Kardinali Pengo: Wanaomuita Rais Dikteta wajitafakari upya. Je, watoto kusoma bure na kujenga Hospitali ni udikteta?

Ngoja tuone...

Lazima asifie, la sivyo ataambiwa akaoneshe kaburi la bibi wa bibi yake bibi yake ili kuthibitisha uraia wake...

Cc: mahondaw
Kama tuna maRC na maDC wanajeshi wastaafu, kuna kosa gani Askofu mstaafu kusifia ili ateuliwe kuwa DC akingoja kuchaguliwa kuwa Papa? Wateule vijana wanamuangusha mteuaji labda ajaribu wastaafu maana hakuna mteule mwanajeshi aliyetenguliwa.
 
Mzee wetu ungenyamaza walaa usinge rudi kua padre ungendelea kua cardinal
Jua we ni kinywa cha wengi sana
Kuna watu umewadissapoint sana kuna watu umewafurahisha sana
 
Akili ikiwa nama-Pengo huwezi kuongea point... elimu bure sio kiashiria cha kutokuwepo udikteta! Enzi za Roma empire udikteta ulitwala hivyo sishangai huyumtu kutetea ukandamizwaji wa baadhi ya watu bila haya
 
Watalaam wa akili za wanadamu duniani eti wanasema ukishafika miaka 75 inakuwa mwisho wa kuwa creative yaani IQ yako imefikia kikomo then akili inaanza kurudi utotoni mdogo mdogo..!!
 
Kabla yake hospitali hazikujengwa? Watu hawakusoma bure. Ujenzi wa hospitali na elimu imeanza baada ya Magufuri kuwa rais mzee hebu jiheshimu.
 
Tanzania ni nchi ya hovyo sana. Yani viongozi wa dini hawaogopi kabisa kulaghai na kutetea mitumbo yao....sasa kama viongozi wa dini wenyewe hawamwogopi MUNGU, sisi tumuogope wa nini?
Mkuu usifuate mkumbo, hata kiongozi wa dini mbele za Mungu ni binadamu wa kawaida tu kama wewe!
 
Leo Katika kikao kilichoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na viongozi wa dini kardinal Pengo amemtetea dictator Mussolin aliyetawala Italia enzi hizo kama ifuatavyo

Mussolin aliondoa baa au balaa la Malaria Katika mji mdogo wa Italia, Kwa mujibu wa kardinal Pengo wakati huo malaria ilitishia maisha ya watu hapo Italia

Kuna mambo mazuri ya Mussolin na Hiltrer hayazungumzwi kwa mujibu wa kardinal Pengo

Pengo amesisitiza darasani watu hufundishwa Hiltrer aliua wayaudi zaidi ya Milioni sita lakini hawataki Kuongelea mazuri ya Hitler

Pengo ameiomba jamii itofautishe kati ya Dictate na neno dictator

Akijenga hoja kuhusu watu wanaomuandika mheshimiwa Rais kuwa ni dictator,amewaomba watafakari upya

Je, kujenga hospital ni udikteta? Amehoji kardinal Pengo

Je, watoto kusoma bure wao na wajukuu zao ni udikteta? Amehoji kardinal Pengo

Amepongeza uongozi wa Makonda kama moja ya watu vijana wanamsaidia Rais

Aidha Kardinal Pengo amesema alikuwa na hofu Rais wa sasa akimaliza muda wake nani atafaa na kufanya kama Rais wa sasa, Hofu imepungua kuona kuna vijana kama Makonda wanachapa kazi

Kardinal Pengo amesisitiza uwepo wa vijana wachapa kazi kama Makonda na wakijitokeza wengi hana shaka kabisa kazi za Rais zitaendelezwa vizuri

Kwa mujibu wa kardinal Pengo na Askofu mkuu mstaafu wa jimbo kuu la Dar es Salaam amesema haya mambo ya kumuita Rais dikteta anayasoma mitandaoni lakini pia kwa Uzee wake kuna watu wema wanampa taarifa nini kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii

Mwana Jamii Forum aitwaye "Barafu" ameelezea sana kwenye uzi mmoja jinsi Mussolin alivyoliteka kanisa wakati huo na kukandamiza Raia huko Italia

Hili la Hiltrer na Mussolin Nadhani ni elimu mpya kuwa kuna mambo mazuri walifanya

Tunaruhusu povu kwa wale wanaowalaumu viongozi wa kikatoliki, Kikubwa Wakatoliki kila jumapili kabla ya kuanza misa hutubu dhambi zao tofauti na wale wanaoanza kukusanya sadaka

====

Kardinali Pengo amewashangaa watu wanaomuita Rais wa Tanzania, John Magufuli dikteta na kueleza kuwa wanakosea.

