Rjx
Member
- Oct 20, 2024
- 5
- 11
Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza ujenzi.
- Hakikisha unakiwanja ambacho kimepimwa na kinatambulika na manispaa ya mji...kuepuka migogoro.
- Katika kiwanja unachotaka kuanza ujenzi Hakikisha unatambua upitaji wa barabara(access roads) na mpango mji , kwa mfn kuna maeneo ambayo ni maalum kwa ajiri ya ujenzi wa majengo ya makazi, majengo ya viwanda, majengo ya kibiashara, ya ki-serikali n.k.
- Kabla ya kuanza ujenzi Hakikisha unakuwa na Ramani za ujenzi ikiwezekana pamoja na Gharama zake...Na hakikisha zinapita manispaa ya mji kwa ajiri ya uhakiki na usalama wako wa ujenzi.....Epuka ujenzi wa Ki-mazoea tafuta mtaalam wa ujenzi.
- Kabla ya kuanza kuchimba mashimo kwa ajiri msingi ni lazima kuacha mita moja nusu 1.5 mita kutoka kwenye bikon ya kiwanja chako kwa kona zote.