Mmeletewa miradi wa Bomba la Mafuta cha ajabu Tanga hakuna vijana wallioenda shule wanaaoweza kucompete na soko la ajira, Mbunge wenu yupo hamumwambii hata awasaidie special programes za vijana ili walau operation ikianza basi muweze hata kupata ajira.
IT zinatoka hapo zinakwenda DRC, Burundi, Malawi, bonded Dar es salaam vijana wa Tanga mnapiga soga na hizo kazi zinafanywa na vijana wa temeke na kurasini Dar.
Bandari imeanza kuchangamka lakini wenyeji ni kama hawajui kinachoendelea wageni wanakuja wanapiga mishe wanaondoka.
Uchumi Tanga uko kwenye mikono ya wahindi, waarabu, wachaga, wapare na wasambaa wenyeji mmegeuka kuwa wapambe/machawa na makuwadi wa waarabu na wahindi kazi hakuna.
Mzunguko wa hela hakuna, wenyeji hawana direction ya maisha, vijana wadogo wakike na wakiume wamekaa majumbani hawaendi shule na hakuna muamko wakupeleka watoto shule au kuwekeza kwenye elimu, matokeo yake mabinti wengi wadogo wamebaki kujiuza hapo maeneo ya chichi, Sabasaba, Benbistro na wengine wanatega Tanga beach resort.
Sidhani kama mna sababu yeyote yakuishabikia CCM Tanga, maana CCM ndio imeua uchumi wa Tanga na hakuna juhudi zozote strong kuifanya Tanga kuwa strong economically kupitia resources zake.
Umeongea mengi mno kwa kujikita katika tabia za vijana wa Tanga....sasa CCM ndio iliyowafanya wawe na tabia hizo ?!!
CCM hiyohiyo haijawapa uvivu hao wachaga uliowataja.....
CCM hiyohiyo haijawapa uvivu WAPARE uliowataja.....
CCM hiyohiyo haijawapa uvivu WASAMBAA uliowataja.....
CCM hiyohiyo haijawapa uvivu WAARABU NA WAHINDI uliowataja.....
Tena ukawasifu vijana wa TEMEKE na KURASINI kwa kutokubali "kupewa uvivu" na hiyo CCM....mkuu hebu kuwa serious kidogo ,ha ha ha ha
Kazi kubwa ya serikali ya CCM ni kuujenga uchumi wa jiji la Tanga....
Bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda mpaka "udigoni" Chongoleani ni fursa adhimu kwa vijana wenzangu wa Tanga......kusuka ama kunyoa ni kwao wao wenyewe.....
Kule Mwambani kutakuwa na bandari kubwa mno.....kusuka ama kunyoa ni kwa maswahiba zangu hao wa Chuda ,Chumbageni ,Ngamiani ,Raskazone ,Chumvini , Central-Majestic ,Chumbageni Twiga mpaka Mtupie , barabara za namba,magaoni na Mikanjuni....
BTW si mabinti wa Tanga tu wanaouza "nyaaap" hapo chichi ,Sabasaba na kutega kule Sahare Tanga Beach Resort.....nchi nzima hii baadhi ya MABINTI "wanatega kuuza...".
Humo ndani utakuta wasomi wa vyuo vikuu mpaka makazini.....
Kwa hiyo usitake kuwachafua akina Zaituni ,Mwanamkasi ,Mwamvita,Sikudhani,Libe ,Dori,Zainabu ,Rukia wa huko Duga ,Bombo Area na Kisosora ,ha ha ha ha ha
#Mama Samia apendwa mno huko Tanga !
#JMT milele dumu !!