Kaveli
JF-Expert Member
- Dec 4, 2012
- 5,443
- 8,903
Sawa mkuu mzani umebalance
Mkuu Half american , hii ID yako kila nikiiona hunikumbusha sana Life struggles zangu downtown Kinondoni, back in ze day... maisha ya road, mid to late 2000's.
Kulikuwa na daladala (coaster) yakuitwa 'HALF LONDON' na mpinzani wake mkubwa wa kuitwa 'MWENDO WA LUBEYA'... hizi ndizo daladala zilizotamba sana route ya UBUNGO to DRIVE INN (via Shekilango road, Kawawa road) miaka hiyo ya mid/late 2000.
Katika route hiyo, hizo gari mbili ndizo zilikuwa 'pamba nyepesi'... yaani very neat nje & ndani, mziki mkubwa, suka & konda wote mabishoo, halafu mwendo wa shilingi a.k.a iende irudi. 😎
Hakika huwa napata good memories sana nisomapo ID yako. Live long mkuu HALF AMERICAN.
Samaleko Kinondoni. Samaleko Mzizima. 😎
-Kaveli-