Akizungumza leo Jumatatu Novemba 18, 2019 wakati wa mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini na Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda, Kardinali Pengo amesema kumekuwa na watu wanaozungumza maneno ya kupotosha kuhusu rais Magufuli.

“Katika mitandao kumezuka maneno kwamba Rais wetu ni dikteta. Hivyo yale anayoyafanya anashughulikia kuendeleza vitu kuliko kuendeleza watu.”

“Wanaongelea juu ya kushughulikia vitu kuliko watu, ni watu gani hao hawajashughulikiwa wakati mambo mengi yanafanyika kwa ajili ya watu,” amesema Kardinali Pengo

Kiongozi huyo wa kiroho amesema, “Ni lugha ambayo kwa akili zangu za kizee siwezi kuelewa, utakuwa unamshughulikia mtu kiasi gani kama unamfanya mtoto wake na mjukuu wake waende shule.”

Kardinali Pengo ambaye ni Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam amempongeza Makonda na kumtaja kuwa ni miongoni mwa wasaidizi bora wa Rais Magufuli.

“Nimefurahi, imenidhihirishia wewe ni kiongozi wa aina gani na tunamuomba Mungu atujalie viongozi wa aina yako wengi. Wewe (Makonda) ni mmoja kati ya wasaidizi bora wa Rais Magufuli.”

“Tunajiuliza baada ya Magufuli atakuwa nani ila mkiwepo wengi wa aina yako nisingekuwa na shaka ya kuwaza nani atafuata baada yake,” amesema

Chanzo: Mwananchi
MI HUWA nasikia mapadre wengi ni wasomi an usomi maana yake sio kuwa na vyeti vyenye GPA bali uwezo wako wa kutafakari na kudadavua masuala mbali mbali,kweli JPM kafanya mengi ila maendeleo gani yanaendana na ubaguzi,ubabe,hofu ba dhuluma,watu wamebomolewa nyumba ubungo kimara ujenzi hadi leo hujafanyika,wapinzani wanaishi kama watumwa ndani ya nchi yao,ukimkosoa wewe adui ukimsifia wewe rafiki,kwa nn hajiulizi kama anafanya mengi mazuri kwa nn uoga mkubwa,hajiamini ye kuvaa kijeshi tu,kutishia tu,kuwamaliza wapinzani tu,kwa nn kaogopa hadi uchaguzi wa s/mitaa kwa nn kama yuko at right kuna nn nyuma yake,huyu mzee nahc anavuna fadhila na akili ya usomi inapungua kwa kasi na akili ya uzee inaingia kwa kasi
 
Leo Katika kikao kilichoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na viongozi wa dini kardinal Pengo amemtetea dictator Mussolin aliyetawala Italia enzi hizo kama ifuatavyo

Mussolin aliondoa baa au balaa la Malaria Katika mji mdogo wa Italia, Kwa mujibu wa kardinal Pengo wakati huo malaria ilitishia maisha ya watu hapo Italia

Kuna mambo mazuri ya Mussolin na Hiltrer hayazungumzwi kwa mujibu wa kardinal Pengo

Pengo amesisitiza darasani watu hufundishwa Hiltrer aliua wayaudi zaidi ya Milioni sita lakini hawataki Kuongelea mazuri ya Hitler

Pengo ameiomba jamii itofautishe kati ya Dictate na neno dictator

Akijenga hoja kuhusu watu wanaomuandika mheshimiwa Rais kuwa ni dictator,amewaomba watafakari upya

