Michael Uledi
Senior Member
- Mar 29, 2023
- 132
- 323
Ukiniambia nikae mbele ya TV asubuhi mchana usiku kwa ajili ya kumuangalia Military GENIUS General Paul Kagame siwezi kuchoka wala kusita! Sikatazwi kusema Paul ni mmoja ya viongozi bora wa kizazi chake kuwahi kutokea Africa na duniani!
Sifa kubwa ya Ofisa yoyote wa Jeshi ni kuwa na ujeuri kutoka ndani ya kichwa na hata moyo wake kwamba anaweza kufanya chochote chini ya dunia hii!Ofisa wa Jeshi training yake "inamuinject" uwezo wa kufanya jambo au shughuli yoyote kwa usahihi,uharaka na ubora wa viwango vilivyotukuka!
Ujeuri huo unapatikana kupitia kwa mafunzo maalum "sequntial planned activities"yenye kuvujisha damu na jasho wakati wote wa mafunzo na mwisho wa siku ndio maana unaona wanajeshi wengi"Ofisa" ni watu kufanya kitu kwa matokeo na ubora usiotiliwa shaka!
General Paul kagame yupo katika mpango wa kufa na kupona wa kuifanya Rwanda kuwa Taifa kubwa Afrika kabla ya mwaka 2050 na bahati nzuri wanyarwanda wanamuelewa vizuri sana ndio maana hakukuwa na kelele zozote pale mapendekezo ya kubadilisha Katiba ili Paul aongezewe muda wa kuingoza Rwanda!
Kiongozi wa ngazi ya Paul lazima uwe na maono yasiyofutika kichwani kuhusu aina gani ya Taifa ambalo unataka kulitengeneza lakini zaidi lazima ujue wazi kabisa kuwa maslahi ya Taifa lako yanapatikana kwanza ndani kwako na zaidi kwa jirani yako! "Imperialism".
Mimi pia ni muumini wa kuyatafuta maslahi ya Taifa langu kwenye mipaka ya watu wengine zaidi!Uwezo wa Taifa kutoka katika mipaka yake na kwenda "kumtongoza" jirani ndio sifa kubwa ya Paul Kagame!Paul ndani ya muda mfupi kashafanya ziara nyingi barani Afrika labda kuliko Kiongozi yoyote wa kitaifa barani humu!
Paul ni muumini pia wa falsafa ya Uongozi na kijeshi ya "kucheza mpira" kwenye eneo la adui zake!Paul aliwahi kunukuliwa akisema kuwa yeye anapigana vita ndani ya mipaka ya adui zake!Ujeuri wa Paul Kagame tulimpa wenyewe pale Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha"Cadet Course" moja kati ya eneo ambalo mimi mwenyewe naliheshimu sana na kulijua vizuri!
Nina mengi ya kusema kuhusu Paul Kagame,lakini niseme tu heshima yako Afande General Paul Kagame!
Nataka ujue kuwa Mimi ni mmoja wa waumini wa Uongozi wako!Kila hatua unayopiga wewe binafsi na Taifa lako la Rwanda naiangalia kwa umakini mkubwa kwa maslahi ya Tanzania yangu ya kesho!
Paul najua aina ya Rwanda ambayo ipo kichwani kwako,hata Mimi pia nina Tanzania yangu kichwani kwangu!Namuomba Mungu siku nipate nafasi hiyo ya kuijenga Tanzania ambayo ipo kichwani kwangu!Ninayo Tanzania yangu ninayo mchoro wa ramani yangu ambayo ni kuifanya Tanzania kuwa Taifa kubwa Afrika!
General Paul Kagame, Mimi George Michael Uledi na wewe tunatembea katika ndoto moja labda kwa vile tumewahi kuishi pale "Nengungu".
I salute you afande GENERAL Military Genius,Paul Kagame of Kigali!
+255746726484.
Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app