Karibuni - Application HESLB (Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu)

tatanyengo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2011
Posts
1,133
Reaction score
280
Watanzania waliokuwa wanasubiri kwa hamu na gamu kutuma maombi ya kupata mkopo ili kuweza kusoma katika vyuo vya elimu ya juu muda umewadia.

Maombi yataanza kupokelewa siku ya Jumatano tarehe 1/5/2013. Jiandae kwa kuweka kumbukumbu zako vizuri. mfano vyeti vya masomo ukizingatia kwamba namba za mtihani wa kidato cha Nne (Form Four) hutumika kwa utambulisho wa mwombaji.

Kila la kheri waombaji.
 
Maombi ni kuanzia tarehe 1/5/2013 hadi tarehe 30/6/2013 kwa waombaji wapya na wa zamani. Waombaji wapya watalipa Tsh.30,000/=. Wale wa mwaka wa Tano na Sita watalipa Tsh.10,000/=

Waombaji wanaosoma mwaka wa Pili, Tatu na Nne ambao walilipa ada ya maombi tsh.30,000/= mwaka wa masomo 2009/2010, 2010/2011 na 2011/2012 hawatakiwi kulipa ada tena.
 
Asante, tangazo lao nimeliona jana tbc1 ila kwenye web yao mpaka sasa hakuna taarifa yoyote juu ya application, wenda wakaweka hiyo 1/5/2013
 
Wa mastars je?

Waombaji wa Masters na PhD wawe ni wahadhiri katika vyuo vikuu.

Sifa za mwombaji ni:
1. Awe ni raia wa Tanzania
2. Awe amedahiliwa katika chuo cha elimu ya juu.
3. Awe hana njia nyingine ya kugharimia elimu ya juu.
4. Awe amefaulu masomo mwaka uliotangulia (kwa wale wanaoendelea na masomo).
5. Awe ni mhitaji.
 
Asante kwa taarifa,nauliza mwenye diploma ya ualimu na akaamua kujiendeleza kuchukua degree ya elimu lakini ameomba tcu kwa vyeti vya form six. JE anaweza kupata mkopo huyu kweli? Heshima kwenu jf
 
je na sisi 2naoingia mwaka wa pili ambao hatukupata mkopo inakuje kuhusu viambatanisho na hiyo elfu thelathini
 
sasa cc 2lioko vyuoni 2tasahiniwa na nani ile sehemu ya sahihi za wenyekiti wa mitaa na sehemu ya mzazi au mlezi?
 
sasa cc 2lioko vyuoni 2tasahiniwa na nani ile sehemu ya sahihi za wenyekiti wa mitaa na sehemu ya mzazi au mlezi?

hapo sasa, cna uhakika inaezekana hiyo option haipo kwa walio vyuoni na kama ipo basi ni lazima kurudi kuzifuata hizo signature
 
samahani unaweza ku2orodheshea baadhi ya viambatanisho muhimu????
 
How can I sent my application for loan, i am first year student at Mzumbe University. What i need to know is procedure for application because i was selected through mature entry 2011.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…