Kariakoo: Nimenunua Raba kali kinoma kwa 15,000/=. Madukani huwa naona zinauzwa 70,000/=

Jamani tuwe na shukhurani maana zamani kuvaa kiatu au raba mtoni lazima uwe na ndg nje ya Nchi ili akutumie,au vaa mi chachacha zako! Maendeleo Tz yamekuja kwa kasi sana!!
daah umenikumbusha mbali sana na hizo chachacha...ndo zilikuwa pigo zenyew enzi hizo ila ngoja jua liwake ndo utaona moto wake. asante mzee rukhsa kuifungua nchi. hii nchi tuwashukuru sana hawa wa pandeipi ya pili ya bahari
 
Hiyo raba imitation, huoni haina hata brand name? Made in China streets. Kitu halisi hupati kwa hiyo bei, na ujue kuna feki na original
 
Umepigwa bro hii ndula bei buku nane tu
 
Mtaani kwetu kama hizo wanauza buku Mbili,,,muuzaji kafurahi kweli kapata fala wake
 
Ila ngozi nyeusi tu ndio tunajali mambo ya Og ila wazungu huwa hawajali kabisa wacheki raba zao hasa wale wanaotembea na mibegi mikubwa utakuta kavaa simpo tu na raba hata designer hajulikani hahah!
 
Viatu vya watoto.... Ni tsh 5000 ikizidi tsh 7000
 
Ila ngozi nyeusi tu ndio tunajali mambo ya Og ila wazungu huwa hawajali kabisa wacheki raba zao hasa wale wanaotembea na mibegi mikubwa utakuta kavaa simpo tu na raba hata designer hajulikani hahah!
Mi nawaonaga wanavaa midosho wanapendeza kinoma ,kiuhalisia vaa midosho hamna mtu atajua then uwe navyo vingi maana hazidumu kuliko raba moja og umenimunua laki na kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…