Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 753
- 1,699
Huyu hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumiTwo wrongs don't make a right. Kama kuna janja janja kwenye uongozi wa timu nyie kama wasimamizi mlitakiwa kuchukua hatua sio kufumbia macho ili na nyie mkileta janja janja msiguswe.
Tunaotaka mjiuzuli ni sisi washabiki tunaowawezesheni kupata tuposho,tumshahara na tu garama twa kuwezesha kampira ketu kaendelee kuelea na nyie angalao mwendelee kupatapo tusifasifa hata kama twa uongouongo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace amejibu tuhuma wanazoshushiwa bodi ya Ligi kufuatia uamuzi wa kuahirisha mchezo wa Kariakoo Derby uliopaswa kuchezwa Machi 8, 2025.
Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha redio, Rais Karia amedai kuwa Bodi iachwe ifanye kazi yake na kubainisha kuwa walisimamia na watasimamia kanuni na sheria inavyopaswa lakini kwa wanaosema bodi hiyo itenguliwe je wao uongozi wa Timu zao upo sawa?
“Taratibu tuziache zifuatwe, Lakini huwezi kusema bodi ijiuzulu. Hata wanaosema wawaambie na viongozi wao, hawastahili kujiuzulu? Vitu vingine vinafanyika kitoto, Kama watu wamechoka kucheza mpira basi wakaendelee na Sinema zao.”——amesema Karia
Hadi sasa hakuna timu iliyosusia mechi ile, maana kabla ya muda wa kick off mamlaka zikazuia mechi kufanyika. Huwezi kujua kama ni mind game au serious hadi muda wa mechi ufike. Bodi ilitoa maamuzi yanayojitegemea kwa kuwa kanuni zinaipa mamlaka ya kupanga ratiba. Hata Yanga ilivyotoa tamko kwamba haitacheza mechi nyingine, hiyo kauli sio ya kuichukulia serious hadi muda wa tarehe ya mechi utakapofika na kupita.... Je! Kanuni inasemaje kuhusu timu ngeni kususia mechi kutokana na kukiukwa kwa kanuni ya kwanza hapo juu!?
Kwamba ulitaka barua ya Simba ijibiwe baada ya mechi? Akili umeziweka wapiMaajabu ya soka la tanzania!
Simba wameandika barua masaa matano tu kikao kimeitishwa kujadili swala lao!
Ila barua ya yanga Leo siku ya nane haijatolewa majibu! Hiyo tu inatosha kujua nani anabebwa.