Kariakoo Derby: Simba SC 2 - 2 Yanga SC | Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara - Uwanja wa Taifa Dar

Kariakoo Derby: Simba SC 2 - 2 Yanga SC | Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara - Uwanja wa Taifa Dar

Simba pumzi imezima,hawa simba sio wa kutufunga sisi.Yanga hebu waongeze la tatu tumalize kazi.
My love nimetoka taifa nipo hoi..ukweli lazima niusema...congrats my love
 
Mpira ni matokeo matatu lakini kwa simba hii na pesa walizowekeza vitu viwili tofauti CAF CHAMPIONS LEAGUE KILEMA ,kwenye VPL nako uwezo mdogo tunashinda sababu tunacheza na timu dhaifu, HOJA SIO MATOKEO HATA MPIRA NI KONOKONO NO MIPANGO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati homa ya mchezo wa Watani wa Jadi, Simba na Yanga ikiendelea kupanda huku zikiwa zimebaki saa chache, Mashabiki na Wachezaji wa timu hizo wameendelea kutambiana kuibuka na ushindi

Simba ambayo itakuwa mwenyeji, itaikaribisha Yanga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar leo majira ya saa 11:00 jioni


Takwimu za timu hizo zinaonyesha safu zao za ushambuliaji zimekuwa na makali dakika 45 za kipindi cha pili ingawa Simba inaonyesha iko vizuri pia dakika 45 za mwanzo

Simba katika mechi 10 zilizopita imefunga magoli 10 kipindi cha pili na katika kipindi cha kwanza imefunga magoli 10 huku ikiruhusu goli moja katika kipindi hicho cha kwanza

Yanga nayo imekuwa moto kipindi cha pili kwa kufunga magoli 8 lakini imeruhuru magoli matano na katika Kipindi cha kwanza imefunga magoli 6 na kuruhusu kufungwa magoli matatu

Nitakuwa nikiweka hapa yanayojiri yote moja kwa moja kutoka Taifa-Jijini Dar

UPDATES
View attachment 1312092
Mwamuzi wa Mchezo wa leo ni Mwana Mama, Jonesia Rukyaa

View attachment 1312093
Mashabiki wa timu zote mbili wameanza kuingia uwanjani huku mchezo huo ukitarajiwa kuanza majira ya saa 11:00 jioni

View attachment 1312091
Baadhi ya Mashabiki wa Yanga Wakiwa ndani ya Uwanja tayari
UPDATE YA VIKOSI
View attachment 1312186
Kikosi cha Simba kitakachopambana na Yanga leo Januari 04

View attachment 1312204
Kikosi cha Yanga dhidi ya Simba leo Januari 04​

Simba inapata goli la kuongoza kupitia kwa Meddie Kagere
Klabu ya Simba inapata goli la kuongoza dhidi ya Klabu ya Yanga kupitia goli lililofungwa na Meddie Kagere katika dakika ya 42

Goli la Simba limepatikana kupitia mkwaju wa penati baada ya Meddie Kagere kuchezewa rafu na Beki Kelvin Yondani ndani ya eneo la hatari


======

MICHEZO: Klabu za Simba na Yanga zimeshindwa kutambiana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar baada ya timu hizo kutoka sare ya goli 2-2 katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Simba inapata goli la kuongoza kupitia penati ya Meddie Kagere katika dakika ya 42 na goli la pili la Simba lilitungwa na Deo Kanda katika dakika ya 47

Goli la Kwanza la Yanga lilifungwa na Balama Mapinduzi katika dakika ya 50 huku goli lake la pili likipatikana baada Mohamed Hussein kujifunga katika dakika ya 53
View attachment 1312394
Screenshot_20200104-190514.png


WALIOOONAAA HIII POST.MMELEWAA EEH
TUMEANZA NA LIV 2-0

LEO SIMBA DRW 2-2
Screenshot_20200104-190514.png
 
Yanga let us go,huyu Manula tukampe salaam tena.Simba walipewa penalt hawa .Yanga tumalize hii mechi na ushindi.
Haya uende unyonyeshe sasa..matokeo si ushayaona? Na uache kelele maana hasira zangu huwa nazihamishia kwenye show sasa usije kuungama tena usiku!
 
Back
Top Bottom