Karia uongozi wa TFF umemshinda huo ndo ukweli

Karia uongozi wa TFF umemshinda huo ndo ukweli

Kila aina ya ujinga muufanyao anaangushia yeye, huoni rundo la mazuri yake au watu mnayo maradhi ya asili yasiyotibika
Mazuri yanafanywa na GSM na Mo na Magoli ya Mama , wengine ni wasindikizaji tu, na kujinufaisha binafsi
 
Kwakua viongozi waliopita, nani amekua na mafankio zaidi ya karia kiasi cha sisi kutupatia ujasiri wa kumkataa?
Mafanikio yameletwa na Goli la Mama na wadhamini wa hizi timu , hao tiefef wao ni maslaha binafsi
 
Kila aina ya ujinga muufanyao anaangushia yeye, huoni rundo la mazuri yake au watu mnayo maradhi ya asili yasiyotibika
Hatoshi hana uwezo wa kutatua migogoro,

Malalamiko ama migogoro inatakiwa ipatiwe ufumbuzi sahihi na kwa Wakati, (at a desired time)

Lack of crisis management skills
 
Mafanikio aliyoyapata ni kwa sababu tu dunia imebadilika kwenye afcon zamani ilikuwa ni nafasi 16 ila sahivi ni 24 ndo maana inakuwa ni rahisi kwa sisi kufuzu

Kwenye club bingwa hivyo hivyo wanapanga based on merits zaman timu ya Tanzania kwenye mtoano tu lazima upangiwe al ahaly ndo maana timu kufika makundi ilikuwa ngumu

mfano kwenye mziki msanii wa leo atakua na mabadiliko zaidi ya wazamani kwa sababu hategemei redio apate ela kuna vyanzo vingi sana vya kuingiza fedha

Karia
Sasa hayo mabadiliko si yapo kwa nchi zote mbona Afcon iliyopita majirani zetu wote Kenya,Uganda na Rwanda hakuna aliyefuzu
Ligi ya Tanzania ni ya 6 kwa ubora barani Africa ikizidiwa na ligi moja tu ya South Africa ukiachana na ligi nne la kiarabu zinazoizidi hayo mafanikio yote ingekuwa ni kwasabu uliyoitoa kwanini isiwe kwa Zambia,Zimbabwe,Malawi,Kenya au Uganda iwe Tanzania tu? Nani hajui miaka kadhaa tu nyuma ligi za Zambia,Congo,Guinea hata Zimbabwe zilikuwa zimeiacha hii ligi mbali sana ikiwa si miongoni hata mwa ligi 30 bora barani Africa leo tupo wapi?
 
Mpira wa Tz hauwezi kukua hadi timu ya Yanga na followers wake waaadhibiwe kwa uhuni wanaofanya mara kwa mara, Simba wanafanyiwa fujo nyingi sana yule mkuu wa mkoa wa mwanza nae kisa ni shabiki wa yanga alienda kuwafanyia simba fujo mazoezini.

Jana tena simba kafanyiwa fujo na mabaunsa wa Yanga , bado mambo mengi Yanga wanafanya ikiwepo upangaji wa matokeo kuna timu huko singida iliamua kupanga kikosi ambacho siyo cha ushindani ili kupanga matokeo yanga ishinde, ujinga kama huu ndo maana Yanga inaishia kucheza ligi ya ndani tu kimataifa itaendelea kuwa na maisha magumu sana
Pamoja na kupewa penalti za mchongo na wapinzani kupewa red cards za ajabu kuwadhoofisha, bila refa kuchukuliwa hatua.
 
Kiukweli ukiangalia matukio mengi ya mpira kwa Tanzania chanzo ni uongozi mbovu tunafanya mambo kwa kubembelezana sana hakuna professionalism kabisa

Ligi ya series A wanaadhibu timu bila kujali ukubwa juventus walishashushwa daraja na ac milan kukatwa point

Mpira wetu ili uendelee tunatakiwa tuache kubembelezana na unafki na hii tabia ya unafki inatufanya hata kupiga vita umaskini inakua ngumu sana

Kama kweli tunataka mpira wa Tanzania ufike mbali karia hafai kuendelee kuwa kiongozi

Sahivi kuna timu mbili watu wanajiamulia watakavyo lazima watu waambiwe bila wao ligi itachezwa tu tuache mambo ya kubembelezana
Hapo amesha lobby kuongeza muda wakae hadi Afcon 2027.....yuko radhi kuua mtu au watu abakie hapooo ....
 
karia hathamini mpira anauchukulia kama vile kazi ya kihuni na kitoto, hapa tz mpira na mziki ni kazi zisizo thaminiwa kabisa ndo mana anaweza kuamua vyovyote na hakuna wa kufanya chochote coz ata mashabiki wake wenyewe ni wale wale tu
 
Back
Top Bottom