The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Bulembo anafeli wapi? Ni miaka 7 no salary increase kwa visingizio kibao vya stiglaz na sgr kumbe sukuma gang wanapiga wakijinasibi kwamba ni zamu yao na wao ndio wanakura raha Sana..Karani katika halmashauri ya Muheza jijini Tanga, Saum Juma amesema ongezeko la mshahara lililotangazwa na Rais Samia Suluhu litawanufaisha kwa vitu vingi ikiwemo kununua viwanja, kujenga nyumba, kusomesha wadogo zao, kuwasaidia baadhi ya ndugu zao matumizi mbalimbali.
Akijitolea mfano yeye, kasema mshahara ukiongezeka ataweza kumjengea baba yake nyumba, kumnunulia gari kutokana na ongezeko hilo.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Muheza, Halima Bulembo amesema watumishi wa Wilaya ya Muheza wamemshukuru na kumpongeza Rais Samia kwa ongezeko la mshahara la 23.3%.
Halima Bulembo amesema yeye kama kiongozi wao watumishi walimfata na kumwambia kwa kuwa rahisi yeye kumfikia Rais, amfikishie salam zao kwani inatambulika watumishi walikuwa hawajaongezewa mishahara kwa miaka sita sasa na mama kawaongezea mwaka wa 7.
Watumishi wamesema wanamuombea Mama Samia kwa Mungu
View attachment 2228029
Saizi miradi inaenda na salary zimeongezwa.