Karia: Wanaosema Bodi ya Ligi ijiuzulu timu zao uongozi upo sawa?

Karia: Wanaosema Bodi ya Ligi ijiuzulu timu zao uongozi upo sawa?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
753
Reaction score
1,699
1742141059575.jpeg

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace amejibu tuhuma wanazoshushiwa bodi ya Ligi kufuatia uamuzi wa kuahirisha mchezo wa Kariakoo Derby uliopaswa kuchezwa Machi 8, 2025.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha redio, Rais Karia amedai kuwa Bodi iachwe ifanye kazi yake na kubainisha kuwa walisimamia na watasimamia kanuni na sheria inavyopaswa lakini kwa wanaosema bodi hiyo itenguliwe je wao uongozi wa Timu zao upo sawa?

“Taratibu tuziache zifuatwe, Lakini huwezi kusema bodi ijiuzulu. Hata wanaosema wawaambie na viongozi wao, hawastahili kujiuzulu? Vitu vingine vinafanyika kitoto, Kama watu wamechoka kucheza mpira basi wakaendelee na Sinema zao.”——amesema Karia

 
Sheria, kanuni na miongozo ndiyo pekee itaamua hatma ya mechi ile.
Kanuni inaruhusu timu ngeni kufanya mazoezi katika muda ambao mechi itapaswa kuchezwa. Je! Muongozo unasemaje katika kuifafanua kanuni hii?

Ndiyo! Timu ngeni ilikosa fursa hiyo ya kikanuni. Je! Kanuni inasemaje kuhusu timu ngeni kususia mechi kutokana na kukiukwa kwa kanuni ya kwanza hapo juu!?

Natambua ukiukwaji wa kila kanuni una adhabu yake stahiki. Acha mvua izidi kunyesha ili tuone panapo vuja.
 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace amejibu tuhuma wanazoshushiwa bodi ya Ligi kufuatia uamuzi wa kuahirisha mchezo wa Kariakoo Derby uliopaswa kuchezwa Machi 8, 2025.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha redio, Rais Karia amedai kuwa Bodi iachwe ifanye kazi yake na kubainisha kuwa walisimamia na watasimamia kanuni na sheria inavyopaswa lakini kwa wanaosema bodi hiyo itenguliwe je wao uongozi wa Timu zao upo sawa?

“Taratibu tuziache zifuatwe, Lakini huwezi kusema bodi ijiuzulu. Hata wanaosema wawaambie na viongozi wao, hawastahili kujiuzulu? Vitu vingine vinafanyika kitoto, Kama watu wamechoka kucheza mpira basi wakaendelee na Sinema zao.”——amesema Karia
Tunaotaka mjiuzuli ni sisi washabiki tunaowawezesheni kupata tuposho,tumshahara na tu garama twa kuwezesha kampira ketu kaendelee kuelea na nyie angalao mwendelee kupatapo tusifasifa hata kama twa uongouongo.
 
Ni aibu sana kuwa na kiongozi mkubwa mwenye akili na hoja za darasa la saba b!! Yani mi nikikosea nisisemwe kwa kuwa na nyie kule mmekosea!! Kila kosa liadhibiwe kwa nafasi yake! Wajumbe ni makolo wahed hawana sifa , watoke waje wengine mpira wetu uende mbele!!

Hebu weka video tuone kama kweli kasema.
 
.... Je! Kanuni inasemaje kuhusu timu ngeni kususia mechi kutokana na kukiukwa kwa kanuni ya kwanza hapo juu!?
Hadi sasa hakuna timu iliyosusia mechi ile, maana kabla ya muda wa kick off mamlaka zikazuia mechi kufanyika. Huwezi kujua kama ni mind game au serious hadi muda wa mechi ufike. Bodi ilitoa maamuzi yanayojitegemea kwa kuwa kanuni zinaipa mamlaka ya kupanga ratiba. Hata Yanga ilivyotoa tamko kwamba haitacheza mechi nyingine, hiyo kauli sio ya kuichukulia serious hadi muda wa tarehe ya mechi utakapofika na kupita
 
Back
Top Bottom