Karen Nyamu Azomewa KICC: Hafla ya Endometriosis Yageuka Uwanja wa Kisiasa.

Karen Nyamu Azomewa KICC: Hafla ya Endometriosis Yageuka Uwanja wa Kisiasa.

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
Seneta mteule Karen Nyamu alikatizwa na kelele za “Wantam!” alipokuwa akihutubia mamia ya Wananchi, wengi wao vijana, waliohudhuria hafla ya Natalie’s Endometriosis Warriors (N.E.W) katika Ukumbi wa KICC, Nairobi, Jumapili.

Video kutoka hafla hiyo inaonesha baadhi ya waliohudhuria wakianza kumzomea Nyamu alipokuwa akizungumza, huku Seneta huyo akiendelea na hotuba yake licha ya usumbufu huo.

Seneta huyo alihudhuria hapo kuzungumzia endometriosis, suala ambalo amekuwa akilisukuma bungeni katika miezi ya hivi karibuni. Mnamo Agosti, Nyamu aliitaka Mamlaka ya SHA kuchunguza iwapo bima hiyo inagharamia ipasavyo gharama halisi za matibabu ya endometriosis, huku akitaka pia kuwe na takwimu za kitaifa, wataalamu zaidi na huduma maalumu kwa wagonjwa.

Hafla hiyo iliandaliwa na Mwanahabari na Mtangazaji Natalie Githinji, ambaye amekuwa akizungumzia hadharani safari yake ya kuishi na endometriosis, na ilikuwa na lengo la kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa huo na kuwakutanisha wanawake wanaougua.

Kwa hiyo, tukio la KICC limeleta picha mbili kwa wakati mmoja: jukwaa lililokusudiwa kuzungumzia afya ya wanawake likageuka pia kuwa jukwaa la kisiasa, huku baadhi ya waliohudhuria wakionyesha kutoridhishwa kwao na Nyamu.

Je, hii ilikuwa tu 'reaction' kwa Karen Nyamu kama Mwanasiasa, au inaonesha jinsi matukio ya kijamii yanavyozidi kuwa maeneo ya Wananchi kuonesha hisia zao za kisiasa?
 
Back
Top Bottom