Je, kujenga hospital ni udikteta? Amehoji kardinal Pengo

Je, watoto kusoma bure wao na wajukuu zao ni udikteta? Amehoji kardinal Pengo

Amepongeza uongozi wa Makonda kama moja ya watu vijana wanamsaidia Rais

Aidha Kardinal Pengo amesema alikuwa na hofu Rais wa sasa akimaliza muda wake nani atafaa na kufanya kama Rais wa sasa, Hofu imepungua kuona kuna vijana kama Makonda wanachapa kazi

Kardinal Pengo amesisitiza uwepo wa vijana wachapa kazi kama Makonda na wakijitokeza wengi hana shaka kabisa kazi za Rais zitaendelezwa vizuri

Kwa mujibu wa kardinal Pengo na Askofu mkuu mstaafu wa jimbo kuu la Dar es Salaam amesema haya mambo ya kumuita Rais dikteta anayasoma mitandaoni lakini pia kwa Uzee wake kuna watu wema wanampa taarifa nini kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii

Mwana Jamii Forum aitwaye "Barafu" ameelezea sana kwenye uzi mmoja jinsi Mussolin alivyoliteka kanisa wakati huo na kukandamiza Raia huko Italia

Hili la Hiltrer na Mussolin Nadhani ni elimu mpya kuwa kuna mambo mazuri walifanya

Tunaruhusu povu kwa wale wanaowalaumu viongozi wa kikatoliki, Kikubwa Wakatoliki kila jumapili kabla ya kuanza misa hutubu dhambi zao tofauti na wale wanaoanza kukusanya sadaka

====

Kardinali Pengo amewashangaa watu wanaomuita Rais wa Tanzania, John Magufuli dikteta na kueleza kuwa wanakosea.

Akizungumza leo Jumatatu Novemba 18, 2019 wakati wa mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini na Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda, Kardinali Pengo amesema kumekuwa na watu wanaozungumza maneno ya kupotosha kuhusu rais Magufuli.

“Katika mitandao kumezuka maneno kwamba Rais wetu ni dikteta. Hivyo yale anayoyafanya anashughulikia kuendeleza vitu kuliko kuendeleza watu.”

“Wanaongelea juu ya kushughulikia vitu kuliko watu, ni watu gani hao hawajashughulikiwa wakati mambo mengi yanafanyika kwa ajili ya watu,” amesema Kardinali Pengo

Kiongozi huyo wa kiroho amesema, “Ni lugha ambayo kwa akili zangu za kizee siwezi kuelewa, utakuwa unamshughulikia mtu kiasi gani kama unamfanya mtoto wake na mjukuu wake waende shule.”

Kardinali Pengo ambaye ni Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam amempongeza Makonda na kumtaja kuwa ni miongoni mwa wasaidizi bora wa Rais Magufuli.

“Nimefurahi, imenidhihirishia wewe ni kiongozi wa aina gani na tunamuomba Mungu atujalie viongozi wa aina yako wengi. Wewe (Makonda) ni mmoja kati ya wasaidizi bora wa Rais Magufuli.”

“Tunajiuliza baada ya Magufuli atakuwa nani ila mkiwepo wengi wa aina yako nisingekuwa na shaka ya kuwaza nani atafuata baada yake,” amesema

Chanzo: Mwananchi
Hoja za Kardinali ni hoja zake binafsi na Sio hoja za Kanisa, hivyo basi maoni yake yaheshimiwe kama mtanzania yeyote mwenye haki yakueleza mapendekezo yake.
 
Lkn anawafuasi na anawakilisha
 
Anaharibu sifa na heshima aliyojijengea kwa kukubali kuwa mpiga debe wa bashite ambae atowezafanikiwa dhima yake ya kuendelea kuwa kiongozi baada ya awamu hii.
 
Tungepata mtu kama Adolf Hitler au Musolin atuongoze Tanzania kwa miaka 20 nadhani tungeweza ongea lugha moja maana tumezoea fyokofyoko sana.

Tunahukumu ubaya wao kwa kusoma historia ambayo tuliandikiwa na muingereza kipindi wanatugombani. Tunafuata mkumbo wa kuwachukia kwa chuki ya kupandikizwa.

Kinachoshangaza zaidi mazuri yaliofanywa na Hitler na Mussolini hayasemwi.
NB: Magufuli anatosha kwani anauthubutu, hana porojo nyingi yeye ni utendaji. Aongezewe muda angalau 30 years inatosha.
 
Back
Top Bottom