Ama kweli cha mlevi huliwa na mgema. Vya Mafisadi wanafaidi dada zetu ingawa mwisho wake inabidi walipe mshahara wa makosa hayo yao. Huyu dada nafikiri anaweza kuwa mke mzuri kwani fundisho alilopata hatalisahau milele, ila sema kipanga huyo anaweza kuwa kashayakanyaga mawaya na kwa maana hiyo bibie na yeye kashakuwa member akitafuta kugawia wengine .
Kinachonichanganya akili ni hii MONGELA kupewa kazi ya ukuu wa Wilaya. Yaani unaweza kukuta hata uwezo wake mdogo ila kapewa ili kumpoza maumivu aliyoyapata. Kwa maana hii, Watanzania tunaendelea kulipa au kubeba mzigo wa UJINGA wa hawa mafisadi. Sasa huko Kigoma kweli, watakuwa wamepata Mkuu wa wilaya wa maana? Mtu aliyeletwa ili kumpoteza machungu yake? Uongozi huu wa kupewa kama njugu sijui kama tutafika tunakotaka kwenda.
Au kwa sababu Waarabu wa Pemba hujuana kwa Kilemba? Maana nasikia kuna Kigogo mmoja alitembea na mke wa Mzee mmoja aliyejenga kigorofa chake huko Mbezi Beach karibu na barabara. Mzee huyo mwenye mtoto wa kike maarufu sana Dar es Salaam, aliposikia hivyo, basi akaamua KUJIUWA. Binti kwa sasa yuko Uarabuni kutokana na wana MAJUNGU. Kwa maana hiyo, naona Tanzania kama una mke mzuri basi kaa chonjo, mafisadi wa CCM watakuvamia sasa hivi. Ditopile yeye hadi alishikwa UGONI. Khaa, jamani. Hii nchi yetu? Pale nilipokuwa naishi Ilala Flats, alikuwepo mzaa wa Kipare na mke wake mzuri tu miaka ya 80. Huyu na yeye alinyanganywa mke na Naibu waziri mmoja. Mzee wa Kipare hadi leo nafikiri hajaowa tena. Huyu Marehemu Mgonja kafariki juzijuzi na yeye alimnyanganya Patrick Balidisya Mke wake. Cha ajabu hakuna hata adhabu wanayopata kwa Ushetani wao huo waufanyao. Ile Tanzania ina wanawake kibao na wazuri kama Lulu, ila bado tu waenda kumla mke wa mwenzio? Kama Minyama vile!! Lohh, haki ya nani!!!!!