Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Hahaha
Kariakoo wwtakuroga mdomo ukae upande.

Umewasagia kunguni bila kuwwonea
 
Ni kweli bei ya vifaa vya ujenzi kariakoo na tegeta ni sawasawa .. nilishangaa sana nyavu za madirisha gerezani na tegeta kwa mpemba sawasawa..
 
Na hii ingekuwa fursa kwa mji wa Dodoma, wafanyabiashara wengi wa nje (land locked countries) wanapita Dodoma.

Mimi ningekuwa Waziri wa viwanda biashara ningefanya yafuatayo ili lengo la kupanua miji na hasa jiji la Dodoma litimie ningefanya yafuatayo:

1. Kupromote wafanya biashara kuwekeza biashara zao Dodoma.
2. Kupromote nchi za jirani kuchukua mizigo Dodoma
3. Ningeweka punguzo la ushuru kwa mzigo wowote unaotoka nje na kushushwa Mkoa wa Dodoma (hii ingechochea magodown na stoo nyingi kujengwa Dodoma ili wapokelee mizigo yao.
4. Ningeongea na vyombo vya usafiri hasa treni waweke miundo mbinu rafiki na bei ya chini sana kwa mzigo unaosafirishwa kutoka Dar es salaam kavu au bandarini kuelekea Dodoma
Kwa kufanya hivi ni ndani ya miaka mitatu Dodoma ingefurika wafanya biashara wa nje na Mikoa ya ndani na hivyo kuacha Mkoa (katikato ya nchi) ujijenge na kujitangaza wenyewe bila nguvu.

Asante
 
Wanatafuta maisha kwa kuongeza bei za bidhaa?ivi hii ni akili?
Kwani kwenye biashara unapataje faida unajua wewe ni kilaza
Hata ukiwa na duka bidhaa uliyonunua kwa bei ya jumla lazima uongeze bei ili upate faida hii iko kwa wote sio kwa winga tu
 
Inakwaza sana mteja nimekuja mwenyewe dukani mawinga zaidi ya 3-5 wanaanza kunibuguzi buguzi mteja nilie jileta kwenye Duka hii hapana.
All the best
 
Ni kweli bei ya vifaa vya ujenzi kariakoo na tegeta ni sawasawa .. nilishangaa sana nyavu za madirisha gerezani na tegeta kwa mpemba sawasawa..
Ndo maajabu ya Kariakoo ya Sasa
 
kinachonikera zaidi ni kila unapokwenda ni vifaa vya kichina tu, yani ni ma copy kwenda mbele
 
Sijuhi nianzishe Uzi mpya WA mafundi ujenzi wanavyojifanya mawinga WA wauza matofari.....ukiwa na kiwanda cha kufyatua tofari usipowapa kazi ya uwinga mafundi ujenzi biashara inakufia ...kibaya zaidi wanakushawishi wewe mjenzi ukanunue matofari "biscuit" mradi wanapata kamisheni yao.
Hii nchi tuna laana sio bure!
 
KATORO-Geita uhakika
 
Niliishawahi kuliongelea hilo
 
Ni suala la MUDA tu...nani aliwaza suala la ticket MTANDAO za mabasi ya masafa marefu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…